Menu

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo

Thursday, November 27, 2014

Fahamu Siri ya Namba Kiroho




Fahamu Siri ya Namba Kiroho

NAMBA NA MAANA ZAKE KIBIBLIA.

Utanguizi.
Tunapoendelea kujifunza maneno ya Mungu, Leo nimepewa fulsa ya kujadiliana kuhusu Namba ndani ya biblia na maana yake katika maisha yetu ya kimwili na Kiroho hapa Duniani..Namba ndani ya biblia zimewekwa na Mungu na tunatakiwa kuziangalia kwa umakini wake sana kama vile maneno(text) tunavyoyatumia.Tumepewa na Mungu kanuni ya kulinganisha mambo ya Kiroho na Roho(1Wakoritho 2:13) Na inatuonesha ya kwamba Biblia na yaliyomo ndani yake ni sehemu ya mambo ya Kiroho.Na tunajua ni lazima tutafute na kujua kwa namna gani Mungu anazitumia namba. Biblia ni kitabu sahihi kabisa hakina makosa wote tunafahamu na yamevuviwa na Mungu (pumzi ya Mungu). Vilevile Namba ni sehemu ya Maneno kwa maana nyingine tunasema ndani ya maneno kuna namba. Mungu ameweka maneno yake ndani ya biblia kiasi kwamba hata mtoto mdogo wa miaka 6 anaweza kuelewa kwa usahihi kabisa kama mtu mzima kama Mungu anavyotaka. Ni kweli Biblia ni kama msitu unaweza potelea huko na usiweze kuelewa lakini kwa msaada wa Roho mtakatifu tunaweza kuelewa ukweli wote wa biblia (Mark 4:11-12;Mithali 25:2;1Wakori. 2:11-14).
Jambo la msingi hapa ni lazima uelewe kwanza kwamba Namba ni maneno (Numbers are words) ndipo utakapo zitumia namba vizuri bila shida kama maneno.

Sasa kwa nini kwa nini  ? Ni kwa ni nadra sana kuona somo hili likifundishwa
Si kwamba namba zote ndani ya biblia zina maana flani ila kwa madhumuni maalum kwa mfano;

1              .Namba zinaweza kutumika katika kupima muda (Kutoka 12:40)
  1. Namba zinaweza kutumika kuelezea kundi fulani la watu,madhumuni mbalimbali na nk(1petro 3:20).
  2. Namba zinaweza kutumika kupima kitu Fulani(Mwanzo 6:15).
  3. Namba zinaweza kutumika kwa maana Fulani na kwa wakati huohuo maana ya Kiroho au Alama Fulani(Yohana 21:11) samaki 153 waliovuliwa hawa ni samaki halisi waliovuliwa lakini Namba 153 pia ina maana maalum Kiroho lakini imejificha sana kwenye uelewa wetu.
  4. Kwa wakati mwengine namba zinaweza kuwa na maana ya kiroho au alama Fulani yenye kutambulisha kitu Fulani.
Kwa mfano ,Petro alimuuliza Yesu ni mara ngapi mtu akikukosea unaweza kumsamehe hata mara saba?(Mathayo 18:21)
Na yesu akajibu sio mara saba tu lakini hata sabini mara saba. Sasa 70 x 7 = 490 je Yesu alifundisha tusamehe mara 490 halafu tuwache kumsamehe mtu? Na tunajua Yesu alitufundisha tuwasamehe watu kama yeyey alivyotusamehe sisi bure, Na tunafahamu ya kwamba Yesu hakusamehe mara 490 pale msalabani.Alipokufa pale msalabani alisamehe watu na dhambi zao zote bure (Mark 2:5-12;Yohana 8:10-11;Wakolosai 2:13) kwa hiyo 70×7 ina maana ya Kiroho zaidi kwamba kusamehe hakuna mwisho (completeness cycle) hata leo Yesu anasamehe ukitubu na kuacha dhambi zako.
  1. Namba kubwa ugawanjwa vipande vipande (by using factors) vya namba ndogo ili kuona maana yake Kiroho. Mfano 490 = 70 x 7, 153 = 3x3x17. Namba (3) ni kusudio la Mungu ,Namba (17) kuwapeleka mbinguni wale waliookoka wakati wa mwisho.
Namba ndani ya biblia hazipo kwa bahati bahati tu bali zina makusudio maalumu kuwekwa hapo.Kwa kifupi na tuanze kujadili Namba moja moja ina maana gani au ishara gani Kiroho.

