Menu

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo

Thursday, August 20, 2015

MAPAMBANO DHIDI YA ADUi SHETANI



Mapambano dhidi ya adui shetani
Silaha za Mungu
Mkristo anapaswa kuvaa silaha zote za Mungu ili aweze kusimama na kumshinda adui katika moto wa aina yeyote atakaotaka kuuwasha, silaha hizi lazima kuizima mishale ya moto ya adui mwovu. Na hizi silaha za Mungu zavaliwa kwa njia ya maombi na kuishi maisha yetu ya kila siku kwa imani.
Bible inatuambia kwenye Waefeso 6:10-18 namna ya kuvaa silaha zote za Mungu.
Mstari wa 10: Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
Kuna vita ipo ikiendelea kati ya nuru na giza.Kazi ya giza ipo kukuharibu wewe kiumbe wa Mungu, lakini hazina nafasi endapo utajitoa na kumtii Mungu ipasavyo.
Mwenye nguvu ni Mungu wetu ambaye ni mtawala wa vitu vyote na anayeishi milele.
Mstari wa 11: Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani.
Kwa kuvaa silaha za Mungu, haina maana kwamba tunavaa vile vitu kwenye miili yetu, vionekanavyo kwa macho kama wanavyovivaa askari wa JW waendapo vitani, kama ilivyokuwa vita vya Tanzania na Uganda miaka ya 80. Bali twapaswa kuzivaa kiroho, kwa kuzivaa kiroho ina maana kwamba tunamtii Mungu. Kwa njia hii ya kumtii Mungu wetu, twaweza kabisa kumshinda adui mwovu. Kwa kuzivaa silaha zote, ina maana kwamba kuvaa kila kifaa tunachoambiwa kuvaa mahali hapa, na sio kuvaa nusu. Kwa kufanya hivyo hatutaweza kumwogopa shetani, kwa maana tunaye Mungu tunayemtumikia. Kama mkristo, hakikisha kwamba hutafumwa ukiwa hujavaa silaha zote za Mungu.
Mstari wa 12: Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya (a) falme na (b) mamlaka, (c) juu ya wakuu wa giza hili, (d) juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Vita si kati yetu na wanadamu wenzetu hapana, yaani sio kati ya sisi kwa sisi, bali ni kati yetu sisi na adui mwovu shetani. Tunashindana na shetani pamoja na sheji lake zima na mapepo yote, yaani na ufalme wake wote. Hatuwezi kuwaona kwa kuwa wao ni roho hawana miili, ila kwa kweli wana nguvu na hujipanga kweli kweli. Wapo nje nje kutukamata na kutuharibu, ila kumbuka kwamba ukiwa ndani ya Yesu na kulitii neno lake, hawezi kukushinda Efeso 2:20-21. Yesu ni juu ya vitu vyote, na kama tukilijua hilo, basi nasi tupo pamoja naye Efeso 2:6.
Mstari wa 13: Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Shetani alishahukumiwa tayari, tena siku nyingi pale Bwana wetu Yesu Kristo alipolipa gharama ya dhambi zetu sisi wanadamu kwa kufa kwake kwa njia ya msalaba. Tusimame katika imani kwenye neno lake (Ebrania 2:14), shetani hana nguvu katika neno la Mungu na wala hawezi kulipinga.
Mstari wa 14-17: (Silaha sita) Basi simameni, hali mmejifunga
(a) Kweli viunoni
Tunafahamu ya kwamba Yesu ni kweli, na neno la Mungu ni kweli. Kwa hiyo sote tunapaswa kuliweka neno la Mungu na kulitunza ndani ya mioyo yetu. Hii inafanyika kwa kulisoma na kujifunza neno la Mungu. Kwa hiyo basi, tulitumie neno la Mungu katika maisha yetu ya kila siku ili tuweze kumshinda adui.
(b) Na kuvaa dirii ya haki kifuani,
Lazima tuishi maisha safi na yenye haki mbele za Mungu Baba yetu aliyetuweka duniani ili tumtumikie. Tusiishi maisha ya dhambi kama hao wote wasiomjua na kumfuata Yesu Kristo. Tutaweza kuishi maisha haya pale tu tutakapotambua kuwa Bwana wetu Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Kila amwaminiye Yesu Kristo, anakuwa amevalishwa haki mbele za Mungu (2Wakorintho 5:21). Na hii inatokea pale unapomkiri na kumkubali Yesu awe kiongozi wa maisha yako hapa duniani. Damu yake imekusafisha dhambi zako na haupo mbali na Mungu, umeunganishwa na Mungu Baba yake na baba yetu. Umefanywa mwenye haki mbele ya macho ya Mungu kwa njia ya upatanisho wa Bwana Yesu pale alipoziosha dhambii zako kwa damu yake. Tuendelee kuishi maisha matakatifu kwa kuikinga miili yetu ili isichafuliwe na takataka za shetani. Kwani miili yetu ni nyumba ya Mungu, iwe safi siku zote, ili asitukimbie maana hakai kwenye uchafu.
(c) V.15 Na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
Watahubiri namna gani kama wasipotumwa na kupelekwa. Ina heri miguu ile inayokwenda kulihubiri neno la amani na habari njema ya Bwana katikati ya watu (Warumi 10:15). Wakristo hatupaswi kuwa na aibu ya neno la Bwana wala tusilionee haya. Habari njema kuhusu neno la Kristo ndio njia pekee ya kuleta ukombozi na amani katikati ya watu. Tutembee katika mwanga siku zote 1Yohana 1:17. Kutembea katika mwanga ina maana tuzitii amri zote za Mungu na kuepukana na kila kitu ambacho hakipo katika mpango wake.
(d) V.16 Zaidi ya yote mkitiwa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto wa yule mwovu,
Askari anapokuwa amevaa ngao, anakuwa amekingwa na hiyo ngao (bullet proof) na wala hakuna mshale wa aina yeyote utakaomlenga. Vile vile kwa mkristo ni lazima kuvaa bullet proof ambayo ni imani katika Kristo (1 Yohana 5:4-5). Tunahitaji kuwa na imani ili kuishinda hofu kwa adui. Tukiwa na imani kwa Kristo, mishale ya adui ikija mbele yetu itagonga ngao hii ya imani na kudondoka chini pasipo kutudhuru.
Zingatia: Lazima kila wakati tukumbuke ya kwamba tunalindwa na Mungu pale tunapomwamini – tunapoliamini neno lake.
(e) V.17 Tena ipokeeni chepeo ya wokovu,
Chepeo ni lile kofia la chuma ambalo huitwa helmet huvaliwa na wale wajenzi au askari wakivikinga vichwa vyao visiumie endapo itatokea hatari ya aina yeyote ile. Kuvaa chepeo ni kuwa na hakika ya uzima wa milele. Tambua ya kwamba hatujaokolewa kwa kuwa tumefanya jema au zuri lolote, bali wokovu wetu ni ule halisi, tumeokolewa na Yesu (Efeso 2:8-9). Wokovu ni zawadi toka kwa Mungu kama tunaamini kwa imani (1 Yohana 5:12-13). Kama askari vitani amejeruhiwa kichwa chake pasipo kuvaa chepeo basi huyo atakuwa mahututi. Katika ulimwengu wa roho, shetani hujaribu kumdhuru mwanadamu kwenye nafsi yake, anafanya hivi kwa kutuwekea mawazo mabaya na ya uongo ndani ya nafsi zetu. Shetani huwaambia wakristo ya kwamba hawajaokoka, yaani hamna wokovu hapa duniani ni kudanganyana tu, kwani imekuwa ni mchezo siku hizi dini zimeanzishwa ili wachungaji kujipatia pesa. Ukimsikiliza, ujue kuwa umeacha kumtii Mungu na matokeo yake atakushinda.
(f) Na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
Ni lazima na muhimu kujua neno la Mungu lasema nini kuhusu maisha yetu hapa duniani ili tuweze kufika Mbinguni. Yesu alikuwa na umri wa miaka 30 pale alipoanza kuhubiri neno la Mungu, alihubiri na kuponya watu. Baada ya kubatizwa aliendelea kufanya hivi na alifunga siku 40 (yaani mchana 40 na usiku zilikuwa nazo 40). Katika kipindi hiki shetani alimjaribu sana. Je wafahamu Yesu alimshinda vipi shetani? Yesu alimshinda shetani kwa njia ya kumtamkia neno la Mungu. Neno la Mungu lililotoka kinywani kwa Yesu ndilo lililomfukuza shetani, na malaika wa Mungu walikuja na kufanya kazi na Yesu. Neno la Mungu lina nguvu, na shetani akilisikia hukimbia kwa kuwa analichukia, anaijua nguvu iliyoko huko.
Neno la Mungu linaitwa upanga kwa kuwa ni kali, linapenya hadi ndani ya moyo wa mwanadamu na kuwajulisha uovu wao na kwamba inabidi wakutane na mwokozi wao. Hakikisha hufumwi ukiwa huna neno la Mungu, na kuwa na neno la Mungu haimaanishi kuwa utembee na bible ukiwa umeishika mkononi, la hasha ulijue neno la Mungu, likae moyoni mwako na ulitumie kila wakati ukiwa unaongea na Mungu na ukiwa vitani pia Ebrania 2:14
1 Yohana 2:14 tunamshinda shetani endapo neno la Mungu lakaa ndani yetu. Tumpende Mungu Baba yetu aliyetupa ahadi nzuri, anayetupenda tuishi maisha safi na ya ushindi. Tuache kuyang’ang’ania ya dunia hii ambayo yaongozwa na shetani. Mshike Mungu ambaye anadumu milele, maana tamaa za dunia na kiburi cha uzima vyote vina mwisho, ila neno linadumu daima.
Mstari wa 18: Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu kuwaombea watakatifu wote.
Mkristo yeyote lazima akeshe na kudumu ktika maombi kila wakati, la sivyo lazima atarudi nyuma kiroho. Maombi ni mawasiliano halisi kati ya mwanadamu na Mungu wake. Mungu bado akiendelea kuongea nasi kila siku, na tutaisikia sauti yake endapo tutakuwa karibu naye kwa njia hii. Ukifanya hivyo utakuwa ukimsikia kila siku kupitia Neno Lake. Mungu anapenda kushirikiana nasi kwa njia ya maombi huku tukijulishana mawazo yetu, mipango yetu, hata tukimuuliza habari zetu. Tunaweza kusali kimya kimya, kwa sauti au kwa namna yeyote ile, lakini ili mradi tunawasiliana nae kila wakati. Na ukitaka kuwafahamu watu utawafahamu kwa njia ya mawasiliano, ukiwakuta wakiongea. Naye Mungu wetu vivyo hivyo, tutamfahamu pale tutakapokuwa tukiwasiliana naye. Angalia kwenye kitabu cha Yohana 17 jinsi Yesu alivyokuwa akiwasiliana na Baba yake kwa njia ya maombi.
Tusimwendee Mungu pale tunapokuwa na shida tu, tuwasiliane naye hata wakati wa furaha. Utakubaliana nami kwamba, mtu akiwa hana mawasiliano nawe, halafu akawasiliana nawe wakati wa shida yake. Hebu jaribu kufikiria utajisikiaje? Lazima utalalamika kuwa huyu jamaa ananitafuta wakati ana shida tuu, mie simsaidii maana shida yake ikiisha atarudi tena kulekule. Basi na Mungu wetu vile vile huwa hapendezwi na wale wanaomjua wakati wa shida tu, na kumwacha wakiwa hawana shida. Ni furaha iliyoje kwa watu wapendanao na kuwasiliana kila wakati, na kwa Mungu ni vivyo hivyo. Hii ndio inatakiwa iwe na ndivyo inavyomaanisha kwenye maombi.
Anayetuvalisha silaha
Luk 11:20-26
Kidole cha Mungu kinatupa kumshinda shetani, kidole cha Mungu ni Roho Mtakatifu wa Mungu. Twahitaji kidole cha Mungu katika vita. Mara tunaposhinda, ufalme wa Mungu unakuja juu yetu, maana yake, tunafunikwa na ufalme wa Mungu kwa hiyo hakuna atakayetutoa hapo.

