Menu

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo

Sunday, October 25, 2015

KUSIFU NA KUABUDU

FAHAMU NINI A KUSIFU NA KUABUDU KATIKA BIBLIA

 Mt. Meshack Ezekia Kitova    phone;0757672626

 Nini maana ya kusifu na kuabudu


KUSIFU NA KUABUDU ni maneno tofauti na yana maana tofauti
1. kusifu

MAANA --- nikuelezea wasifu au wajihi za kitu au mtu. Sasa tunaposema tunamsifu Mungu inamaanisha ni KWA KUMUINUA JUU, KUSHUKURU KUMPAZIA SAUTI,KUFANYIA SWANGWE, KUJISHUSHA CHINI YAKE KWA UNYEYEKEVU,nk Zaburi 100:4

Neno hili kusifu kwa kiebrania lilikuwa na maana ya;
Tehila, yaani kutamka neno kwa kuongeza vionjo na mbwembwe zaidi. Mfano neno haleluya unalitamka (Ha, ha leluya huuu eee) Tehila ni kuwa kama kichaa unaposifu au kuabudu kwa utukufu wa Bwana. (Nilidhani labda hapa ndipo waswahili walipopata neno taahila).

Yadaa yaani kujiachia kwa Mungu (you just surrender yourself to the Lord).
Barak yaani kusaluti mbele za Bwana. Ni kuonyesha kwamba ni yeye peke yake anayestahili heshima na utukufu. Huwezi kumpigia saluti mtu usiyemwona, hivyo ni kwa njia ya kumwabudu Mungu katika roho na kweli ndipo tunapomwona kama alivyo na utukufu wake

2. Kuabudu 
Neno la Kiebrania shachah lina maana ya kuabudu, kusujudia, kuinama kwa kuonesha unyenyekevu, kuonesha heshima kubwa au kuanguka kifudifudi. Neno la Agano la Kale proskuneo halikadhalika lina maana ya kubusu mkono, au kupiga magoti na kugusa ardhi kwa paji la uso kwa unyenyekevu mkuu. Maneno mengine mawili ya kuabudu yana maana ya kutumika, kufanya ibada Takatifu na kumtolea Mungu Sadaka.

Waache Watu Wangu Waondoke, Ili Wapate Kunitumikia, Dai hili Mungu alilolirudia mara kwa mara lilipelekea Farao kuwaruhusu watu wa Mungu kutoka Misri. Tangu wakati huo, Mungu, Mungu mwenye wivu, amekuwa akipambana na watu wake akiwazuilia kuabudu miungu mingine na sanamu, na badala yake wamwabudu Mungu aliye hai na wa kweli. Kutoka 7:16
Ibada ni kumtukuza Mungu na kumfurahia daima. Mungu anawatafuta watu wa kumwabudu, na kufanya ibada ndiyo wito wetu wa kwanza (Yn4:23 Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. Msitari wa 24 unasema Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.). Ibada ya kweli ni pale tunapomruhusu Roho Mtakatifu atuongoze kutoka katika roho zetu au mioyo yetu kuabudu katika roho na katika kweli na sio tumaini letu ktk miiliau akili zetu Flp 3:3.

Ibada ni tendo la thamani kubwa, ni la kipekee na linamhusu Mungu (utatu mtakatifu) ambao peke yao wanastahili. Lucifer, aliyekuwa mhusika mkuu wa ibada huko mbinguni, alitaka ibada hiyo iwe kwa ajili yake, maana yake aabudiwe yeye badala ya Mungu; na hilo ndilo lililopelekea kuanguka kwake (Isaya 14 na Ezekieli 28). Hata wakati fulani alitaka Yesu amsujudie ili eti ampe falme zote za dunia lakini Bwana alikataa Mt4:8-10.

Kwa hiyo kuabudu ni ibada na tunaposema ibada sio zile taratibu za kibinadamu tulizojipangia katika ibada zetu za siku za leo, ibada za leo tumeweka mambo mengi sana na yanatumia muda mwingi sana kuliko ile maana hasa ambayo mungu aliikusudia katika agano la kale utana ibada zilikuwa zinafaywa kwa mambo makuu 2 neno la Mungu, na Kuabudu.

Kuabudu ni sehemu ya maisha wanadamu tumeumbiwa kuabudu, watuwezi kuishi bila kuabudu hapa haijalishi unaabudu nini!!! Unaweza kuwa unaabudu Mungu wa kweli au miungu kama ambavyo ukisoma bilia utaona kuna miungu mingi inatajwa mfano Baali, Dagon ink na hata leo iko miungu mingi ambayo wanadamu wanaiabudu lakini wa kuabudiwa ni mmoja tu. Na katika biblia tunaona kuaudu kwa mara ya kwanza kulikofanywa na Ibrahimu kutoka katika kitabu cha mwanzo 12: 8 Psalms 34:1 inaonyesha tunatakiwa kumwabudu Mungu kila wakati.