Namba 1
Hii ni namba ya Mungu. Mungu ni mmoja ni yeye peke yake hakuna Mungu mwingine.
 Namba 2
Namba 2 ni Namba ya wale waeneza Neno la Mungu (Wainjilishaji) Kwa mfano Yesu aliwatuma wanafunzi wake 70 “Wawili wawili”(Luka 10:1). Ufunuo 11 tunaona wale Mashaidi 2 waliouwawa na baadaye wakafufuka kutangaza Neno la Mungu. Matendo 13, Paulo na Barnabas walipelekwa pamoja kama Wamisionari wa kwanza kutangaza neon la Mungu. Kwa hiyo Namba 2 kama ina maana Kiroho au ina alama fulani basi kwa wale wasambaza neno la Mungu Wainjilisti na watu wengine waoeneza neon la Mungu kwa njia moja au nyingine. (Nimefanya utafiti kwa ku angalia miaka na tarehe ya kuzaliwa na katika maisha yao kwa ujumla namba 2 inajitokeza sana )
Namba 3
Namba 3 Ni Kusudio la Mungu/Kusudi la Mungu kwa mfano wakati wa tukio zima la kusulubiwa kwa bwana Yesu Lilikuwa ni kusudio la Mungu mwenyewe.Kumbuka kulikuwa na Misalaba 3(Marko 15:27) Petro alimkana Bwana Yesu mara 3(Marko 14:66-72) Mitume 3 walikuwa pamoja na Bwana yesu pale bustani ya gethsemani(marko 14:33),Bwana Yesu aliomba mara 3 mle Bustanini(marko 14:32-41),Jina “YESU WA NAZARETH MFALME WA WAYAHUDI” Liliwekwa msalabani kwa lugha 3 (Yohana 19;19-20) makundi 3 Makuhani, Viongozi wa dini na waalimu na Wote walitaka Yesu asurubiwe(Mathayo 26:59)nk.Vilevile kuna Namba inaweza kujitokeza katika namba kubwa lakini zikiwa sawa na 3 kama Yuda alipewa vipande 30 kumsaliti Yesu(Mathayo 26:15), Kulikuwa giza masaa 3 kutoka saa 6 mpaka saa 9, 12, 27 nk (mathayo 27:45).Kwa matukio yote hayo hii namba 3 inayojirudirudia ni kwa bahati mbaya au ni kwa kusudi maalum? Namba 3 hapa inatuonyesha kwamba tukio lote la kusulubiwa kwa Bwana Yesu ilikuwa kwa Makusudi ya Mungu (purpose of God/willing of God) Fikilia kukiwa na mashaidi wawili watatu basi neno lidhibitike, pakiwa na wawili watatu na Mimi Mungu nipo pamoja nao.
 Namba 4
Namba 4 inamaanisha dunia nzima (Ulimwengu) (worldwide) Biblia inatabua kwamba kuna pande 4 za dunia Mashariki,Magharibi,Kaskazini na Kusini (zaburi 107:3). Biblia Inazungumzia pepo (winds) 4 za dunia (Mathayo24:31) na inatambua kuna pande 4 za dunia (Ezk 7:2).Kwa hiyo kama namba 4 inamaanisha alama yeyote au maana yeyote Kiroho basi inatambulisha Dunia au Ulimwengu kwa ujumla.
Vilevile namba 4 iamaanisha ukamilifu wa jambo linapofikia mwisho kabisa (hitimisho la jambo) kwa mfanoYesu alisubili mpaka siku 4 Lazaro alipokufa kabla yakufufuliwa (Yohana 1:15-17) Mfalme Jehu’aliruhusiwa kutawala kizazi cha 4 (2Wafalme 10:30,13:1,9-10,14:16,2915:8-18) Israeli walikaa utumwani mpaka kizazi cha 4 baada ya kutumikishwa miaka zaidi 400 (Mwanzo15:13-16).Abraham alinunua kipande cha ardhi kwa ajiri ya kumzikia Sarah mkewe kwa shekeli 400 (Mwanzo23:15) Kwa hiyo kwa maaana hii Namba 4 vivile ina maana ya utimilifu wa kitu au mwisho wa kitu ktk muda, kwa kipidi Fulani. hata kumaanisha Mwisho wa dunia (2Petro 3:10).
Namba 5
Namba 5 ina maanisha Wokovu au Hukumu.Yesu alipata hukumu ili tupate Wokovu kwa hiyo usishagae namba 5 ikiwakilisha Wokovu au hukumu kwa wakati mmoja .Namba 5 inaonekana ½. Namba ya 10, 5 inawekuwa kama 5 50 500 5000 nk. Unaweza kufikiria ushuru wa hekalu ulikuwa shekeli 5(kutoka 30:13) au wale watu 5000 aliowalishwa chakula Bwana Yesu (Yohana 6:10-13) au unawea kufikiria wale wanawali 5 wapumbavu na 5 wenye busara (mathayo 25:1-2) nk .kwa hiyo kama namba 5 ni alama au maana fulani ya Kiroho basi ni hiyo yaWokovu au Hukumu.