Wednesday, August 19, 2015

USHUHUDA WA KUZIMU @ VICTORIA

Ushuhuda wa Victoria Juu ya Kuzimu





Muda Unaisha Haraka!

Huu ni ufupisho wa ushuhuda wa Victoria Nehale
Nilizaliwa na kuishi Namibia maisha yangu yote; na niliyatoa maisha yangu kwa Yesu tarehe 06 Februari 2005. Bwana Yesu Kristo ameshanifunulia mambo mengi katika ulimwengu wa roho ikiwa ni pamoja na safari za kuzimu. Bwana alinipa maelekezo kwamba niwashirikishe watu uzoefu wangu; pia alinionya kuwa nisiongeze wala kupunguza chochote katika vile alivyonionyesha na kuniambia. Wakati nikiandika kitabu hiki, mwishoni mwa 2006, nilishatembelewa mara 33 na Bwana Yesu Kristo. Kila aliponitembelea, Bwana alikuwa akiniambia kabla ya kuondoka: MUDA UNAISHA HARAKA!



Safari ya kwanza kuzimu


Katika wikiendi ya tarehe 23 Julai 2005, nilipanda taksi kwa ajili ya safari ya dakika thelathini kutokea mji wa Ondangwa ambako ndiko ninakofanya kazi na kuishi, hadi kijijini kwetu, kwa lengo la kwenda kuwa na wazazi wangu wakati wa wikiendi ile. Wakati nikielekea nyumbani, nilipata hisia kwamba kuna jambo lisilo la kawaida ambalo lingetokea jioni ile. Nilifika nyumbani kwenye saa 12 jioni; na hapo watu walikuwa wanaandaa chakula cha jioni. Nilikuwa jikoni pamoja na familia yetu, huku nikiwa nimelala kwenye mkeka. Watoto wa hapo nyumbani walikuwa wakiimba nyimbo zao za Shule ya Jumapili. Ghafla nilijisikia upako mzito ukinishukia; mwili wangu ukawa dhaifu sana; na nikawa nimetoka kwenye mwili kutokana na nguvu za Mungu. Nilimwona mwanamume amevaa joho jeupe refu likiwa limefungwa kwa kamba ya rangi ileile; akiwa anatembea kuelekea pale nilikokuwa nimelala. Kulikuwa na nuru imemzunguka kana kwamba ilikuwa ikitokea kwake. Alikuwa amevaa viatu vya wazi vya kahawia. Mwonekano wake ulikuwa kama wa watu wa Mashariki ya Kati, huku akiwa na ngozi nzuri ya hudhurungi. Uso wake ulikuwa mpole sana na umejaa utukufu lakini sikuweza kumtazama machoni. Alipoongea, sauti yake ilikuwa ya upole, na upendo, lakini pia  yenye mamlaka; mawimbi ya upendo yalikuwa yakitoka kwake.



Alinyoosha mkono wake kwangu na kuninyanyua kutokea pale nilipolala. Ghafla nilijiona nikiwa nina mwili mzuri sana. Nilijiona niko kama nilivyokuwa ningali na miaka kumi na nane. Nilikuwa nimevaa joho jeupe na kamba nyeupe. Japokuwa joho langu lilikuwa jeupe, lilitengenezwa kwa matirio tofauti na ya joho la yule mwanamume.  Joho lake lilikuwa la hariri huku liking’aa kiasi kwamba hata nashindwa namna ya kuelezea.


Alisema, kwa sauti ya upendo na upole sana: “Victoria, nataka uende nami; nitakuonyesha mambo ya kuogopesha na ninakupekela mahali ambako haujawahi kufika katika maisha yako.” Alinishika mkono wa kulia na tukaondoka. Nilijiona kama vile tunatembea hewani na muda wote tulikuwa tukielekea tu juu. Baada ya muda, nikawa nimechoka sana, na nikamwambia kuwa nisingeweza kuendelea na safari. Hivyo nikamsihi aniruhusu nirudi. Hata hivyo, alinitazama kwa upendo na kusema, “Haujachoka – uko sawa tu. Kama ukichoka, nitakubeba, lakini kwa hivi sasa uko tu sawa. Amani iwe kwako. Tuendelee.”


Tulifika mahali ambako ni pakavu sana; pakavu kuliko jangwa lolote analojua binadamu; hakukuwa na dalili zozote za uhai. Hakukuwa hata na mti mmoja au hata jani au kiumbe chochote hai. Lilikuwa ni eneo linalofadhaisha sana.


Hatimaye tulifika kwenye geti moja na yule mwanamume alinigeukia na kusema: “Victoria, tutaingia kupitia geti hili na mambo ambayo utayaona yatakuogopesha na kukufadhaisha – lakini uwe na uhakika kuwa kokote nitakakokupeleka, utakuwa na ulinzi mkamilifu. Wewe fungua tu macho yako na kutazama kila nitakachokuonyesha.” Nilijawa na hofu na kuanza kulia. Nilikuwa nalalamika na kumwomba anirudishe. Nilimwambia kuwa sikutaka kuingia kwenye sehemu ile maana tayari nilikuwa naona kupitia getini kile kilichokuwa kikiendelea ndani. Aliniangalia na kusema,  “Amani iwe nawe; niko pamoja nawe. Ni lazima tuingie ndani, maana muda unakimbia haraka.”


Tuliingia kupitia getini. Siwezi kukusimulia utisho wa mahali pale. Nina uhakika kabisa kuwa hakuna sehemu yoyote ulimwenguni ambayo ni mbaya kama ile! Sehemu ile ilikuwa ni kubwa sana na nilipata hisia kuwa inaendelea kupanuka muda wote. Ilikuwa ni sehemu ya giza totoro na joto lake halipimiki; ilikuwa ni joto kuliko moto ulio mkali kabisa. Sikuona miali yoyote ya moto au chanzo cha joto lile lakini kulikuwa ni JOTO! Kulikuwa na wadudu wa kila ukubwa; wa kijani, weusi, na wa kijivu - ila aina ya wadudu unaoweza kuwafikiria. Zaidi ya hapo, kulikuwapo pia kila mahali funza wafupi, wanene, weusi, ambao wanapanda juu ya kila kitu. Walianza kupanda juu yetu na wadudu nao walikuwa wametuzunguka kila upande. Mahali pale kulikuwa na harufu mbaya mno; hakuna maneno ya kutosha kuelezea harufu ile. Harufu ilikuwa kama nyama iliyooza lakini ilikuwa ni mbaya mara mia zaidi ya nyama iliyooza  niliyowahi kunusa maishani mwangu mwote! Kulikuwa na kelele za vilio na kusaga meno, pamoja na vicheko vibaya vya mapepo.