Kwanini tuabudu
kuabudu ni agizo kutoka kwa Mungu kutoka 20 2-4 . Psalm 96:9, Psalm 29:2 Tunapomwabudu mungu naye Mungu hufurahiwa na sisi Zephaniah 3:17 Rom 12:1-2

Your Worship = Your View of God
jinsi unavyoabudu ndiyo mwonekano wa mungu ulivyo ndani yako, haijarishi unaabudu wapi uwe peke yako au mko wengi kama unaabudu kwa kutokumaanisha au kumaanisha itajulikana tu na hivyo ndivyo mtu anaweza kujua ni jinsi gani mtazamo wako kwa Mungu wako.

KUNA NGUVU KATIKA KUSIFU NA KUABUDU
Yoshua 6:20 Matendo 16:23-26 zinaonyesha ambavyo kwa kutumia kusifu tu Mungu alishuka na kufanya lile lililokuwa hitaji lao.

Kusifu kunamfukuza adui
Psalms 50:23. 2 Nyak 20:22. Ukiwa unasifu na kuabudu humfukuza adui mbali kutokana na ukiwa kwenye ibada Mungu hushuka maana yeye anasema anakaa katikati ya sifa hivyo palipo na Mungu shetani hawezi kuwepo lazima akae mbali.akimbie mbali kabisa maana kunakuwepo na uwepo wa bwana wa Majeshi.

Je, ni wakati gani tuabudu?
Ni niyakati zote zinafaa kumwabudu Mungu. Kwa nyakati zilizotengwa Zaburi ya 100 inatuelekeza namna ya kuanza, lakini zaidi ya yote tunapaswa kuishi maisha ya ibada bila kukoma. Kwa kila tunapopumua, kwa kila wazo, kwa neno na tendo, tunapaswa kumwabudu Mungu wetu mzuri tunayemtumikia milele na milele Zab 145:1,2

mwa 12:6- Siku zilipita na watu wakafanyia ibada kwenye Hekalu na kwenye masinagogi; lakini siku hizi miili yetu ni hekalu la Mungu 1Kor 6:19 tu hekalu la Mungu sisi ibada zinatakiwa zifanyike kila wakati na si mara moja kwa wiki kama wengine wanavyo dhani.

Je, Tunafanyaje Ibada?
Biblia inatufahamisha jinsi watu walivyotumia mioyo yao, mawazo yao, mikono yao, viganja vyao, miguu yao, na midomo yao katika uimbaji. Walipaza sauti zao kwa furaha na kusujudu, kucheza, kusifu, kubariki na kushukuru.

Maneno kama halal na haleluya kutoka katika Zaburi yana maana ya kusifu, kumwinua na kumwadhimisha Bwana. Neno Yadah lina maana ya kunyoosha mikono hewani, na neno barak lina maana ya kupiga magoti katika ibada ya kumbariki Mungu. Kuitoa miili yetu katika kumhudumia Mungu na mwanadamu ni ibada pia (Rum 12:1). Watu pia humwabudu Mungu katika sanaa zao, katika uandishi wao, katika michezo ya kuigiza, katika muziki, katika usanifu wa majengo, na hata katika utoaji wa fedha zao kwa ajili ya Injili.

Kusifu na kuabudu sio kuimba tu
Watu wengi wanajua kuwa kusifu na kuabudu ni kuimba tu hapana kuna njia nyingi za kusifu au kuabudu, unaweza kutumia sanaa nyingine kumwabudu mungu au watu wengine wakamwabudu Mungu mf maigizo, ngonjera, shaili, uchoraji, upambaji au unakshi wa vitu, kujenga .nk

Ibada Kanisani
KatIka kanisa makusanyiko yetu yanapaswa kujawa na zaburi, nyimbo, na tenzi za rohoni ambazo zinaweza kuongozwa na Roho katika lugha mpya anazotupatia Yeye. Kwahiyo mikutano mingi ya kisasa haina tofauti sana na burudani za kikristo kama kwenye kumbi za starehe. Watu huwa wanaangalia tu, lakini je, wanaabudu? Uwepo wa Mungu na Roho wake katika ibada zetu utawafanya watu wasioamini kuanguka chini na kuabudu (Kol 3:16) (1Kor 14:15,16,25,26) (Efe 5:19) (Mdo 2:4).

Ibada Ya Kweli Ina Gharama
Biblia inazungumzia habari za sadaka za kusifu. Daudi alicheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote, na akakataa kumtolea Mungu kafara ambayo isingemgharimu cho chote (2Sam 6:14; 24:24). Wale mamajusi wa Mashariki walitoa zawadi za gharama kubwa walipokuja kumwabudu Yesu (Mt 2:9-12), na mwanamke mmoja alimpaka Yesu kwa mafuta ya gharama kubwa, akamwosha miguu yake kwa machozi yake, na kuifuta kwa nywele zake (Lk 7:36-50). Hivyo ibada yoyote inaambatana na kutoa tena vitu vyetu vya thamani.