Namba 6
Kama namba 6 inamaanisha alama au maana yeyote Kiroho basi itakuwa inamaanisha KAZI. Mungu alitumia siku 6 kuumba ulimwengu (kutoka 20:11).Namba 666 katika Ufunuo 13:18 ni Wasiookolewa walio kwenye mikono ya shetani wakijitahidi kupata haki mbele ya Mungu.
Namaba 7
Namba 7 inatumika sana kwenye biblia katika maana ya Ukamilifu wa Ki Mungu (Completed cycle) (siku7, miaka7) kama kusamehe ni 70x7times maana yake kusamehe hakuna mwisho samehe samehe samehe……Vile vile namba hii 7 inatabulika kama na namba ya Mungu. Ukiomba kitu chochote katka Mungu mara 7 hakika Mungu atakupa jibu.(Tatizo letu tunamchagulia Mungu majibu, Majibu mengine hatutaki na tunaendelea kuomba kwa hasara).Kwa mfano Ukuta wa babeli ulidondoka baada waisrael kusunguka mara 6 na mara 7 ukuta kukadondoka.Naamani aliambiwa akajichofye mara saba na baada ya hapo ukoma ukapona kabisa.
Namba 8
Namba 8 ni 2×4 au 2x2x2 maana yake ni mchanganyiko wa maana ya namba 2 na namba 4.
 Namba 9
Namba 9 ni 3×3.kwa hiyo maana yake ni sawa na namba 3
Namba 10
Namba 10 ni sawa na namba 1inaweza kuwa 10, 100, 1000, 10000…. Nk. Namba 10 ina maanisha Ukamilifu kamili. Biblia inasema kuhusu sarafu 10(luka 15:8), Kondoo 100 (luka 15:4) miaka 1,000 (2Petro 3:8),Vizazi 1000 (Kumb.7:9)etc.kwa hiyo kama namba 10 ni alama ya jambo fulani au ina maana fulani kiroho basi ni Ukamilifu.
Namba 11
Namba 11 inatumika katika biblia inamaanisha mapungufu katika usahihihi (defective fullness). Kwa mfano kulikuwa na makabila 12 (lakini halisi ni 13) ya waisraeli, lakini Daudi alipofanya sensa Mungu alisungumzia Makabila 11(1wafalme 11:31-32).Wakati Yuda aliyekuwa mmoja kati ya Wanafunzi wa Yesu 12 (Yohana 6:70-71) alijiua baada ya kumsaliti Yesu, Walibakia Wanafunzi 11, Baadaye alichaguliwa Mtume mwingine kuchukua nafasi yake na kuwa 12 tena.(Matendao 1-13-26). Kwa hiyo namba 11 kama ina alama yeyote au maana yeyote kibblia basi ni Usaliti.
Namba 12
Kama namba 12 ni alama au ina maana yeyote kiroho basi ni Utimilifu katika muonekano Kwa mfano kulikuwa na Makabila 12 na Mitume 12, Mji mtakatifu una urefu wa 12000 mara 12000 mara 12000 (Ufunuo 21-16)nk. Kwa hiyo kama namba 12 ina maanisha alama au ina maana Kiroho basi ni Utimilifu katika muonekano.Namba 7,10,12 zote zinafanana kila moja kama utimilifu wa kiroho isipokuwa ikiambatanishwa na namba zingine kama 2×6,2x2x3 nk..
 Namba 13
Namaba 13 kama ina maanisha alama au maana fulani ya Kiroho basi ni Hakika ya Utimilifu. Biblia inasungumzia Mitume 12, Lakini hakika kabisa ni 13. Wa 13 ni Mtume Paulo aliposisitiza akiwa katika katika roho Mtakatifu kuwa amekidhi matakwa/Vigezo vyote vya kuwa Mtume kama wale 12.(1Wakoritho9:2;15:8-9; 2Wakoritho12:11-12) Biblia kwa kawaida kabisa inasungumzia Makabila 12 ya Israel lakini Uhakika na kimsingi Yalikuwa Makabila 13(Mwanzo 49:1-28;Hesabu 32:33;Joshua 16 na Joshua 17) Namba 13 ina maanisha Uhakika wa Ukamilifu.
Namba 17