Kibaya kabisa kwenye sehemu hii ni kuwa pamejaa watu. Walikuwa ni wengi sana kiasi kwamba hawahesabiki. Walikuwa ni mifupa tu. Ninaweza kusema kwa ujasiri na uhakika kabisa kwamba mifupa hii ilikuwa ni wanadamu kwa vile niliweza kuwatambua baadhi ya ndugu zangu wa karibu na watu kutoka kijijini kwangu. Mifupa yao ilikuwa ya kijivu cheusi na mikavu sana. Walikuwa na meno marefu makali kama wanyama wa porini. Midomo yao ilikuwa mikubwa na mipana na ndimi zao zilikuwa ndefu na nyekundu sana. Mikono na miguu yao ilikuwa na vidole vyembamba virefu, na kucha kali, ndefu. Baadhi yao walikuwa na mikia na pembe.


Kulikuwa na mapepo yakichanganyika na watu: mapepo yalionekana kama mamba na yalitembelea miguu minne. Yalionekana yanajisikia vizuri tu kwenye mazingira yale na mara zote yalikuwa yakiwachokoza na kuwatesa wanadamu. Kelele kutoka kwa yale mapepo zilikuwa ni kama vile yako kwenye sherehe; maana yalionekana yana furaha. Yalikuwa pia yakicheza na kurukaruka muda wote. Wanadamu kwa upande wao, walionekana wana mateso na fadhaa; walikuwa katika hali ya kukosa msaada. Kelele za wanadamu zilisababishwa na maumivu. Walikuwa wakilia, wakipaza sauti na kusaga meno yao; na walikuwa katika hali ya mateso makali yasiyo na mfano.


Watu katika sehemu ile, walikuwa ni wengi mno, lakini niliweza kuona kuwa wengi wao walikuwa wanawake. Waligawanyika katika makundi mbalimbali. Japokuwa walikuwa katika makundi, ilikuwa haiwezekani kukadiria idadi yao katika kundi lolote maana makundi yenyewe yalikuwa ni makubwa kupita kiasi!


Mwanamume yule alinipeleka hadi kwenye kundi mojawapo upande wa mashariki wa sehemu ile. Kisha alinitazama na kusema: “Victoria, hili ni kundi la watu ambao walikataa kuwasamehe wengine. Niliwaambia mara nyingi na kwa njia nyingi kuwa wawasamehe wengine lakini walinikataa; Mimi nimewasamehe wao dhambi zao zote lakini wao walikataa kuwasamehe wengine. Muda wao uliisha na wakajikuta wako hapa. Watabakia hapa milele yote; wanakula matunda ya kazi yao milele na milele. Hata hivyo, inaniuma sana kuwaona kwenye sehemu hii mbaya na katika sehemu hii ya milele – maana ninawapenda.”


Nilipelekwa kwenye kundi linalofuata, na mwanamume yule aIiniambia kuwa watu wa kundi lile la pili walikuwa ni wale waliokuwa na madeni: walikuwa na uwezo wa kulipa madeni yao lakini waliendelea kuahirisha. Walikuwa wakisema kuwa tutalipa kesho, wiki ijayo, mwaka ujao, hadi muda ukawaishia. Hapa ndipo watakaa milele; wanakula matunda ya kazi yao.  


Aina ya pili ilikuwa ni ya wale ambao walikuwa na madeni na walikuwa na uwezo wa kuyalipa; na walikuwa tayari kuyalipa, lakini walikuwa wakiogopa matokeo maana, labda, kama wangesema kweli, wangeishia kukataliwa, au wangefungwa, au labda kile ambacho walitenda kingejulikana duniani kote nao wangeaibika. Yule mwanamume akasema:  “Hakuna kati yao ambaye alinijia kuniomba njia ya kufanya. Kama wangeniomba, ningewaonyesha njia rahisi kabisa ya kutoka kwenye hali zilizowakabili. Muda wao uliisha na wakajikuta wako hapa ambako ndiko watakuwako milele. Wanakula matunda ya kazi zao.”


Kisha akasema: “Kundi la tatu walikuwa na madeni ambayo hawakuwa na uwezo wa kuyalipa, lakini pia, nao hakuna hata mmoja ambaye aliniambia kuwa ana deni asiloweza kulipa. Kama wangefanya hivyo, ningewalipia madeni yao. Pia, walijaribu kutumia ufahamu wao na hekima yao, kitu ambacho hakikuwasaidia kwa njia yoyote. Hivi sasa wamejikuta mahali hapa ambako ndiko watakakoku. Wanakula matunda ya kazi yao. Moyo wangu unauma kwa ajili ya watu hawa wote maana ninawapenda sana.”


Katika kundi la kwanza, niliwaona ndugu zangu wawili wa kike wa karibu sana pamoja na mtoto wa miaka kumi na mbili, naye pia akiwa ndugu yangu. Nilijua alikuwa na miaka kumi na mbili maana huo ndio ulikuwa umri wake wakati anakufa. Katika kundi la pili nako pia niliwaona baadhi ya ndugu zangu, pamoja na Mchungaji ambaye nilimfahamu vizuri sana. Rafiki yangu wa kiume, Jakes, ambaye alijiua kwa sababu mimi niliamua kumpa Kristo maisha yangu, naye alikuwa kwenye kundi la pili. Niliwaona baadhi ya majirani zangu kwenye makundi yote pia.


Niliwatambua watu niliowajua kabla ya kufa kwao; nao pia walinitambua. Ndugu zangu walijawa na hasira sana waliponiona na wakaanza kunitukana. Walikuwa wakitumia lugha chafu kabisa wakati wakinitukana. Mmoja wao alisema kuwa sikustahili kumfuata mwanamume yule ambaye nilikuwa naongozana naye; walikuwa wakiongelea mambo ambayo nilikuwa nikiyafanya kabla ya kutoa maisha yangu kwa Kristo. Hawakuwa wakisema uongo. Mambo waliyokuwa wakinituhumu nayo yalikuwa ya kweli. Jakes alikuwa akisema kuwa mimi nilikuwa wa kwake na kwamba nilitakiwa kwenda pale alipokuwa maana nilitenda dhambi zilezile kama alizotenda yeye. Mara ya kwanza, yule mchungaji alionekana amefurahi kuniona na akasema nimefanya vema kuja, lakini alibadilika ghafla pale alipomwona yule niliyekuwa nimeongozana naye; kisha naye akajiunga na wale waliokuwa wakinilaani kwa matusi. Mwanamume yule aliyekuwa nami akaniambia nisiwajali maana hawajui walitendalo.


Nilipigwa na bumbuazi na kujawa na huzuni kubwa sana. Mwili wangu ulikuwa ukitetemeka na sikuweza kusimama. Nilikuwa nikilia bila kuweza kujizuia. Mwanamume yule alinigeukia, akanikumbatia, na kusema: “Amani iwe nawe, Victoria.” Nguvu zangu zilinirejea na nikajisikia salama mikononi mwake. Kisha akaniambia kuwa tulitakiwa kuondoka pale na kurudi. Alinitazama na kusema: “Victoria, nimeshakuonyesha. Sasa inabidi uchague ni kundi lipi unataka kuingia; uchaguzi umo mikononi mwako. Ni lazima uwaeleze watu kila kitu ulichokiona lakini usiongeze au kupunguza chochote.”


Nakumbuka kuwa tuliondoka pamoja kwenye ile sehemu ya kutisha lakini sikujua nimemwacha wapi maana fahamu zangu za kawaida zilinirudia. Nilifungua macho yangu na kujikuta kwenye mwili wangu wa nyama, huku nikiwa nimelazwa kwenye Hospitali ya Oshakati. Nilikuwa nimetundikiwa dripu kwenye mkono wangu wa kushoto; na nilimwona mama yangu na ndugu zangu wengine wa kijijini kwenye kona moja ya chumba, ambako walikuwa wakiniangalia kwa mshangao. Niliona kwenye uso wa mama yangu kwamba alikuwa analia. Nilimwuliza nesi mmojawapo kama alikuwa anafahamu tatizo langu lilikuwa nini lakini alinifanyia tu mzaha na kusema: “Umerudishwa. Labda ulifanya kosa fulani na unatakiwa kutubu.” Nesi alikuwa anajaribu kuelezea kwa lugha nyepesi namna hali yangu ilivyokuwa, lakini nilibaini kuwa alikuwa anaogopa kunikaribia. Nilimwomba aniitie daktari aliyenihudumia. 