Tunapaswa kumsifu Mungu kwa jinsi alivyo na kwa matendo yake; lakini Mungu mwenyewe anawatafuta na anawataka wafanya ibada, na si mradi ibada tu. Kusifu kwaweza kufanywa hadharani, lakini ibada mara zote ni jambo la ndani ya moyo. Kusifu mara zote kunaweza kuonekana au kusikika, lakini kuabudu yaweza kuwa ya kimyakimya na iliyofichika. Kusifu kunaonekana, kuna kutumia nguvu, kuna misisimko na furaha; lakini ibada mara zote ni heshima na hofu katika uwepo wa Mungu.
Biblia pekee inatuonesha jinsi Mungu anavyo hitaji na kutamani kuabudiwa na yeye pekee yake ndiyo anayestahili kuabudiwa.

Kusifu na kuabudu kwa siku za leo
Katika siku za leo kuna ufinyu wa mafundisho katika kusifu na kuabudu na ndiyo maana ya kuanda somo hili ili tupanuane mawazo. Watu wengi wa leo wanadhani kusifu ni kuimba kwa nyimbo zenye midundo ya harakaharaka(zouk&sebene) na ukipunguza spidi ndo kuabudu. Hasha tunaposema kusifu inatokana na maneno yaliyopon kwenye wimbo husika kweli ni ya kusifu, kama ni maneno ya kusifu tunasema ni wimbo wa sifa haijarishi speed inayotumika na hali kadhalika nyimbo za kuabudu. Watu katika kipengele hiki huwa wanachakanya nyimbo utakuta wakati wa kusifu anaimba wimbo wa kutia moyo au wa maombi, kinachotakiwa ni kujua kuwa kila jambo lina wakati wake ziiko nyimbo za mazishi, kufariji, kutia moyo, za maombi, za kusifu , na za kuabudu nk sasa usichanganye kwenye kusifu wewe unaimba parapanda italia au tuonane paradiso, hizo sio za sifa sasa najua wewe utafanya zoezi la nyimbo unazozijua ili kufahamu zina ujumbe gani na ziko katika kundi lipi kati ya hayo niliyokufundisha hapo juu.

Baadhi ya maandiko yanayo onyesha aina za kusifu na kuabudu kwa: 

1. Kusimama (Zab 135:1-2, 134:1)

2. Kuinua mikono (Zab 134:2, 28:2)

3. Kuinama au kupiga magoti (Zab 95:6)

4. Kupiga makofi (Zab 7:1)

5. Kucheza (Zab 149:3, 150:4, 2Sam 6:14)

6. Kicheko (Zab 126:2, Ayu 8:20-21)

7. Kufurahi (Kumb 12:11-12, Law 23:40)

8. Kutembea (2Nya 20:21-22)

9. Shangwe (Zab 95:1)

10. Kupiga kelele (Zab 66:1, Law 9:23-24)

11. Kupiga vigelegele (Zab 33:1, 32:11)

12. Ukimya (Mhu 3:7)

13. Kupaza sauti (Isaya 12: 6, Zab 42:4)

14. Kulia/ kutoa machozi katika roho mtakatifu

Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa

Saturday, October 24, 2015

Unaweza Kupata Wapi Amani ya Akili?