Inaonekana sehemu nyingi katika biblia ikisimama kwa maaana ya Mbingu/uungu (Heaven) Kwa mfano katika miaka 17 ya mwisho ya maisha yake Yakobo chini ya Yusufu ambaye ni mtoto wake kipenzi ambaye alisalitiwa kama alivyosalitiwa Yesu wakati alipotumika badala ya Mungu kuwaokoa na njaa kali (Mwanzo 47:28)Yeremia alininunua shekeli 17 kuwanunulia wana wa israel kipande cha ardhi kuonyesha kwamba Mungu amewarudisha tena kwenye nchi yao.Kipande kile kilikuwa kinamaanisha Ufalme wa Mungu umewarudia tena (yeremia 32:9) Kwa hiyo namba 17 kama ina alama au maana ya Kiroho ni mbingu/ Uungu (heaven).
Namba 37
Kama ilivyo namba 23 zinamaanisha Hukumu ya Mungu.Nuhu alikuwa kwenye Safina kwa muda wa siku 370 wakati mungu alipo hukumu dunia(Mwanzo 7:11;8:14-18).Jehsi la Sennacherib liliangamizwa na Mungu kwa usiku mmoja watu 185,000(2Wafalme 19:35) 185,000 = 5x37x1,000.Namba 666, ambayo ni namba inamaanisha watu wasiookoka wali chini ya hukumu ya Mungu(Ufunuo 13:18) kama namba hiyo ukiivunja vunja katika namba ndogondogo ni 3x6x37.Kwa hiyo Namba 37 kama ina alama au maana yeyote Kiroho basi ni Hukumu..
 Namba 40
Namba 40 inajirudiarudia katika biblia ikimaanisha Mwisho wa majaribu/Majaribu.Musa alikaa siku 40 katika Mlima Sinai(Kutoka 24:18), Huku nyuma Wana wa Islael walijaribiwa na kushindwa kuvumilia na kutengeneza miungu yao(Kutoka 32:1-4).Israel walikuwa Jangwani kwa kipindi cha miaka 40 walishindwa na hakuna aliyeokolewa wote hawakufika Kanani isipokuwa watoto wao amabao waliozaliwa baada ya kutoka Misri.(Waebrania 3:17).Yesu alijaribiwa na shetani siku 40 mchana na usiku (Mathayo 4-1-2:Luka 4:1-2) pamoja na majaribu hayo tunamshukuru Mungu kwamba Yesu hakushindwa alimshinda shetani (Mathayo 4:3-11;Luka 4-3-14) Kwa hiyo kama namba 40 inamaanisha alama au maana yeyote Kiroho basi ni Majaribu. Fikiria watu wengi wakifikia umri wa miaka 40 shida na masumbufu huwa yanakwisha na hili kila mtu anaweza kujichunguza au kuchunguza hata kama maisha ya mtu huyo ni ya kimasikini lakini amani na utulivu unakuwepo katika maisha yake( Focus on Future destenity) Utu uzima ni miaka 40. Chunguza 40 zinavyotumika katika maisha na kwa jamii kwa ujumla hizo ni maana za kiroho kumbuka!
Namba 43
Namba 43 ina maana ya Hukumu au Wokovu.Kwa mfano Israel walikaa Misri kwa miaka 430.Mwisho wa miaka hiyo 430 hHukumu ilishuka kwa Wamisri na Uhuru Wokovu kwa kwa Israel). Kwa hiyo namba 43 kama inamanisha alama au maana Kiroho basi ni Hukumu au Wokovu.
Ndugu mpendwa Mungu akubariki na tilia maanani somo hili litakusaidia na wakati mwingine kukuonyesha njia. Unaweza patwa na shida au jambo Kumbuka Mungu anazungumza kupitia Namba. Kwa nini 3 kwa nini 7,2,5,10 nk..Mungu anapozungumza na wewe anaweza kukuonyesha ishara mbalimbali za namba kati jambo fulani katika maisha yako kiroho. Vilevile kumbuka si kila namba ina maana ya kiroho.
Kuna baadhi ya dini na madhehebu huwa wana utaratibu wa kuhesabu hesabu vitu Fulani kama ushanga na nk hata kwa wachawi na waganga huwa wanahesabu hesabu kwa namna Fulani ili kupata namba na maana zake kwenye mambo yao ya kichawi. Nimekwambia hayo ili uweze kujua kwamba katika namba kuna siri kubwa kiroho kwetu sisi tulio okoka na kwa wale wasio mwamini Bwana Yesu.