Daktari alipofika, alisema kuwa hakujua kulikuwa na tatizo gani kwangu. Mwanzoni, alidhani kuwa nilikuwa na malaria lakini vipimo vilionyesha kuwa sikuwa nayo. Aliendelea kunieleza kuwa joto langu, mapigo ya moyo, na shinikizo la damu vilikuwa chini sana kwa viwango vya hatari lakini hakuweza kujua sababu yake. Alisema kuwa hakuwa na cha kufanya tena kwa ajili yangu. Hakuweza hata kuniandikia kulazwa maana sikuwa na ugonjwa. Dripu waliyoniwekea ilikuwa haifanyi kazi mwanzoni, lakini nilipofungua tu macho yangu, ikaanza kufanya kazi. Alipendekeza kuwa nesi aniwekee dripu nyingine mara ile ya kwanza itakapoisha ili niweze kupata nguvu za kutosha kwenda nyumbani.  


Niliogepeshwa na kile nilichoona mahali pale na sikuweza kujizuia kulia. Harufu mbaya ya pale iliendelea kuwa halisi kama nilipokuwapo hapo. Taswira za pale ziliendelea kunijia wakati wote. Nilishindwa kulala na mwili wangu wote ulihisi maumivu makubwa. Nilijihisi kana kwamba miguu na mikono yangu ilinyofolewa na kurudishiwa tena. Ah, nilijisikia vibaya sana. Nilikuwa na tumbo la kuendesha na kichwa kiligonga kwa wiki nzima.


Niliamua moyoni mwangu kwamba nisingemweleza mtu yeyote juu ya kile nilichoona maana ni nani kwanza angeniamini? Watu watanielewaje? Niliendelea kujiambia kuwa sitamweleza kamwe mtu yeyote juu ya mambo hayo. Mmoja wa washauri wangu alinipigia simu siku tatu baadaye kuulizia kuhusu hali yangu maana nilikuwa nimemtumia meseji aniombee. Bila kujitambua, nilijikuta nikimsimulia kuhusu yaliyonikuta. Niliposhtuka, tayari nilishamweleza karibu kila kitu. Nilitamani kujipiga mateke. Nilikuwa nalia kwa kuwa niliamini kuwa nimefanya kosa kubwa kabisa maishani mwangu. Sasa hadithi nzima ilikuwa wazi; hakukuwa na uwezekano wa kuificha tena. Sasa najua kuwa kama Mungu akitaka jambo fulani lielezwe, lazima litaelezwa. Maana yeye si ni Mungu?


***********


Agosti 19, niliamka huku nikijisikia hali ya upako kwenye mwili wangu wa nyama. Nilikuwa dhaifu na kutetemeka, huku mawimbi ya umeme yakipita kwenye mwili wangu. Jioni, niliona mwanga mkali ukija chumbani kwangu, na katikati yake, alikuwa yuleyule mwanamume. Safari hii alikaa chini kwenye kiti karibu na kitanda changu. Hata sielewi kiti hiki kilitoka wapi lakini kilikuwa pale mara tu alipokuwa tayari kukaa. Kilikuwa ni kiti kizuri cha dhahabu tupu. Umbo lake lilikuwa la kiti cha kawaida, kikiwa na sehemu ya kuegemeza mgongo. Kwenye kila mguu kulikuwa na nyota ya madini ya fedha iliyopachikwa kwenye dhahabu ile; nyota ileile ilikuwa pia katikati ya sehemu ya nyuma ya kuegemeza mgongo. Kulikuwa na magurudumu kwenye kila mguu.


Baada ya kunisalimia, aliniambia kuwa alijua kuwa nina maswali mengi kuhusu yeye ni nani; hivyo alikuja kujitambulisha kwangu na kufafanua mambo kadhaa ambayo tayari nilikuwa nimeyapitia. Alisema: “Mimi ni Yesu Kristo, Mwokozi wako. Kama una mashaka yoyote, tazama mikono yangu. Mahali pale ambako tulienda, ni Kuzimu.” Nilipoangalia mikono yake, niliona makovu ambamo misumari ilimtoboa.


Rafiki, napenda nikueleze kuwa kuzimu si sehemu ya kufikirika tu mawazoni; lakini ni mahali halisi na si kuzuri hata kidogo. Ni mahali ambako hakukutengenezwa kwa ajili ya wanadamu bali kwa ajili ya shetani na mapepo yake. Sehemu inayotustahili ni Mbinguni pamoja na Yesu lakini inatubidi tumchague Yesu kabla hatujachelewa. Leo, unapoisikia sauti yake, usifanye moyo wako kuwa mgumu; mkubali Yesu awe Mwokozi wako binafsi kisha uishi kwa ajili yake. Kuzimu ni kubaya mno: ni sehemu ya hofu na huzuni; ni sehemu ya mateso na vilio vya milele na kusaga meno. Shetani anataka awachukue watu wengi kadiri iwezekanavyo ili aende kule pamoja nao. Usishirikiane naye; shirikiana na Yesu nawe, badala ya kufa, utaishi.


Sikuelewa kwa nini Bwana aliniambia nichague kati ya makundi mawili aliyonionyesha kule kuzimu ilhali mimi tayari nilikuwa Mkristo niliyeokoka. Nimeshamkubali maishani mwangu lakini bado alikuwa akiniambia nichague kama nataka kwenda kuzimu au la! Sikuweza kuelewa. Nilianza kuomba na kumwuliza Mungu anipatie ufunuo juu ya kile alichomaanisha na ni nini anataka nifanye. Bwana alinifunulia kuwa nilikuwa nimeficha roho ya kutosamehe na chuki moyoni mwangu kwa sababu ya dada yangu mmoja, pamoja na binamu yangu mmoja. Nilimwomba Bwana anisamehe kutokana na kutosamehe kwangu. Pia nilimwomba dada yangu anisamehe kwa kuweka hasira na uchungu moyoni mwangu kwa ajili yake. Bwana alinielekeza niende pia nikamwombe msamaha binamu yangu.


Bwana pia alinikumbusha kuwa kulikuwa na wakati ambapo nilipata kazi ya ualimu kwa kutumia cheti cha diploma cha uongo na alihesabu hilo kuwa ni deni na wizi. Nilikusudia kutenda kilicho sahihi na nilimwomba anisaidie kutoka kwenye tatizo hili na anionyeshe njia rahisi ya kutoka humo maana hili lilikuwa ni kosa kubwa na lingeweza kunifannya nifungwe. Alinielekeza niende kwenye Idara ya Elimu nikakiri kosa nililofanya. Nilikuwa tayari kwenda jela kama ingebidi. Nilipata upendeleo wa Bwana kwa kiasi kikubwa sana. Nilipofika kule, mhusika kwenye Idara ya Elimu aliniambia niamue kile ninachotaka kufanya: ama kulipa mshahara ambao nilipokea kutoka serikalini au la. Waliahidi kuwa hawatanishtaki maana walishangazwa na kitendo changu cha kwenda kukiri kosa lile. Mungu wetu ni Mungu mwaminifu ambaye analiheshimu Neno lake.


Kama uko kwenye hali inayofanana na niliyokuwa nayo, napenda nikutie moyo kuwa utende kile kilicho sahihi, bila kujali matokeo. Unaweza kufungwa kwenye jela ya kidunia lakini hiyo ni ya muda tu. Hakuna maumivu au aibu inaweza kulinganishwa na kutengwa na Mungu milele. Kuzimu si mahali pazuri: ni bora kumruhusu Mungu akuhukumu sasa kabla hujachelewa. Hatutakiwi kuogopa hukumu ya Mungu tungali bado kwenye kipindi cha Neema; ni lazima tumruhusu afunue chochote kisicho sawa kwenye maisha yetu tungali bado na muda wa kuweka mambo sawa naye, maana hakuna msamaha upande wa pili wa kaburi.


Safari ya pili kuzimu


Oktoba 18, 2005, niliamka saa 11:30 asubuhi lakini sikuweza kwenda kazini. Nilijisikia hali ya udhaifu sana na  kulewa; sikuweza kusogea au kugeuka kitandani kwangu; na uwepo wa Bwana ulikuwa mzito sana chumbani. Nilikuwa natetemeka na nikahisi kama umeme ukipita mwilini mwangu. Bwana alinijia kabla tu ya saa 2:00 maana kwa mara ya mwisho nilipotazama saa ilikuwa ni saa 1:48; na Yeye alifika muda mfupi tu baada ya hapo. Alinisalimia na kusema kuwa tunatakiwa kwenda tena maana muda unaisha haraka sana. Nilisimama na tulianza kutembea. Utembeaji wa safari hii ulikuwa tofauti kabisa na safari zingine zote. Japokuwa miguu yetu ilikuwa inafanya kitendo cha kutembea, tulikuwa kama vile tunaelea zaidi kuliko kutembea. Wakati tukiwa njiani, Yesu aliniambia kuwa dhambi zote ni mbaya na hakuna kitu kama dhambi ndogo au dhambi kubwa. Dhambi zote mwisho wake ni mauti - ziwe kubwa au ndogo. Bwana aliniambia kwamba tunaenda kutembelea kuzimu tena na akaniuliza iwapo nilikuwa nina hofu. Nilimjibu kuwa nilikuwa nayo.


Alisema, “Roho ya woga haitoki kwa Baba yangu au kwangu; inatoka kwa Ibilisi. Woga utakusababisha utende mambo ambayo yatakupeleka kuzimu.” 


Bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu na hofu ni kinyume kabisa cha imani. Ni wazi kuwa hofu haimpendezi Mungu kwa kuwa inaharibu imani yetu. Muda wote tulipokuwa njiani, tulikuwa tunatembea kila mmoja peke yake. Lakini mara tu tulipofika kwenye lango la kuzimu, alinishika mkono wangu kwa mkono wake wa kulia kwa muda wote tuliokuwa kuzimu. Nilifurahi sana kwa Bwana kunishika mkono maana kwa namna alivyokuwa amenishikilia kwa nguvu, hofu yote ilitoweka. Sehemu ile ilikuwa bado iko vilevile: hakukuwa na tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Kulikuwa na wadudu, funza, joto kali sana, harufu, mifupa, kelele: kila kitu kilikuwa kama mwanzo nilipoenda pale. Tulipita tena kwenye geti lilelile baya na Bwana akanipeleka kwenye kundi moja la watu. Kulikuwa na watu wengi niliowafahamu wakati wangali duniani. Maskini, walikuwa kwenye hali mbaya sana. Walionekana ni wenye taabu na maumivu makubwa; lakini baya zaidi ilikuwa ni nyuso zao zisizo na matumaini kabisa.   


Bwana alimwonyesha mwanamke mmoja wa makamo ambaye nilimfahamu kabla hajafa. Alikufa kwa ajali ya gari mwanzoni mwa mwaka 2005. Nilipigwa na butwaa kumwona pale maana sote tulimjua kuwa ni mtu aliyekuwa na hofu ya Mungu na aliyempenda Mungu. Bwana aliniambia kuwa mwanamke yule alimpenda na Yeye Bwana naye alimpenda; alimwokoa angali akiwa duniani; aliwashuhudia wengi ambao walimwijia Bwana na alifahamu Neno vizuri sana. Alikuwa mkarimmu kwa maskini na wahitaji; aliwapatia walichohitaji, na kuwasaidia kwa njia nyingi. Alikuwa ni mtumishi mzuri wa Bwana kwa namna nyingi.


Maneno hayo ya Bwana yalinishitua hata zaidi; nami nikamwuliza kwa nini amwache mtu kama huyo aliyemtumikia kwa kiasi kikubwa hivyo aingie kuzimu? Bwana alinitazama na kusema kuwa mwanamke yule aliamini uongo wa Ibilisi. Japokuwa aliyajua Maandiko vizuri, aliamini uongo wa ibilisi kwamba kuna dhambi ndogo na kubwa. Alidhani kuwa dhambi ‘ndogo’ zisingempeleka kuzimu, maana alikuwa Mkristo hata hivyo.


Bwana aliendelea kusema, “Nilimwendea mara nyingi na kumwambia aache kile alichokuwa anakifanya lakini mara nyingi alijenga hoja akilini mwake kuwa kile alichokuwa anakifanya kilikuwa ni kidogo sana na alichukulia kuwa yale maonyo yangu yalikuwa ni hisia zake tu za hatia. Kulikuwa na muda ambapo aliacha kwa muda lakini baadaye alijishawishi tena kuwa maonyo yale hayakuwa yanatoka kwangu, bali ni sauti yake tu kwa kuwa aliona kuwa dhambi ile ilikuwa ni ndogo sana kuweza kumhuzunisha Roho Mtakatifu.”


Nilimwuliza tena Bwana ili aniambie ni dhambi gani basi mwanamke yule alitenda. Alinijibu kwamba, “Mwanamke huyu alikuwa na rafiki ambaye alikuwa nesi kwenye Hospitali ya Oshakati. Kila mwanamke huyu alipoumwa, hakwenda hospitali na kulipa kwa ajili kadi yake kama inavyotakiwa kwenye taratibu za kawaida; badala yake yeyé alipiga tu simu na kumwambia rafiki yake amfanyie mipango ya dawa kutoka kwenye  Zahanati ya Hospitali. Na mara zote rafiki yake yule alikubali na kumwambia kuwa apite pale muda fulani kuchukua dawa. Kwanza, aliamua kukubali uongo wa ibilisi juu ya kuwapo kwa dhambi kubwa na ndogo na kuikataa kweli yangu; alimsababisha mtu mwingine atende dhambi na kuiba kwa niaba yake, lakini kibaya zaidi, ALIMHUZUNISHA ROHO MTAKATIFU. Hicho ndicho kilichomfanya afike kuzimu. Haijalishi kwamba utaleta mamilioni ya roho kwa Bwana; bado upo uwezekano wa kuingia kuzimu kutokana na kumhuzumisha Roho Mtakatifu. Si tu kwamba ni lazima ujali wokovu wa wengine lakini pia ni lazima uwe mwangalifu usije ukasahau roho yako. Kuwa makini na Roho Mtakatifu wakati wote.” Baada ya maneno hayo, Bwana alisema ni wakati wa kurudi.


************


Wakristo wengi waliosikia hadithi yangu hii huiona kama ina matatizo. Mara nyingi huwa wanniuliza, “Vipi kuhusu kuhesabiwa haki, rehema, na neema?” na pia “Inawezekana kweli kupoteza Wokovu wako baada ya kuwa umeupokea?”  
“Huko si kuvuka kiwango?”
“Mungu anaweza kuwa mkatili kiasi hicho?”


Kama nilivyosema kwingineko kwenye kitabu hiki, mimi siongei theolojia yangu hapa. Ninasema tu kile ambacho Bwana alinionyesha na kunifundisha – na kile alichoniruhusu kukishuhudia. Tafadhali someni Biblia zenu ili kupata majibu. Tazama aya zifuatazo, kisha uhukumu mwenyewe.


“…bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.”(1Wakorintho 9:27)


Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?(Warumi 6:1-2)


Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake.” (Warumi 6:12)


Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. (Waebrania 10:26 –27)


Unasema, “Je, naweza kwenda kuzimu baada ya kuwa nimemtumikia Bwana na kuwaleta wengi kwa Kristo?” Hukumu mwenyewe!


Kutokutii


Jumatatu ya tarehe 6 Machi 2006, niliamshwa na saa ya kengele saa 11:30. Nilianza kuomba na nikatambua kulikuwa na upako mzito juu yangu. Mwili wangu ulikuwa dhaifu na nilikuwa nikitetemeka; mawimbi ya umeme yalikuwa yanapita kwenye mwili wangu.


Wakati wa mchana, nikiwa nimelala kitandani, niliona nuru nyeupe ikijaza chumba changu. Niliona shanga ndogondogo, nyeupe, za duara, zenye ukubwa wa kichwa cha pini. Shanga hizi zilikuwa zikianguka kama mvua inavyonyesha na zilipogusa ngozi yangu, zilizama ndani. Zaidi ya hapo, niliona kama wingu linalofanana na ukungu mweupe likija kutokea juu. Nalo pia lilikijaza chumba na likawa likizama kwenye ngozi yangu kila liliponigusa. Baada ya hapo, nilimwona Yesu akitembea katikati ya lile wingu la ukungu kuelekea pale nilipokuwa. Alikaa kwenye kiti chake pembeni mwa kitanda changu. Hata sielewi kiti hiki kinatokea wapi; huwa kinatokea tu mara anapokuwa tayari kukaa.  Ni kiti kizuri kilichotengenezwa kwa dhahabu. Umbo lake ni kama la viti vingi tunavyovifahamu lakini kina sehemu ya kuegemeza mgongo. Kwenye kila mguu kuna nyota ya fedha; na nyota nyingine ya aina ileile, japo ni kubwa zaidi, iko kwenye sehemu ya kuegemea. Kuna magurudumu kwenye kila mguu.


Yesu alinisalimia na akaninyooshea mkono wake na kuniambia niamke maana muda unakimbia haraka sana. Alinivuta mkono wangu nami nikainuka na kukaa kitandani kwangu.


Kisha akaniambia, “Victoria, tuombe.” Aliomba kwa lugha ambayo siielewi; nilielewa neno moja tu ‘Amen’. Kisha aliendelea kwa kuniuliza nilikuwa naona nini nami nilimwambia kuwa nilikuwa naona kundi la watu wakienda kazini kwao na wengine wakirudi kutoka kazini kwao. Nilikuwa pia naona vile vishanga vyeupe vikiwaangukia wale waliofika mwanzo kazini kwao. Baada ya kundi la kwanza, kundi jingine nalo lilifika baadaye.  Wakati huo, ile mvua ya vile vishanga iliacha kunyesha.


Niliona pia makundi mbalimbali ya watu, wakiwasili kwenye makanisa mbalimbali Jumapili asubuhi. Mvua ile ingeanza kunyesha mara tu watu wa mwanzo wanapoingia kwenye uwanja wa kanisa. Iliendelea kunyesha kwa muda kisha ikasimama. Wale wanaochelewa hawakuti chochote.  


Yesu aliniuliza iwapo nilikuwa naelewa maana ya maono yale, nami nilimwambia kuwa sikuelewa. Ndipo alinifafanulia kwa kusema kwamba: “Maono haya yanamaanisha kuwa kila mahali ambako unatakiwa kuwako kwa muda fulani na wewe unajua ni wakati gani unatakiwa kuwa pale, mara zote huwa kuna malaika wanagawa baraka kwa ajili ya muda huo. Kama ukifika mapema, utapokea baraka zako, lakini ukichelewa, unakosa baraka zako kwa siku ile maana malaika hugawa baraka kwa muda ule tu. Victoria, nataka kukuonya kwa sababu huwa unaenda kazini kwa kuchelewa, na hasa huwa unaenda kanisani kwa kuchelewa. Ni lazima ujue kuwa kwa nyakati zile huwa unachelewa bila kuwa na sababu za msingi; umekuwa ukikosa baraka zako kwa siku zile; hazitakurudia tena.  Victoria, ni lazima uache jambo hili na usilitende tena, isipokuwa pale unapokuwa na sababu ya msingi ya kuchelewa.”  