Unaweza Kupata Wapi Amani ya Akili?
Kuna tofauti nyingi kati ya wakati wetu na wakati wa Thoreau, aliyetajwa katika makala iliyotangulia. Tofauti moja kubwa ni kwamba leo kuna ushauri kemkemu juu ya kupata amani ya akili. Wanasaikolojia na waandishi wa vitabu vya kujisaidia—hata waandishi wa magazeti—hutoa maoni yao. Huenda ushauri wao ukasaidia kwa muda mfupi; lakini jambo kubwa zaidi linahitajiwa ili kupata masuluhisho ya kudumu. Watu waliotajwa katika makala iliyotangulia walitambua hivyo.
MALEZI na matatizo ya Antônio, Marcos, Gerson, Vania, na Marcelo yalikuwa tofauti. Lakini walikuwa na mambo matatu yanayofanana. Kwanza, kuna wakati ‘walipokuwa hawana tumaini na walikuwa bila Mungu katika ulimwengu.’ (Waefeso 2:12) Pili, walitamani sana amani ya akili. Na tatu, wote walipata amani ya akili waliyotaka baada ya kukubali kujifunza Biblia na Mashahidi wa Yehova. Walipofanya maendeleo, walikuja kutambua kwamba Mungu anawapenda. Kwa kweli, kama Paulo alivyowaambia Waathene wa wakati wake, Mungu “hayuko mbali sana na kila mmoja wetu.” (Matendo 17:27) Kuamini jambo hilo kwa moyo ni muhimu ili kupata amani ya akili.
Kwa Nini Hakuna Amani?
Biblia hutoa sababu mbili za msingi zinazofanya kusiwe na amani ulimwenguni—iwe amani ya akili au amani kati ya watu. Sababu ya kwanza inaelezwa kwenye Yeremia 10:23: “Njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.” Mwanadamu hana hekima wala busara ya kujitawala bila msaada, na msaada pekee ulio na manufaa ya kweli hutoka kwa Mungu. Wanadamu wasiofuata mwongozo wa Mungu hawatapata kamwe amani yenye kudumu. Sababu ya pili inayofanya kusiwe na amani imetajwa na mtume Yohana: “Ulimwengu mzima unakaa katika nguvu ya mwovu.” (1 Yohana 5:19) Bila mwongozo wa Mungu, jitihada za mwanadamu za kupata amani zitazuiwa sikuzote na utendaji wa yule “mwovu,” Shetani, ambaye ni mtu halisi—mwenye nguvu sana—ingawa haonekani.
Kwa sababu hizo mbili—kwamba watu wengi hawatafuti mwongozo wa Mungu na kwamba Shetani ni mwenye utendaji mwingi ulimwenguni—jamii yote ya kibinadamu iko katika hali mbaya sana. Mtume Paulo aliifafanua hali hiyo vema: “Viumbe vyote vinafuliza kupiga kite pamoja na kuwa katika maumivu pamoja hadi sasa.” (Waroma 8:22) Ni nani asiyekubaliana na maoni hayo? Katika nchi tajiri na vilevile nchi maskini, matatizo ya familia, uhalifu, ukosefu wa haki, mahitilafiano ya nyutu, shaka za kiuchumi, chuki za kikabila, uonevu, magonjwa, na kadhalika, hunyima watu amani ya akili.
Mahali pa Kupata Amani ya Akili
Wakati Antônio, Marcos, Gerson, Vania, na Marcelo walipochunguza Neno la Mungu, Biblia, walijifunza mambo yaliyobadili maisha yao. Jambo moja walilojifunza ni kwamba hali ya ulimwengu itabadilika wakati mmoja. Hilo si tumaini tu lenye shaka kwamba mambo yatakuwa mazuri mwishowe. Ni tumaini hakika, lenye msingi mzuri kwamba Mungu ana kusudi fulani kwa wanadamu na kwamba hata sasa tunaweza kunufaika na kusudi hilo tukifanya mapenzi yake. Walitumia maishani mwao yale waliyojifunza katika Biblia, na hali yao ikawa bora. Walipata furaha na amani nyingi zaidi kuliko walivyotazamia.
Antônio sasa hashiriki katika mateto wala mizozo ya wafanyakazi. Anajua kwamba mabadiliko yanayotokana na kufanya hivyo ni machache na ya muda mfupi tu. Kiongozi huyu wa zamani wa wafanyakazi amejifunza juu ya Ufalme wa Mungu. Mamilioni wengi huomba Ufalme huo wanapokariri Sala ya Bwana (au, sala ya Baba Yetu) na kumwambia Mungu hivi: “Ufalme wako uje.” (Mathayo 6:10aZaire Swahili Bible) Antônio alijifunza kwamba Ufalme wa Mungu ni serikali halisi ya mbinguni ambayo itawaletea wanadamu amani ya kweli.