Asante Mungu akubariki tuombeane
- See more at: http://jicheki.com/fahamu-siri-ya-namba-kiroho/#sthash.2nW3FIwo.dpuf

MIUJIZA YA YESU, YESU KUUOKOA ULIMWENGU, UFUFO WA LAZARO

Yesu anapakwa marashi
(Mat 26:6-13; Marko 14:3-9)
1Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alifika Bethania alikoishi Lazaro ambaye Yesu alikuwa amemfufua kutoka wafu. 2Huko walimwandalia chakula cha jioni, naye Martha akawa anawatumikia. Lazaro alikuwa mmoja wa wale waliokuwa mezani pamoja na Yesu. 3Basi, Maria alichukua nusu lita ya marashi ya nardo safi ya thamani kubwa, akampaka Yesu miguu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba yote ikajaa harufu ya marashi. 4Basi, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema, 5“Kwa nini marashi hayo hayakuuzwa kwa fedha dinari 300, wakapewa maskini?”6Alisema hivyo, si kwa kuwa alijali chochote juu ya maskini, bali kwa sababu alikuwa mweka hazina, na kwa kuwa alikuwa mwizi, mara kwa mara aliiba kutoka katika hiyo hazina. 7Lakini Yesu akasema, “Msimsumbue huyu mama! Mwacheni ayaweke kwa ajili ya siku ya mazishi yangu.8Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini hamtakuwa nami siku zote.”
Njama za kumwua Lazaro
9Wayahudi wengi walisikia kwamba Yesu alikuwa Bethania. Basi, wakafika huko si tu kwa ajili ya kumwona Yesu, ila pia wapate kumwona Lazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka kwa wafu. 10Makuhani wakuu waliamua pia kumwua Lazaro, 11maana kwa sababu ya Lazaro Wayahudi wengi waliwaasi viongozi wao, wakamwamini Yesu.
Yesu anaingia Yerusalemu kwa shangwe
(Mat 21:1-11; Marko 11:1-11; Luka 19:28-40)
12Kesho yake, kundi kubwa la watu waliokuja kwenye sikukuu walisikia kuwa Yesu alikuwa njiani kuja Yerusalemu.13 Basi, wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki; wakapaza sauti wakisema:
“Sifa! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.
Abarikiwe mfalme wa Israeli.”
14Yesu akampata mwanapunda mmoja, akapanda juu yake kama yasemavyo Maandiko:
15“Usiogope mji wa Siyoni!
Tazama, Mfalme wako anakuja,
amepanda mwanapunda!”
16Wakati huo wanafunzi wake hawakuelewa mambo hayo, lakini Yesu alipokwisha tukuzwa, ndipo walipokumbuka kwamba hayo yalikuwa yameandikwa juu yake, na kwamba watu walikuwa wamemtendea hivyo.
17Kundi la watu wale waliokuwa pamoja na Yesu wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua kutoka kwa wafu, walimshuhudia. 18Kwa hiyo umati huo wa watu ulimlaki, maana wote walisikia kwamba Yesu alikuwa amefanya ishara hiyo. 19Basi, Mafarisayo wakaambiana, “Mnaona? Hatuwezi kufanya chochote! Tazameni, ulimwengu wote unamfuata.”
Wagiriki kadhaa wanataka kumwona Yesu
20Kulikuwa na Wagiriki kadhaa miongoni mwa watu waliokuwa wamefika Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu hiyo. 21Hao walimwendea Filipo, mwenyeji wa Bethsaida katika Galilaya, wakasema, “Mheshimiwa, tunataka kumwona Yesu.” 22Filipo akaenda, akamwambia Andrea, nao wawili wakaenda kumwambia Yesu. 23Yesu akawaambia, “Saa ya kutukuzwa kwa Mwana wa Mtu imefika! 24Kweli nawaambieni, punje ya ngano hubaki punje tu isipokuwa ikianguka katika udongo na kufa. Kama ikifa, basi huzaa matunda mengi. 25Anayependa maisha yake, atayapoteza; anayeyachukia maisha yake katika ulimwengu huu, atayaweka kwa ajili ya uhai wa milele. 26Anayetaka kunitumikia ni lazima anifuate, hivyo kwamba popote pale nilipo mimi ndipo na mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu yeyote anayenitumikia Baba yangu atampa heshima.
Yesu anasema juu ya kifo chake
27“Sasa roho yangu imefadhaika, na niseme nini? Je, niseme: ‘Baba, usiruhusu saa hii inifikie?’ Lakini ndiyo maana nimekuja – ili nipite katika saa hii. 28Baba, ulitukuze jina lako.” Hapo sauti ikasema kutoka mbinguni, “Nimelitukuza, na nitalitukuza tena.”
 29Umati wa watu waliokuwa wamesimama hapo walisikia sauti hiyo, na baadhi yao walisema, “Ni ngurumo.” Lakini wengine wakasema, “Malaika ameongea naye!” 30Lakini Yesu akawaambia, “Sauti hiyo haikutokea kwa ajili yangu mimi, ila kwa ajili yenu. 31Sasa ndio wakati wa ulimwengu huu kuhukumiwa; sasa mtawala wa ulimwengu huu atapinduliwa. 32Nami nitakapoinuliwa juu ya nchi nitamvuta kila mmoja kwangu.”33(Kwa kusema hivyo alionesha atakufa kifo gani).
 34Basi, umati huo ukamjibu, “Sisi tunaambiwa na sheria yetu kwamba Kristo atadumu milele. Wawezaje basi, kusema ati Mwana wa Mtu anapaswa kuinuliwa? Huyo Mwana wa Mtu ni nani?” 35Yesu akawaambia, “Mwanga bado uko nanyi kwa muda mfupi. Tembeeni mngali mnao huo mwanga ili giza lisiwapate; maana atembeaye gizani hajui aendako.36Basi, wakati mnao huo mwanga uaminini ili mpate kuwa watu wa mwanga.” Baada ya kusema maneno hayo, Yesu alikwenda zake na kujificha mbali nao.
Watu hawana imani
37Ingawa Yesu alifanya miujiza hii yote mbele yao, wao hawakumwamini. 38Hivyo maneno aliyosema nabii Isaya yakatimia:
“Bwana, nani aliyeuamini ujumbe wetu?
Na uwezo wa Bwana umedhihirishwa kwa nani?”
39Hivyo hawakuweza kuamini, kwani Isaya alisema tena:
40“Mungu ameyapofusha macho yao,
amezipumbaza akili zao;
wasione kwa macho yao,
wasielewe kwa akili zao;
wala wasinigeukie, asema Bwana,
ili nipate kuwaponya.”
41Isaya alisema maneno haya kwa sababu aliuona utukufu wa Yesu, akasema habari zake.
 42Hata hivyo, wengi wa viongozi wa Wayahudi walimwamini Yesu. Lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakumkiri hadharani kwa kuogopa kwamba watatengwa na sunagogi. 43Walipendelea kusifiwa na watu kuliko kusifiwa na Mungu.
Yesu alikuja kuuokoa ulimwengu
44Kisha Yesu akasema kwa sauti kubwa, “Mtu anayeniamini, haniamini mimi tu, ila anamwamini pia yule aliyenituma. 45Anayeniona mimi anamwona pia yule aliyenituma. 46Mimi ni mwanga, nami nimekuja ulimwenguni ili wote wanaoniamini wasibaki gizani. 47Anayeyasikia maneno yangu lakini hayashiki, mimi sitamhukumu; maana sikuja kuuhukumu ulimwengu bali kuuokoa. 48Asiyeyashika maneno yangu anaye wa kumhukumu: Neno lile nililosema ni hakimu wake siku ya mwisho. 49Mimi sikunena kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila Baba aliyenituma ndiye aliyeniamuru niseme nini na niongee nini. 50Nami najua kuwa amri yake huleta uhai wa milele. Basi, mimi nasema tu yale Baba aliyoniagiza niyaseme.”