Bwana alipomaliza kusema maneno yale, kwa kweli nilitamani kutoweka au angalau nimpatie sababu inayokubalika kutokana na kukosa kwangu nidhamu. Nilimwambia kuwa wakati mwingine napitiliza kulala lakini alinitazama moja kwa moja machoni na kusema kuwa nilikuwa nasema uongo na kwamba nilikuwa nina tabia mbaya ya kurudi kitandani baada ya kuwa nimeamka, ili kutimiza ile shauku ya kusema ‘ngoja nilale kidogo tu.’


Baada ya Yesu kuwa amenionya. alisema, “Simama. Tuondoke sasa. Muda unakimbia haraka sana. Kuna mambo ambayo ni lazima tuyafanye.”


Safari hii Bwana alinipeleka mahali ambako sikuwahi kufika kabla. Ilikuwa pia ni mara ya kwanza kufuata barabara tuliyotembea siku ile. Tulifika kwenye bustani iliyojaa maua mazuri na miti mizuri ya kijani. Hakuna kitu duniani kinachoweza kulingana na mahali pale. Maua yalikuwa ya kila aina ya rangi za kung’aa.  Tulikaa kwenye benchi zuri la bustanini, ambalo lilitengenezwa kwa dhahabu safi huku likiwa na nyota ndogo za madini ya fedha ya kung’aa.


Tulipokaa, alionyesha kidole mbele na kusema, “Victoria, tazama, unaweza kuona mji ule?”  Nilipotazama, niliona jiji kubwa sana. Lilikuwa zuri kuliko maelezo. Jiji lile lilikuwa na geti la dhahabu inayong’aa, na kwenye geti lile kulikuwa na mwanamume amekaa, mwenye umri mkubwa. Alikuwa na ndevu ndefu nyeupe na nywele nyeupe. Nilishamwona mwanamume huyo kabla; na nilipomwuliza Yesu kuwa mwanamume yule ni nani, aliniambia kuwa alikuwa ni Ibrahimu, baba wa imani.

Niliona barabara nyingi kwenye mji ule, ambazo nazo ni za dhahabu. Kuna majengo marefu, ambayo nayo yalikuwa ya dhahabu inayong’aa. Mng’ao wa mji ule hata hauelezeki!


Yesu alinigeukia na kuniuliza, “Unawaza nini juu ya jiji lile?”


Nilimjibu kuwa lilikuwa ni zuri sana na nilikuwa natamani kwenda pale. Yesu alisema: “Nitakupeleka pale kama ukiendelea kuwa mtii maana hapo pia ndiko nyumba yako itakakokuwako. Uendelee tu kuwa mtii – maana ukikosa utii, Victoria, kunguru wataruka kwenye nyumba yako. Nyumba yako itakuwa makao ya bundi na viwanja vya kuchezea vya mizimu. Hata hivyo, usiogope, maana mimi niko pamoja nawe. Wewe uwe mtii tu. Kwa kila mmoja ambaye si mtii, nyumba yake itakuwa na kunguru wakiruka pale; itakuwa ni makao ya bundi na mahali pa mizimu pa kuchezea.”


Yesu ni halisi na anatupenda kwa pendo lisiloweza kuelezeka. Shauku yake kubwa ni sisi tuchague uzima na kuishi milele naye. Moyo wake unauma kwa ajili ya wale watu ambao wanakufa na kuenda kuzimu kwa vile tu wanachagua kukataa Wokovu aliowapa na badala yake wanachagua mauti.


Uwe ni Mkristo uliyeokoka au la, tafadhali siku zote kumbuka jambo hili: Muda unakimbia haraka!


**********************

Mpendwa msomaji wa blog hii, kama ungependa kusoma au kusikiliza ushuhuda huu kwa Kiingereza, bofya HAPA. Mungu wa mbinguni akubariki na kukutia nguvu.

Tuesday, August 18, 2015

SIKU ZA MWISHO BWANA YESU ATARUDI ATACHUKUA WALIO WAKE






















Mojawapo ya jambo ambalo halijawahi kuzoeleka na wala halitazoeleka, ni kifo. Kifo amekuwa adui mkubwa mno wa mwanadamu. Ingawa wakati mwingine mwanadamu apatwapo na mambo magumu sana hutamani kifo, lakini ukweli ni kwamba bado ni jambo lisilozoeleka.
Hakika ndugu unayesoma ujumbe huu kama hujawaho kufiwa na wazazi wako, basi umefiwa na kaka, dada ama wadogo zako. Kama katika hayo yote bado, basi umefiwa na rafiki yako mliyependana sana. Kama hamna, basi umefiwa na mke, mme au mchumba wako mliyetarajia kuoana. Hakika kwa kila namna sote tumeumizwa na kifo. Hivyo kifo ndo maana hakijawahi kuzoeleka.
Lakini hivi kweli kifo kitaacha kutuua au kutuulia jamaa zetu lini? Mara nyingi maswali magumu yasiyo na majibu huulizwa na wafiwa, "Nitampata wapi mtu mwingine kama huyu?" "Mbona afe huyu na wala si wengine, hivi MUNGU nimemkosea nini mimi?" Kama watu hao wakikosa majibu katika maswali yao magumu, hujiingiza katika mambo mabaya kama kunywa pombe, kuvuta bangi na kula madawa ya kulevya wakifikiri kwamba huenda vitu hivyo vitatuliza huzuni zao kuu.
Lakini sisi wafanya kazi wa ukurasa huu wa "Matukio Ya Mwisho Wa Dunia" kwa nguvu za MUNGU Atupendae tunakuleteeni habari za Matumaini;
"Ndugu zenu wote walio kufa mtawaona tena"
Habari hii ni ya uhakika wala si ya mashaka. Twatamani mkumbuke kwamba haya matukio magumu yanayotokea duniani ni ishara ya dunia kutetemeka kwa sababu kuna Mmoja Anakuja akiwa na mng'aro wa kama mwanga wa jua mara bilions. Huyo ni YESU KRISTO Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana na Rais wa marais. Huyo ndiye Anayekuja kukomesha kifo maana Yeye ni kiboko ya kifo kwa sababu kifo kilijaribu kummeza lakini baada ya siku tatu hakukiweza kuendelea kumshikiria kwa vile Yeye ni Shujaa. Na Alipokuwa akitoka kaburini alituthibitishia kuwa anao tayari ufunguo wa kifo hivyo Atakaporudi kifo ni kukiangamiza kifo kabisa. KRISTO Atafuta machozi yetu huku akitupa pole kwa kujibu maswali yetu magumu tuliyohoji juu ya kifo.
Mpendwa, pamoja na kwamba ujumbe wetu wa leo umekuwa mrefu kiasi, lakini tunapenda tumalizie kwa kusema kwamba; Hatuna budi kusisitiza ndugu, kaka, dada, mjomba, shangazi, bibi na jamaa zetu wengine kumwamini huyu YESU Ajaye ili akisha kuja tupate kufurahia sote kwa kuishi milele bila kifo maaana lazima tuseme ukweli huu ili watu tusije tukabweteka.
Ukweli ni kwamba wale ndugu zetu ambao hawakumwamini YESU na kufa dhambini, watafufuliwa ndiyo lakini baadae watachomwa moto na kubaki majivu tu wala kumbukumbu lao halitakuwepo kabisa.
Mfariji Wa Ajabu's photo.
Hivyo kwa vile twaamini wawapenda ndugu na jamaa zako, usiwaonee aibu kuwaasa wamwamini KRISTO ili hata wafapo, wawe na sehemu yao katika ufufuo wa kuingia maisha mapya yasiyo na machozi, mauti, maombolezo, vilio na maumivu.