Marcos alijifunza kutumia ushauri wa Biblia wenye hekima kuhusu ndoa. Hivyo, sasa mwanasiasa huyu wa zamani amemrudia mkewe na wana furaha. Yeye pia anatazamia kwa hamu wakati ujao karibuni ambapo Ufalme wa Mungu utaondoa mfumo huu wa ulimwengu wenye pupa na ubinafsi na kuleta ulimwengu bora. Yeye anaelewa vizuri sana ule mstari katika Sala ya Bwana usemao: “Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama mbinguni.” (Mathayo 6:10bZSB) Mapenzi ya Mungu yatakapofanywa duniani, wanadamu wataishi maisha ambayo hawajapata kamwe kuishi.
Namna gani Gerson? Yeye sasa hasafiri bila kusudi wala haibi. Maisha ya Gerson, ambaye zamani alikuwa mtoto mwenye kurandaranda mitaani, sasa yana maana kwa sababu yeye hutumia nguvu zake kuwasaidia wengine wapate amani ya akili. Kama vile mambo hayo yaliyoonwa yaonyeshavyo, kujifunza Biblia na kutumia yale isemayo kunaweza kubadili maisha ya mtu yawe bora.
Amani ya Akili Katika Ulimwengu Wenye Taabu
Yesu Kristo ndiye mhusika mkuu katika kutimizwa kwa mapenzi ya Mungu, na watu hujifunza mengi sana kumhusu wanapojifunza Biblia pamoja na Mashahidi wa Yehova. Usiku alipozaliwa, malaika walimwimbia Mungu sifa: “Utukufu katika mahali pa juu kwa Mungu, na juu ya dunia amani miongoni mwa watu wa nia njema.” (Luka 2:14) Yesu alihangaikia kuboresha maisha ya watu alipokuwa mtu mzima. Alielewa hisia zao na kuwaonyesha huruma ya pekee wenye taabu na wagonjwa. Na, kama maneno ya malaika yaonyeshavyo, Yesu aliwaletea wapole kiasi fulani cha amani ya akili. Mwishoni mwa huduma yake, aliwaambia mitume wake hivi: “Mimi nawaachia nyinyi amani, nawapa amani yangu. Mimi siwapi nyinyi hiyo kwa njia ile ambayo ulimwengu huitoa. Msiache mioyo yenu itaabishwe wala msiiache ikunyatike kwa sababu ya hofu.”—Yohana 14:27.
Yesu hakuwa mfadhili tu. Alijilinganisha na mchungaji, na kuwalinganisha wafuasi wake wenye upole na kondoo aliposema: “Mimi nimekuja ili wapate kuwa na uhai na wapate kuwa nao kwa wingi. Mimi ndiye mchungaji mwema; mchungaji mwema hutoa nafsi yake kwa ajili ya kondoo.” (Yohana 10:10, 11) Naam, tofauti na viongozi wengi leo ambao hujihangaikia kwanza, Yesu alitoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake.
Tunaweza kunufaikaje na yale aliyofanya Yesu? Wengi wanafahamu maneno haya: “Mungu aliupenda ulimwengu sana hivi kwamba akatoa Mwana mzaliwa-pekee wake, ili kila mtu anayedhihirisha imani katika yeye asipate kuangamizwa bali awe na uhai udumuo milele.” (Yohana 3:16) Kudhihirisha imani katika Yesu huhitaji, kwanza kabisa, tumjue yeye na kumjua Baba yake, Yehova. Kumjua Mungu na Yesu Kristo kunaweza kutokeza uhusiano wa karibu pamoja na Yehova Mungu ambao utatusaidia kupata amani ya akili.
Yesu alisema: “Kondoo wangu husikiliza sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata mimi. Nami nawapa hawa uhai udumuo milele, na hawataharibiwa kwa vyovyote, na hakuna atakayewanyakua mkononi mwangu.” (Yohana 10:27, 28) Ni maneno yenye shauku na yenye kufariji kama nini! Ni kweli kwamba Yesu alisema maneno hayo miaka ipatayo elfu mbili iliyopita, lakini yana maana ileile hata sasa. Usisahau kwamba Yesu Kristo bado yu hai na anatenda, anatawala sasa akiwa Mfalme aliyetawazwa wa Ufalme wa mbinguni wa Mungu. Yeye bado anahangaikia wenye upole wanaotamani amani ya akili kama alivyofanya alipokuwa duniani miaka mingi iliyopita. Isitoshe, yeye bado ndiye Mchungaji wa kondoo zake. Tukimfuata, atatusaidia kupata amani ya akili, inayotia ndani matazamio hakika ya kupata amani kamili wakati ujao—amani bila jeuri, vita, na uhalifu.