Wednesday, November 26, 2014

KUMTUMIA ROHO MTAKATIFU

NAMNA YA KUMTUMIA ROHO MTAKATIFU KAMA MSAIDIZI KUPITIA KAZI ZAKE

Na:Patrick Sanga
Yohana 14:16-18 … Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni, wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu”.
Katika somo hili nataka kuandika juu ya kazi za Roho Mtakatifu na kukuonyesha namna unavyoweza kumtumia Roho Mtakataifu kama Msaidizi kupitia kazi zake. Labda niseme kwa lugha hii, kama unataka kuona msaada wa Roho Mtakatifu kwenye maisha yako, ni lazima kwanza uzijue kazi zake, maana kazi zake ndizo zinazotuonyuesha maeneo ya msaada wake, kazi zake ndizo zinazofafanua kwa namna gani Roho Mtakatifu ni Msaidizi.
Roho Mtakatifu ni nani?
Roho Mtakatifu ni Mungu, mwenye nguvu zote, maarifa yote, anayepatikana kila mahali. Yeye anayo nafsi na ameamua kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu. Kusudi kubwa la ujio wake ni kuwaMsaidizi wa mwanadamu kwenye ulimwengu huu wa mwili, ili kumsaidia kuishi katika mapenzi ya Mungu.
Roho Mtakatifu amemamua kuishi ndani ya mwili wa mtu kwa sababu, Mungu hana namna ya  kutawala kwenye ulimwengu wa kimwili bila kuwa na mwili wa damu na nyama, kwa kuwa yeye ni Roho (Yohana 4:24). Hivyo hana budi kuingia kwenye mwili wa mtu na kufanya makao yake hapo, ili kutawala na kumuongoza mwanadamu katika mapenzi yake. (Yohana 14:23, Yohana 14:18, Ufunuo 3:20, 1Wakorinto 3:16-17, 6:19).
Kinachotusaidia kujua kwamba Roho Mtakatifu ana nafsi, ni tabia zake, maana kwenye kila nafsi kuna hisia, nia, kumbukumbu, akili nkBaadhi ya sifa na tabia za Roho Mtakatifu ni; anapatikana kila mahali (Omnipresence), Zaburi 139:7ana maarifa/anajua yote (Omniscient, Intelligence), 1 Wakorinto 2:10-11ni mwenye nguvu zote/wa umilele (Omnipotent),Mwanzo 1:2ni Mtakatifu, Luka 11:13, ana hisia (Waefeso 4:30, Mwanzo 6:3) – Wala msimuhuzunishe Roho wa Mungu…, Roho yangu haitashindana na Mwanadamu mileleana nia (will), 1Wakorinto 12:11 –Hutenda kazi kama apendavyo.
 Kazi za Roho Mtakatifu
  • Kufundisha, Mwalimu (Yohana 14:26) … Atawafundisha yote…
  • Kuongoza, Kiongozi (Warumi 8:14, Yohana 16:13) – Atawaongoza awatie kwenye kweli yote, wote wanaoongozwa na Roho hao ndio … Mfano (Matendo ya Mitume 13:4, Acts 8:29)
  • Ni mfunuaji wa mambo/mafumbo/siri za Mungu (1Wakorinto 2:10) –Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote. Usipoteze muda kumtaka Mungu akufunulie siri zake, wewe mwambi Roho Mtakatifu hiyo ndiyo kazi yake.
  • Muombezi (Warumi 8:26) – Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
  • Mtoa/mpasha habari za mambo yajayo (Yohana 16:13f) – Na mambo yajayo atawapasha habari yake.
  • Ni msemaji wa mambo ya Mungu/Yesu (Yohana 15:26, 2 Petro 1:21) – Yeye atanishuhudia (he will speak about me), Wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
  • Ni mtetezi/msemaji wa mambo yetu (Marko 13:11) – Kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu.
  • Ni mkumbushaji wa yale uliyojifunza au uliyoagizwa na Mungu (Yohana 14:26)… Atawakumbusha yote niliyowaambia.
  • Kutia/kuwapa nguvu watu wake nguvu/uwezo (Matendo1:8) –Lakini mtapokea nguvu akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu…
  • Kuuhakikisha (convict, make aware, sadikisha) ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu (Yohana 16:8) e.g unajuaje kwamba kuna hukumu? Warumi 8:16
Naam kazi hizi za Roho Mtakatifu zinatufikisha mahali pa kujua kwambajukumu lake kubwa ni kuwa Msaidizi wa mwanadamu. Kufanyika msaada wa mwanadamu katika mambo hayo hapo juu pale mwanadamu atakapohitaji msaada huo.  Hivyo ni jukumu lako kumpa nafasi kwa kuboresha mahusiano yako na yeye ili akusaidie. Hata hivyo Roho Mtakatifu kuitwa Msaidizi haina maana kwamba ndio umvunjie heshima, bali fahamu kwamba, Roho Mtakatifu ni Msaidizi kwa namna ambayo bila yeye mimi na wewe hatuwezi kutenda neno lolote.
Kazi hizi zinatupa kujua kwamba Roho Mtakatifu yupo tayari kutusaidia katika kila eneo la maisha yetu. Ni jukumu letu kumpa  nafasi hiyo na kutambua kwamba bila msaada wake sisi hatuwezi lolote. Watu wengi leo hawaoni msaada wa Mungu kwao kwa sababu ya kutokumpa Roho Mtakatifu nafasi ya kuwasaidia katika maisha yao na pia kwa kutokujua maeneo ya kumtumia Roho Mtakatifu kama Msaidizi.
Je, unahitaji msaada wa Roho Mtakatifu eneo gani la maisha yako?, ni ndoa, kazi, madeni, huduma, kanisa, utawala nk mpe nafasi akusaidie, akufundishe na kukuongoza katika kweli yote. Kumbuka yeye ni Mungu ambaye ni Mwalimu na Kiongozi pasina yeye mimi na wewe hatuwezi neno lolote. Unataka kumjua Mungu, kuwa na maombi yenye matokeo mazuri na kufanikiwa katika maisha yako kiroho na kimwili pia mwambie Roho Mtakatifu akusaidie.
Msaada wa Roho Mtakatifu hauna mipaka maadam unahitaji msaada katika yale ambayo ni mapenzi ya Mungu. Hivyo haijalishi unapita katika jambo gani mpe nafasi Roho Mtakatifu akusaidie. Na ili uweze kuthamini msaada wa Roho Mtakatifu jifunze siku zote kufikiri kwa dhana kwamba bila msaada wake wewe huwezi lolote, na kwa sababu hiyo utaona umuhimu wa yeye kukusaidia katika maisha yako.
Usisubiri mambo yako yaharibike au usiachague mambo unayofikiri magumu ndio umshirikishe akusaidie, yeye anataka kuwa Bwana wa maisha yako, akusaidie kwa kila kitu hata mambo madogo kabisa kwenye maisha yako. Kina-muumiza Mungu kuona watoto wake chini ya jua wanahangaika katika maisha yao, wakati yeye amemleta Roho Mtakatifu ili awasaidie katika maisha hayo. Tumia vizuri fursa ya Roho Mtakatifu sasa maadam anapatikana, kuna wakati hatapatikana.