Sunday, August 9, 2015

SIFA ZA UPENDO WA KIUNGU (AGAPE)



BWANA YESU Asifiwe ndugu msomaji, leo tupitie somo kuhusu Upendo wa Kiungu (AGAPE) na sifa zake. 2WAKORINTHO 13:1-13.
Upendo wa Kiungu ni hali ya kupenda mtu bila kujali mtu huyo alivyo au ana sifa gani.
*Mtu aliye na Upendo huu huchukuliana na kila mtu pasipo kujali tabia yake au sifa zake.
*Mtu aliyeokoka na kujazwa Roho Mtakatifu anao Upendo huu.
*Upendo ni Sifa na Amri kuu ya mtu aliyeokoka.
*Huu ni Upendo wa kipekee tofauti na Upendo wa kidunia tunaoufahamu ambao mtu hupendwa kutokana na jinsi alivyo, pesa zake,mali zake, umaarufu wake, cheo chake, n.k. Upendo huu ni zaidi ya hapo.
- Tukumbuke kuwa sisi sote tulikuwa wenye dhambi na wenye uchafu wa kila aina lakini Upendo huu Alionao Mungu Baba, haukujali hayo yote tuliyokuwa nayo, bali Yeye Alilipa gharama ya kumtoa Mwanawe wa Pekee, Yesu Kristo, Mungu Mtakatifu, Akajitoa sadaka kwa ajili Yetu wenye dhambi. YOHANA 3:16
- Hii inatufundisha jambo la kipekee sisi tuliopokea Upendo huo, basi nasi tuudhihirishe kwa wale wasiomjua Kristo, ili wavutwe waokoke.
SIFA ZA UPENDO WA KIUNGU (AGAPE)
*Upendo huvumilia
*Hufadhili
*Hauhusudu
*Hautakabari
*Haujivuni
*Haukosi kuwa na adabu
*Hautafuti mambo yake
*Hauoni uchungu
*Hauhesabu mabaya
*Haufurahii udhalimu
*Hufurahi pamoja na kweli
*Huvumilia yote
*Huamini yote
*Hutumaini yote
*Hustahimili yote
*Haupungui neno wakati wowote
>Hizi ni sifa za kipekee ambazo twahitaji kumwomba Roho Mtakatifu Atuwezeshe kuwa nazo ili tuweze kufika Mbinguni.
1PETRO 4:8 'Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi'
MUNGU AKUBARIKI SANA!

BWANA YESU HUFANYA NJIA PASIPO NA NJIA

**MUNGU HUFANYA NJIA PASIPO NA NJIA***
Wakati fulani tunakutana na majaribu, matatizo, shida na vikwazo kiasi cha kudhani hakuna njia nyingine ya kutuwezesha kusonga mbele. Leo naomba nikukumbushe kuwa Mungu hufanya njia na kuleta suluhisho wakati ambapo huonekana kama hakuna kabisa njia au suluhisho. Mungu siku zote huleta utatuzi kwa tatizo lolote tunalokutananalo na kufanya mlango kwa jaribu lolote linalotupata kwa kuridhia kwake (1 Wakorintho 10:13; Mwanzo 22:9-14)
Usiambiwe kitu fulani hakiwezekani ukaamini, kwani siku zote ipo njia. Huwezi kushindwa usipokata tamaa. Jiamini, chukua hatua na usikate tamaa katika kutafuta utatuzi wa tatizo, shida au hali yoyote inayokusumbua katika maisha yako kwani kila muda, kila hali, kila tukio na kila jambo huleta uwezekano na fursa ya kufanya kitu kitakachokuwezesha kusonga mbele na kuleta mabadiliko katika maisha yako.
Kataa kukwamishwa au kuyumbishwa na matatizo na vikwazo toka kwa mwovu shetani ambaye tunashindana naye kila siku na badala yake mwombe Mungu akujaze ufahamu na hekima za Kiroho ili uweze kuzijua na kuzifuata njia zake; (Kutoka 33:13; Zaburi 86:11) Naye atakuonyesha njia na asipokuonyesha atakuwezesha kuifanya njia, kuvivuka vikwazo na kuzishinda changamoto unazokutana nazo.
Katika Jina la Yesu Kristo ninakuombea mafanikio katika hili!

JIFUNZE KWA NDEGE TAI

NDEGE TAI JIFUNZE KWAKE
Ninampenda Yesu's photo.

Tai huwa hapambani na nyoka juu ya ardhi. Yeye humnyakuwa na kwenda naye juu sana angani, na hivyo kubadilisha uwanja wa mapambano, halafu humshambulia na kumwachia adondoke chini ardhini. Nyoka huwa hana 'stamina', hana nguvu, wala ‘balance’ akiwa hewani. Huwa mdhaifu, mwepesi kudhurika na asiye na uwezo wa kufanya chochote tofauti na awapo juu ya ardhi ambapo huwa ni hatari, mjanja na mwenye nguvu.
Nawe kama mwana wa Mungu, unapokutana na adui zako na kupigwa vita hamishia mapambano yako katika ulimwengu wa Kiroho ambapo Mungu huchukua nafasi. Usipambane na changamoto zako katika ulimwengu wa kimwili; Jifunze kwa Tai na kubadili uwanja wa mapambano kama yeye. Hapo ndipo utakuwa na uhakika wa ushindi usio wa upinzani. Omba na umwachie Mungu ingilie kati.
Lakini unapopambana katika ulimwengu wa Kiroho kumbuka; kutegemea nguvu za Mungu, sio nguvu zako (2 Wakorintho 10:3) kwa sababu kushinda vita hii hauhitaji nguvu za kimwili, bali akili ya kiroho, kukemea kwa jina la Yesu (Matendo Ya Mitume 19:13-17), kukaa ndani ya Yesu na kujikinga kwa kuvaa silaha zote za Mungu (Yohana 15:7, Warumi 13:12-14 na Waefeso 6:10-18), kupigana vita kwa upanga wa roho ambao ni Neno la Mungu, na mwisho kukumbuka kwamba, unapopigana vita vya kiroho na Shetani na mapepo yake, sio kila dhambi au taabu ni pepo ambalo linahitaji kukemewa.
Ngoja nikupe simulizi moja niliyowahi kusimuliwa na mdogo wangu Loveness Mlay; Kuna siku wanamaombi walikuwa wakimwombea binti mmoja aliyekuwa akipiga kelele kama aliyepagawa na pepo; kwa muda mrefu walimwombea na kukemea lakini mapepo hayo hayakutoka, Mchungaji alipokuja akawanong’oneza kuwa anaona huyo binti hana pepo kwa hiyo watoke nje ya chumba na wamwache pekeyake kwa muda… Baada ya muda kidogo kupita binti akiwa ameachwa pekeyake akaacha kupiga zile kelele kama wafanyavyo wapunga pepo, kukawa kimya; nao walipochungulia wakamuona binti akiangaza macho ili kuona kama kuna mtu karibu anamwangalia; alipoona hakuna mtu akainuka na kuondoka zake. Kwa hiyo umwonapo mtu akipiga kelele kama wapunga pepo wafanyavyo mtazame kwa macho ya rohoni kwani wengine hujifanyisha na unapokemea kelele zao unatumia nguvu za Mungu vibaya.
Ila pia unapoona kama vita ni ngumu kwako kumbuka vita si yako bali ni ya Mungu, (2 Mambo Ya Nyakati 20:14-15) kwa hiyo yakupasa upigane kwa imani!
Ninamwomba Mungu akusaidie kufanikiwa kwa hili katika Jina la Yesu Kristo!