Manufaa za kweli hutokana na kujua na kuamini kwamba Yehova atatusaidia kupitia Yesu. Je, unamkumbuka Vania, ambaye aliachiwa madaraka makubwa akiwa msichana mdogo na kufikiri kwamba Mungu amemwacha? Sasa Vania anajua kwamba Mungu hakumwacha. Yeye asema: “Nilijifunza kwamba Mungu ni mtu halisi mwenye sifa zenye kupendeza. Upendo wake ulimsukuma amtume Mwana wake duniani ili atupatie uhai. Ni muhimu sana kujua jambo hilo.”
Marcelo asema kwamba uhusiano wake na Mungu ni halisi. Marcelo, ambaye zamani alikuwa mwenda-karamuni, aeleza: “Mara nyingi vijana hawajui wafanye nini, na mwishowe hujiumiza tu. Baadhi yao huanza kutumia dawa za kulevya, kama nilivyofanya. Natumaini kwamba vijana wengi zaidi watabarikiwa kama mimi, kwa kujifunza kweli juu ya Mungu na Mwana wake.”
Kupitia funzo la makini la Biblia, Vania na Marcelo walisitawisha imani yenye nguvu katika Mungu na uhakika katika utayari wake wa kuwasaidia kutatua matatizo. Tukifanya vile walivyofanya—kujifunza Biblia na kutumia yale isemayo—sisi pia tutapata amani nyingi sana ya akili. Kisha kitia-moyo hiki cha mtume Paulo kitatufaa kwelikweli: “Msihangaikie kitu chochote, bali katika kila jambo kwa sala na dua pamoja na utoaji-shukrani acheni maombi yenu ya bidii yajulishwe kwa Mungu; na amani ya Mungu izidiyo fikira yote kwa ubora italinda mioyo yenu na nguvu zenu za akili kwa njia ya Kristo Yesu.”—Wafilipi 4:6, 7.
Kupata Amani ya Kweli Leo
Yesu Kristo anawaelekeza wanaotaka kuijua kweli kwenye njia ya uhai udumuo milele katika paradiso ya kidunia. Anapowaongoza kwenye ibada safi ya Mungu, wanapata amani kama ile inayofafanuliwa katika Biblia: “Watu wangu watakaa katika kao la amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu.” (Isaya 32:18) Na huo ni mwonjo tu wa kimbele wa amani watakayopata wakati ujao. Tunasoma hivi: “Wenye upole watairithi nchi, watajifurahisha kwa wingi wa amani. Wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele.”—Zaburi 37:11, 29.
Hivyo, je, tunaweza kuwa na amani ya akili leo? Ndiyo. Isitoshe, tunaweza kuwa na hakika kwamba karibuni, Mungu atawabariki wanadamu watiifu kwa amani nyingi kuliko wakati mwingineo wowote. Basi, kwa nini usimwombe kupitia sala akupe amani yake? Ikiwa una matatizo yanayokunyima amani, sali kama alivyosali Mfalme Daudi: “Katika shida za moyo wangu unifanyie nafasi, na kunitoa katika dhiki zangu. Utazame teso langu na taabu yangu; unisamehe dhambi zangu zote.” (Zaburi 25:17, 18) Uwe na hakika kwamba Mungu husikiliza sala za aina hiyo. Yeye hunyosha mkono wake na kuwapa amani wale wote wanaoitafuta kwa unyofu wa moyo. Tunahakikishiwa kwa upendo hivi: “BWANA yu karibu na wote wamwitao, wote wamwitao kwa uaminifu. Atawafanyia wamchao matakwa yao, naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.”—Zaburi 145:18, 19.
[Blabu katika ukurasa wa 5]
Mwanadamu hana hekima wala busara ya kujitawala bila msaada, na msaada pekee ulio na manufaa ya kweli hutoka kwa Mungu
[Blabu katika ukurasa wa 6]
Kumjua Mungu na Yesu Kristo kunaweza kutokeza uhusiano wa karibu pamoja na Yehova Mungu ambao utatusaidia kupata amani ya akili
[Picha katika ukurasa wa 7]
Kufuata ushauri wa Biblia husaidia kuwa na maisha ya familia yenye amani