Monday, November 24, 2014

MALAIKA: WAJUMBE WA MUNGU

‘Familia yote ya mbinguni na duniani’
Malaika kwa sasa ni sehemu ya lile ambalo mtume Paulo aliiita ‘ubabu wote wa mbinguni’ – Mungu Baba, 
Yesu mwana wa Malaika. Karibu familia itakuwa imekamilika Yesu atakaporudi mara ya pili hapa duniani 
na ndipo wataongezeka ‘wana wa Mungu’-Wanafunzi waaminifu wa Kristo – ambao watatawala dunia.
Pamoja naye; kwa hiyo nampigia Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo magoti, ambaye kwa jina lake 
ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa. (Waefeso 3:14,15,UV). Muumba anakaa katika nusu
isiyoweza kuharibiwa na anaweza kuonekana kuwa yuko mbali sana na sisi mara kwa mara. Lakini ile
familia ya Mungu imetoa ule utofauti uliokuwepo, na siku itakuja ambapo mwisho wa miaka Elfu moja
dhambi zote zitakuwa zimeondolewa na mauti itashindwa na Mungu atakuwa yote katika wote (1
Wakorintho 15:28).
Ni jinsi gani Malaika wanavyotuhudumia?
Kwa mwamini, kule kufahamu kwamba malaika wapo kwa faida yake hii ni msaada wa kutosha. Kama
tunavyoweza kuwa na Imani na daktari wa upasuaji mkubwa (ingawaje hatumuoni kwa macho kwa
sababu ya dawa ya usingizi na ganzi), hivyo kuelewa kazi ya malaika ni kuwa na imani katika ulinzi wa
Mungu kwetu na namna Mungu anavyohusika katika maisha yetu. Kwa hakika, kwa matendo ni kitu zaidi 
ya hapo. Kama kweli tuwaaminifu, tunamwomba Mungu na Mungu anajibu maombi yetu kwa pamoja
kama anavyopenda yeye. Hutuma malaika wake ambaye, bila kuonekana anaamuru mazingira na hali
tulizonazo, na hivyo kubadilisha maisha yetu: Hatua za mtu huimarishwa na BWANA. 
Tufupishe kwa kusema, kweli malaika wanaishi na wapo kwa ajili ya kutusaidia kama tunamcha Mungu. 
Ukweli hautegemei yale tunayoyaona. Na hali ndilo kosa kubwa alilolifanya Bwana Khrushchev. Vitu
kinavyoonekana ni ya muda tu bali visivyoonekana ni vya milele ( 2Wakorintho 4:18,UV).
Wakati Jeshi la mbinguni wanapotumwa kuwakusanya wateule pamoja kwa ajili ya hukumu Yesu
atakaporudi, wateule wataweza kukutana na kuwaona malaika kwa mara ya kwanza Mwaliko huenda
ukawa hivi, ‘Bwana amekuja anawaita!" (Yohana 11:28). Kwa sasa ni wakati wa kumwamini BWANA
MUNGU na malaika zake na hivyo kujiandaa kwa ajili ya tukio hili kubwa: "Unifumbue macho yangu, ili
niyatazame maajabu yatokayo katika Sheria yako". (Zaburi 119:18).
(8)
MALAIKA: WAJUMBE WA MUNGU 
MAFUNDISHO YA BIBLIA KUHUSU HUDUMA YA VIUMBE WA KIROHO. 
Habari imeeleza jinsi mwanaanga wa kwanza wa Kirusi aitwaye Yuri Gagarin, aliagizwa na Khrushchev
waziri mkuu wa serikali ya Urusi ( iliyokuwa inaitwa Soviet) ili kuangalia kama kuna malaika angani,
ilikuwa ni mwezi wa April mwaka 1962. Aliporudi kutoka angani alitoa taarifa kwamba "hakuna malaika
aliowaona". Na Khruschehev" alimpongeza, nilijua usingewaona kwani hakuna vitu vya namna hiyo" 
Ni rahisi kudhania, kwamba kile usichokiona hakipo!.
Je, wewe unaamini kuwa malaika wapo? Je, unafahamu malaika ni nani, au wanafanya nini? Je, ni fikra 
za mafundi sanaa katika michoro ya dini toka karne na karne? Hivi kweli kuna kitu tunachopaswa
kukifahamu? Je ni muhimu kujua kama malaika wapo?
Tuangalie Biblia 
Majibu sahihi ya maswali hayo yanapatikana tu katika Biblia . hatuna chanzo kingine cha habari
kinachoaminika .Biblia ni neno lenye pumnzi ya Mungu na lina maktaba ya habari inayoongelewa, kwa
hiyo,ni wapi pa kuangalia? 
Twende moja kwa moja kwenye biblia, kupata ushahidi unaoonekana kuhusu hawa viumbe wa mbinguni. 
Mfano tunaopaswa kuangalia, wa kwanza si tukio la kwanza kabisa wakati malaika wanapotajwa, lakini ni 
wa kutupatia mwanga. Katika nyakati zile, mnamo karne ya 8KK falme za syria na Israel zilikuwa
zikipigana vita. Mfalme wa Shamu alifadhaishwa baada ya kugundua vilipo vikosi vyake vya mbele.
2wafalme 6:8-11. Baada ya kuambiwa kuwa mtoa habari alikuwa Elisha nabii wa Mungu, watumishi wake 
wakamteremkia Elisha na mtumishi wake katika mji mdogo ulio Kaskazini mwa Israeli. Mfalme wa Shamu 
alipeleka jeshi kubwa kwenda kumkamata nabii, wakaizunguka Dothani wakiwa na magari ya farasi na
wapanda farasi wakati wa usiku. Mtumishi wa Elisha alipotazama asubuhi aliliona jeshi kubwa
aliogopeshwa, "Ole wetu, bwana wangu tutafanyaje?" 
Mtu ambaye macho yake yalifumbuliwa 
Ilikuwa ni mwitikio wa asili: Walizingirwa na jeshi kubwa lililokuwa katili na adui aliye penda kutesa
asiyeweza kuonyesha huruma hakika alistahili kwa njia yoyote kutishika. Lakini bwana wake yeye
alitenda tofauti kabisa! Hakuwa na wasiwasi na alikwa mwenyematumaini, mwitikio wa Elisha ulikuwa!
"Usiogope!" usiogope? Ninani asiyeweza kuogopa katika hali ya namna hii? Sababu ilikuwa,
"walioupande wetu ni wengi kuliko walio upande wao": Alikuwa ana maanisha nini? Je, yawezekana
Elisha aliweza kuona kitu ambacho mtumishi wake hakuweza kuona ? Yote yaliweza kuwa wazi wakati
nabii alipomuomba Mungu. 
Bwana ninakusihi mfumbue macho yake ili aweze kuona. Naye BWANA akayafumbua macho ya kijana
naye akaona tazama kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyo kuwa yamemzunguka
Elisha pande zote" (2 Wafalme 6:17). 
Elisha alikuwa mtu wa Mungu, naye BWANA alikuwa ametuma jeshi lake la ulinzi wake katika
kumhudumia nabii wake. Elisha tayali alikuwa ameshaona jambo kama hilo muda kabla ya Eliya
mtangulizi wake hajachukuliwa kwenda juu kutoka kwake ndipo Elisha alilia "Baba yangu, baba, yangu
gari la Israeli na wapanda farasi wake (2 wafalme 2: 12).
Elisha alijua kutokana na tukio aliloliona ya kwamba malaika walikuwepo pale, mtumishi wake ambaye
alikuwa hajawahi kuona alikuwa hafahamu uwezo halisi hutoka wapi. Macho yake kiroho yalikuwa
yamefumbwa. 
Mungu hufanya kazi kupitia Watumishi wake. 
Tukio la Dothani ni ufunuo unaofundisha namna Mungu anavyo fanya kazi kwa kumlinda mtu kwa njia ya 
jeshi lake ambao ni wajumbe watumishi.
(