JIFUNZE MAARIFA ACHA KIBURI

***JIFUNZE KWA EDOMU USIDANGANYWE NA KIBURI***
Ninampenda Yesu's photo.

Obadia ni kitabu ufupi katika Agano la Kale, kina sura 1 na mistari 21 tu! Kinatangaza adhabu ya Mungu dhidi ya taifa la kale na lililosahaulika kwa muda la Edomu; na kumfanya Obadia kuwa mojawapo wa manabii watatu tu ambao walitamka hukumu juu ya mataifa mengine; wengine wakiwa ni Nahumu Habakuki. Lakini kuna zaidi ya hicho kwenye kitabu hiki. Wakati vitabu vingine vya kinabii vina kurasa zenye mistari ya hukumu juu ya Edomu na mataifa mengine, lengo kuu la Obadia japo wengi wetu inatuwia vigumu kulielewa ni ukweli kuhusu uhusiano wa ubinadamu na Mungu.
Ili kumwelewa vizuri Obadia, tunahitaji kurudi nyuma hadi katika kitabu cha Mwanzo. Tunaanzia kugusa Mwanzo 12:1-3 pale Mungu alipomuahidi Ibrahimu kuwa atawabariki watakao mbariki na kuwalaani watakao mlaani. Halafu Mwanzo 21:12; 26:24 pale baraka zilipohamishiwa kwa Isaka mwana wa Ibrahimu. Halafu Mwanzo 25: 23-26 pale baraka hizi zinapokuja kwa mmoja wa wana mapacha wa Isaka.
Katika Mwanzo sura ya 25, kuanzia na mstari wa 23, tunajifunza kwamba Rebeka mke wa Isaka alikuwa na ujauzito wa watoto mapacha. "Bwana akamwambia, “Mataifa mawili yamo tumboni mwako; makabila mawili yatakayozaliwa nawe, yatafarakana. Moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine; mkubwa atamtumikia mdogo.” Hapa Mungu alikuwa akimaanisha mapacha Yakobo na Esau. Esau alikuwa wa kwanza kuzaliwa, hivyo yeye alikuwa na haki juu ya urithi toka kwa baba yake. Lakini Yakobo akamdanganya ndugu yake na kumpatia haki ya kuzaliwa badala yake kwa bakuli la supu. Lakini ukifikiria utaona Esau hakufurahishwa na hili, hivyo alijenga chuki dhidi ya ndugu yake.
Baada ya muda kupita tunasoma kuwa Yakobo anaoa na kuwa na watoto kumi na moja. Siku usiku mmoja akiwa peke yake, alikutana na mtu, akapigana naye mwereka mpaka alfajiri. Mtu huyu alipomwambia Yakobo amwache aendezake, Yakobo akamwambia kwamba hawezi kumwacha mpaka ambariki! Katika hatua hiyo, mtu huyo alimbadilisha jina Yakobo... Jina lake sasa likawa Israeli. (Mwanzo 32:24-28)
Hapa sasa unaweza kupata kitu! Yakobo akawa Israel. Yakobo akaanzisha taifa la Israeli mara baada ya jina lake kubadilishwa; halafu akapata mwana mwingine – wakawa wana 12 ambao ni makabila 12 ya Israeli.
Tukimgeukia Esau tunajifunza nini? Esau alianzisha taifa la Edomu; na Edomu lilikuwa taifa la Wayahudi, kutoka kwa Ibrahimu. Na uchungu kati ya mataifa mawili hakuacha hata wakati Esau alipokufa. Katika 1 Samweli 14, Sauli anapigana vita dhidi ya Edomu. Katika 2 Samweli 8, Daudi alishinda vita dhidi ya Edomu. Katika 2 Wafalme 8 Edomu waliiasi Israeli. Isaya sura ya 34 alisema kuwa hukumu i juu ya Edomu. Yeremia katika sura ya 49 alisema kuwa Mungu ataleta msiba kwa Edomu. Ezekia katika sura ya 35 alisema kuwa Mungu ataiweka miji yao katika uharibifu. Malaki na Maombolezo pia vinataja uharibifu wa Edomu. Na sasa, Obadia.
Lakini tujiulize; kwa nini Mungu ailaani Edomu na si taifa jingine lolote? Je, nchi hii ya Esau imefanya nini hata istahili hukumu hiyo?
Obadia katika mstari huu hapa chini anatujibu swali hili;
Kiburi cha moyo wako kimekudanganya,
Wewe ukaaye katika pango za majabali,
Mwenye makao yako juu sana;
Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi? (Obadia 1:3)
KIBURI NI TATIZO KUBWA LA EDOMU.
Kiburi ni chanzo cha maovu yote ya binadamu. Mithali 6:16 neno linasema; “Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.” Kitu cha kwanza kabisa kwenye listi ni nini? “Macho ya kiburi” vingine vyote vinatokana na kiburi.
Kwa mwanadamu kiburi huja kwa aina mbalimbali. Katika kitabu cha Obadia tuonaona aina mbalimbali za viburi;
Aina mojawapo ya kiburi ni MAJIVUNO.
Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?
Ujapopanda juu kama tai,
Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota,
Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana. (Obadia 1:3,4)
Katika kujiona au kujivuna tunapata picha ya mtu ambaye anasema, "Hakuna mtu anaweza kunifanya chochote. Mipango yangu yote na kila kitu changu kiko sawa. Sihitaji msaada wa mtu yeyote. Nina uwezo wa kufanya chochote bila kumtegemea mtu”
Tabia hii ya kujiona na au kujivuna ni alama ya kiburi. Naye Bwana anasema kwamba " Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko.”
Kibuli hutufanya tusione umuhimu wa uwepo wa Mungu. “Naweza kuendesha maisha yangu, kwa hekima yangu mwenyewe, kwa nguvu zangu mwenyewe, kwa uwezo wangu mwenyewe, kwa kipaji changu mwenyewe...Mungu wa nini?”
Kujiona kunaonekana kwa Mkristo ambaye anamuhitaji Mungu katika nyakati za hatari na hofu na shinikizo tu, na si katika nyakati nzuri. Ngoja nikupe story moja:
“Kuna jamaa alikuwa anaezeka paa la nyumba yake, kwa bahati mbaya akateleza na kuanzwa kuseleleka kuelekea ukingoni mwa paa. Huku akiteleza jamaa akawa anamwomba Mungu; Mungu nisaidie, Mungu nisaidie! Alipokaribia ukingoni mwa paa msumari ukadaka nguo yake; na kumfanya asiendelee kuteleza. Jamaa akamwambia Mungu; “Usijali Mungu nimeshajizuia nisianguke”
Wakristo tunapaswa kuelewa kwamba pale tunapoona kuna kitu chochote kwenye maisha yetu tumekipata au tunaweza kukifanya bila msaada wa Mungu; tunautukuza mwili na kujihusisha na kiburi cha Edomu. Hata kama wewe ni tajiri kwenye biashara zako, kiongozi kwenye jamii au jumuia yako, bosi ofisini au mtumishi kanisani; hakuna unachoweza kufanya bila kumtegemea Mungu.
Aina nyingine ya kiburi ni UDHALIMU;
“Kwa sababu ya udhalimualiotendwa ndugu yako Yakobo, Aibu itakufunika, nawe utakatiliwa mbali hata milele.” (Obadia 1:10)
Mtu anayempiga mkewe, anayemnyanyasa mwingine kijinsia, anayemnyanyasa mtoto, anayedhulumu mali za yatima, na wengine wanaofanya matendo yanayofanana na hayo, wanafanya udhalimu. Kiburi ni kiini cha ubinafsi na hupambana na kufanya udhalimu dhidi ya chochote au yeyote anayethubutu kutoa changamoto juu ya utawala wake mkuu katika maisha.
Aina nyingine ya kiburi ni KUTOJALI;
“Siku ile uliposimama upande, siku ile walipochukua mali zake, na watu wa kabila nyingine walipoingia katika malango yake, na kutupa kura juu ya Yerusalemu, wewe nawe ulikuwa kama mmoja wao.” (Obadia 1:11)
Kutojali ni kusimama na kutazama tu wakati mwingine akipata matatizo badala ya kumsaidia. Kutojali ni aina ya kiburi. Kutojali ni chanzo cha matatizo mengi katika ndoa na mahusiano. Kwenye migogoro mingi ya ndugu na wanandoa utasikia maneno kama; hanijali, ananipuuza, hanisikilizi, hapendi vitu ninavyovipenda na mengine yafananayo na hayo. Hayo yote yanaendana na kutojali ambayo ni sababu moja wapo ya Mungu kumchukia Esau. Wakristo hatupaswi kuwa watu tusiojali.
Aina nyingine ya kiburi ni MASIMANGO;
“Lakini usiitazame siku ya ndugu yako, siku ya mashaka yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao, wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao” (Obadia 1:12)
Mungu anamhukumu Edomu kwa kusimanga na kubeza ambavyo vinatokana na kosa lake la kiburi. Watu wengi tunakiburi cha kubeza au kusimanga wenzetu wanapopata matatizo. Utasikia; “nilikwambia, nilijua tu, ndio ukome, umejitakia na mengineyo ambayo yote ni maneno ya yanadhihirisha tabia ya kubeza, kusimanga na kukejeri ambavyo hutokana na kiburi cha Edom. Tunayafanya au kuyasema haya pale wenzetu wanapopatwa na matatizo wakati sisi tuko salama, ila yanatokana na kiburi ambacho ni chukizo kwa Bwana.
Aina nyingine ya kiburi ni UNYONYAJI
“Wala usisimame penye njia panda, ili kuwakatilia mbali watu wake wakimbiao; wala usiwatoe watu wake waliosalia katika siku ya dhiki.” (Obadia 1:14)
Wakati Waisraeli walipotoka Misri na kutaka kupita katika nchi ya Edom; Waedomi waliwazuia. (Hesabu 20:14-21) Walipofikwa na majanga, Edomu alitumia nafasi hiyo kujifaidisha. Waedomi waliwateka, wakichukulia faida ukweli kwamba hawa walikuwa wakimbizi, na kutumia shida zao na mateso yao kwa faida yao wenyewe. Kuna mifano mingi ya hili katika maisha ya kila siku. Mmoja wapo ni kumshawishi mtu mwenye shida auze kitu chake kizuri ili ukinunue kwa bei ya chini au aweke rehani ili akishindwa kulipa umuongezee fedha kidogo uwe umekipata kwa bei rahisi. Mungu anachukia tunapoutumia udhaifu wa mwingine au bahati mbaya ya mwingine kwa faida yetu.
Hiyo ni baadhi tu ya mifano inayosababisha chuki ya Mungu kwa Edomu. Lakini mkubwa katika hiyo ni pale Obadia anaposema; “Kiburi cha moyo wako kimekudanganya” (Obadia 1:3)
Kiburi ni kibaya. Kinatudanganya, kinatutega, kutunasa na kutufanya tusijitambue hadi pale tunapopatwa na matatizo. Wakati mwingine tunaendelea kujivuna, kujisikia na kuamini mambo yetu yako sawa hata pale ambapo watu wengine wanaona tunaharibikiwa na kupotea. Pengine tunaambiwa kabisa lakini kiburi kinatufanya kushupaza shingo mpaka mambo yanakwenda mrama kabisa.
Unabii wa Obadia unalenga katika nguvu ya uharibifu wa kiburi. Unatukumbusha matokeo ya kuishi kwa namna binafsi ya kujiona wenyewe, ya kuzifuata hisia na tamaa zetu wenyewe bila kuzingatia athari zake kwa wale walio karibu nasi. Ingawa kiburi kimekuwa sehemu ya maisha na maanguko ya mwanadamu tangu janga la kuanguka katika Edeni, Obadia anatukumbusha kujiweka chini ya mamlaka ya Mungu, kuzitumi hamu zetu kwa makusudi yake, na kupata tumaini letu katika kuwa watu wake wakati wa wa kuhukumiwa na kufanywa upya vitu vyote utakapokuja.