Unaweza Kupata Amani Katika Ulimwengu?

e, Unaweza Kupata Amani Katika Ulimwengu Huu Wenye Misukosuko?
JE, UNAISHI kwa amani? Kwa watu wengi, jibu lililo wazi ni hapana. Wanaishi katika maeneo yenye vita, misukosuko ya kisiasa, jeuri ya kikabila, au ugaidi. Hata ikiwa hupatwi na misiba hiyo, amani yako inaweza kuvurugwa na uhalifu, mateso, na ugomvi kutoka kwa wafanyabiashara wenzako au majirani. Pia, katika familia nyingi mara nyingi watu wanapigana badala ya kuwa na amani.
Watu wengi wanatamani sana kuwa na amani ya moyoni. Huenda wakatafuta amani hiyo katika dini, madarasa yanayowafundisha watu kutafakari, au vikundi vya mazoezi ya yoga. Wengine wanatumaini kupata amani kwa kuchukua likizo, kupanda milima, kusafiri katika maeneo ya nyika au jangwa, au kutembelea maeneo ambayo yana chemchemi za maji moto. Hata ingawa inaonekana kwamba watu fulani wanaotafuta amani ya moyoni wanapata amani ya kadiri fulani, huenda wakatambua haraka kwamba amani kama hiyo ni ya juujuu tu na ya muda mfupi.
Hivyo basi, unaweza kupata wapi amani ya kweli? Muumba wetu, Yehova Mungu ndiye chanzo cha amani. Kwa nini? Yeye ni “Mungu anayetoa amani.” (Waroma 15:33) Chini ya utawala wa Ufalme wake ambao unakaribia, kutakuwa na “wingi wa amani.” (Zaburi 72:7; Mathayo 6:9, 10) Hiyo ni amani bora zaidi kuliko amani yoyote ile inayopatikana kutokana na mapatano ya wanadamu. Mara nyingi, mapatano hayo yanakomesha uadui kwa muda mfupi tu. Lakini amani ya Mungu itaondoa mambo yote yanayosababisha vita na ugomvi. Kwa kweli, hakuna mtu atakayejifunza vita tena. (Zaburi 46:8, 9) Mwishowe, sote tutafurahia amani ya kweli!
Ingawa tumaini hilo ni zuri ajabu, huenda ukatamani kupata amani ya kadiri hata sasa. Je, kuna njia ya kupata amani ya moyoni ambayo inaweza kukusaidia katika nyakati hizi zenye misukosuko? Inapendeza kujua kwamba Biblia inatuonyesha jinsi ya kupata amani hiyo. Chunguza miongozo fulani katika sura ya 4 ya barua ya mtume Paulo kwa Wafilipi. Tunakuomba usome mstari wa 4 mpaka wa 13 katika Biblia yako mwenyewe.
“Amani ya Mungu”
Tunasoma hivi kwenye mstari wa 7: “Amani ya Mungu yenye ubora unaozidi fikira zote itailinda mioyo yenu na nguvu zenu za akili kwa njia ya Kristo Yesu.” Amani hiyo haiji kwa kutafakari tu au kwa kujaribu kuboresha utu wetu. Badala yake, ni amani inayotoka kwa Mungu. Amani hiyo ni yenye nguvu sana hivi kwamba ‘ina ubora unaozidi fikira zote.’ Bila shaka, inazidi mahangaiko yetu yote, ujuzi, na fikira zetu. Huenda tukahisi kwamba hatuwezi kushinda matatizo yetu, lakini amani ya Mungu inaweza kutujaza tumaini linalotegemea Biblia la kwamba siku moja matatizo yetu yote yatakwisha.
Je, ni jambo lisilowezekana? Kwa wanadamu haliwezekani; lakini “mambo yote yanawezekana kwa Mungu.” (Marko 10:27) Imani na kumtegemea Mungu kunatusaidia kutohangaika kupita kiasi. Mfikirie mtoto mdogo ambaye amepotea ndani ya duka kubwa. Anajua kwa hakika kwamba kile anachohitaji kufanya tu ni kumpata Mama yake na mambo yote yatakuwa shwari tena. Kama mtoto huyo anavyobebwa anapopatikana, tunaweza pia kuwa na hakika kwamba Mungu atatubeba mikononi mwake kwa njia ya mfano. Atatutuliza na mwishowe ataondoa kabisa mahangaiko yetu yote.
Waabudu wengi wa Yehova wamepata amani ya Mungu wakati wa majaribu makali zaidi. Kwa mfano, fikiria kisa cha Nadine, ambaye alizaa mtoto aliyekufa. Anaeleza: “Ninaliona kuwa jambo gumu kuzungumza kuhusu hisia zangu, na sikuzote ninajaribu kujifanya ili ionekane kwamba hali hiyo hainisumbui. Lakini kwa ndani, nilikuwa nimevunjika moyo. Karibu kila siku, nilimwaga moyo wangu kwa Yehova katika sala na kumsihi anisaidie. Nimehisi nguvu za sala, kwa kuwa wakati wowote niliposhuka moyo na kujiambia hivi: ‘Siwezi kuvumilia tena,’ nilipata utulivu na amani ya moyoni. Nilijihisi nikiwa salama salimini.”
Inalinda Moyo na Akili Yako
Na turudi tena kwenye andiko la Wafilipi 4:7. Linasema kwamba amani ya Mungu italinda mioyo na nguvu zetu za akili. Kama vile tu askari anavyolinda kituo chake, amani ya Mungu inalinda moyo wetu, ili mawazo ya kujirundikia vitu vya kimwili, mahangaiko yasiyo ya lazima, na maadili mapotovu yasiingie katika akili na moyo wetu. Fikiria mfano mmoja.
Watu wengi katika ulimwengu huu wenye misukosuko wanaamini kwamba ili wawe wenye furaha na salama, wanahitaji kuwa na pesa au mali nyingi. Kwa kufuata mashauri ya wataalamu, huenda wakanunua hisa ili wahifadhi kiasi fulani cha pesa zao. Je, kweli wanajihisi wakiwa na amani? Si lazima. Huenda wakachunguza hali kila siku wakiwa na wasiwasi kuhusu thamani ya hisa zao, huku wakijiuliza ikiwa wauze, wanunue, au wabaki na hisa hizo. Huenda pia wakawa na wasiwasi bei ya hisa inaposhuka. Bila shaka, Biblia haimkatazi mtu kuwekeza katika biashara, lakini inatoa shauri hili zuri: “Anayependa fedha hatatosheka na fedha, wala anayependa mali hatatosheka na mapato. Hilo pia ni ubatili. Usingizi wa mtumishi ni mtamu, bila kujali kama anakula kidogo au kingi; lakini wingi alio nao tajiri haumruhusu kulala.”—Mhubiri 5:10, 12.