MALAIKA

Malaika




Malaika ni nani? Imo katika Biblia, Waebrania 1:14, Je? Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Kuna malaika wangapi? imeandikwa ufunuo 5:11 "Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai na za wale wazee, na hesabu yao ilikua elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,"
Je? malaika ni wa kiwango cha juu kuliko wanadamu? Imo katika Biblia, Zaburi 8:4-5 "Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie? umemfanya mdogo punde kuliko malaika; umemvika taji ya heshima."
Malaika aweza kutokea katika mfumo wa watu wa kawaida. Imo katika Biblia, Waebrania 13:2 "Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wame wakaribisha malaika pasipo kujua."
Ni nani kiongozi wa malaika? Imo katika Biblia, 1 Petro 3:22 " Naye yuko mkono mwa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiwa chini yake."
Malaika nikama washungaji wakipekee, imeandikwa Mathayo 18:10 " Angalieni msidharau mmoja yapo ya wadogo hawa; kwa maana na waambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote hutazama uso wa baba yangu aliye mbinguni."
Malaika hutu Linda. imeandikwa Zaburi 91:10-11. "Mabaya hayata kupata wewe, wala tauni haitakaribia hema yako. kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote."
Malaika wata kuondoa kwenye shida imeandikwa zaburi 34:7 Malaika wa bwana hufanya kituo, akiwazungukia wamshao na kuwaokoa."
Malaika huchukua amri za Mungu Imeandikwa Zaburi 103:20-21, " Mhidimu BWANA enyi malaika zake, ninyi mlio hodari mtendao neno lake, mkiisikiliza sauti ya neno lake. Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote, ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake."
Malaika hulieneza neno la Mungu Imeandikwa Luka 2:9-10 "Malaika wa BWANA akawatokea gafula utukufu wa BWANA ukawang'aria pande zote wakaingiwa na hofu kuu malaika akawaambia msiogope; kwa kuwa mimi nime waletea habari njema ya furaha kuu itakayo kuwa kwa watu wote."
Malaika watakuwa na kazi gani atakapo kuja yesu mara ya pili? imeandikwa Mathayo 16:27 "Kwa sababu mwana waadamu atakuja katika utukufu wa baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake." 24:31 " naye ata watuma malika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao wata wakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu mbingu mpaka mwisho huu."
Mashetani walitoka wapii? Imeandikwa ufunuo 12:9 "yule joka akatupwa yule mkubwa, nyoka wazamani aitwaye ibilisi na shetani audaganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa wote pamoja naye."
Je? malaika washetani wana mvuto gani katika maisha ya wanadamu? imeandikwa Waefeso 6:12 "kama kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wagiza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."
Je? Mwisho wa shetani na malaika wake utakuwa vipi? Imeandikwa Mathayo 25:41 "Kisha na atawaambia na wale walioko mkono wakushoto, ondokeni kwangu mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliyo wekewa tayari ibilisi na malaika zake."