Andiko la Wafilipi 4:7 linamalizia kwa kusema kwamba amani ya Mungu inalinda mioyo yetu na nguvu za akili “kwa njia ya Kristo Yesu.” Kuna uhusiano gani kati ya Kristo Yesu na amani ya Mungu? Yesu anatimiza sehemu ya maana sana katika kutimizwa kwa kusudi la Mungu. Yesu alitoa uhai wake ili tuweze kukombolewa kutoka katika utumwa wa dhambi na kifo. (Yohana 3:16) Pia, yeye ndiye aliyewekwa kuwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu. Hivyo, kujua daraka ambalo Yesu anatimiza kunaweza kuchangia sana amani yetu ya akili na moyo. Jinsi gani?
Tukitubu kikweli dhambi zetu na kuomba msamaha kwa msingi wa dhabihu ya Yesu, Mungu atatusamehe, na hilo litatusaidia kuwa na amani ya akili na moyo. (Matendo 3:19) Tunapotambua kwamba hatuwezi kufurahia maisha kikamili mpaka Ufalme wa Kristo utakapokuja, tunaepuka kuishi bila kujali kana kwamba hatuna tumaini la kuishi wakati ujao. (1 Timotheo 6:19) Bila shaka, sisi pia tunapatwa na matatizo, lakini tunaweza kufarijiwa na tumaini hakika la kwamba hivi karibuni tutakuwa na maisha bora zaidi.
Jinsi Unavyoweza Kupata Amani ya Mungu
Hivyo basi, unaweza kupata jinsi gani amani ya Mungu? Tunapata madokezo fulani kwenye Wafilipi 4:4, 5, tunaposoma hivi: “Shangilieni sikuzote katika Bwana. Mara nyingine tena nitasema, Shangilieni! Usawaziko wenu na ujulikane kwa watu wote. Bwana yuko karibu.” Paulo alipoandika maneno hayo, alikuwa amefungwa gerezani isivyo haki huko Roma. (Wafilipi 1:13) Badala ya kulalamika kwa sababu ya kutendewa isivyo haki, aliwatia moyo waamini wenzake washangilie sikuzote katika Bwana. Ni wazi kwamba shangwe yake haikutegemea hali zake, bali ilitegemea uhusiano wake pamoja na Mungu. Sisi pia tunahitaji kujifunza kufurahia kumtumikia Mungu hata hali zetu ziwe namna gani. Kadiri tunavyomjua Yehova vizuri zaidi na kufanya mapenzi yake kikamili, ndivyo tutakavyofurahia kumtumikia. Kufanya hivyo, kutatuletea uradhi na amani ya moyoni.
Zaidi ya hayo, tunatiwa moyo kuwa wenye usawaziko. Tukisitawisha sifa ya usawaziko, hatutatazamia kutimiza mambo mengi zaidi ya uwezo wetu. Tunajua kwamba sisi si wakamilifu; hatuwezi kuwa bora kabisa katika kila jambo. Kwa hiyo, kwa nini tujisumbue tukifikiria jinsi ya kuwa wakamilifu au, angalau, kuwa bora kuliko watu wengine wote? Pia, hatutatazamia wengine wawe wakamilifu. Hivyo, wengine wanapofanya jambo ambalo linatukasirisha tunaweza kubaki watulivu. Tafsiri nyingine ya neno la awali la Kigiriki linalotafsiriwa “usawaziko” ni “kukubaliana na-.” Ikiwa tuko tayari kukubaliana na mtu fulani katika mapendezi ya kibinafsi, tutaepuka ugomvi, ambao mara nyingi hauna faida yoyote bali unaharibu kwa muda amani pamoja na wengine na pia amani yetu ya moyoni.
Maneno yafuatayo kwenye Wafilipi 4:5, “Bwana yuko karibu,” huenda yakaonekana hayapatani na mistari mingine. Hivi karibuni Mungu atabadili ulimwengu huu wa kale na kuleta ulimwengu mpya chini ya Ufalme wake. Lakini hata sasa anaweza kuwa karibu na kila mtu anayemkaribia. (Matendo 17:27; Yakobo 4:8) Kutambua kwamba Bwana yuko karibu kunatusaidia kushangilia, kuwa wenye usawaziko, na kutokuwa na mahangaiko kuhusu matatizo ya leo au ya wakati ujao, kama mstari wa 6 unavyoonyesha.
Tunapochunguza mstari wa 6 na wa 7, tunatambua kwamba amani ya Mungu inahusiana moja kwa moja na sala. Watu fulani wanaona sala kuwa tu aina fulani ya kutafakari, wakifikiri kwamba kila aina ya sala inaweza kuongeza utulivu wao wa moyoni. Hata hivyo, Biblia inasema kuhusu mawasiliano ya unyoofu pamoja na Yehova, yaani, mawasiliano ya karibu kama ya mtoto anayemweleza mzazi mwenye upendo shangwe na wasiwasi wake. Inatia moyo kama nini kujua kwamba tunaweza kumkaribia Mungu “katika mambo yote.” Hata iwe tuna mawazo gani ndani kabisa ya akili au mioyo yetu, tunaweza kuyafunua kwa Baba yetu wa mbinguni.
Mstari wa 8 unatutia moyo tukazie akili mawazo mazuri. Hata hivyo, haitoshi tu kufikiria mambo mazuri. Kama mstari wa 9 unavyoeleza, tunapaswa pia kufuata mashauri mazuri ya Biblia. Kufanya hivyo kutatuwezesha kuwa na dhamiri safi. Methali hii ni ya kweli kabisa: Dhamiri nzuri ni mto laini wa kulalia!
Ndiyo, unaweza kupata amani ya moyoni. Inatoka kwa Yehova Mungu, ambaye anawapa wale wanaomkaribia na wanaotaka kufuata mwongozo wake. Ukichunguza Neno lake, Biblia, unaweza kujua vizuri mawazo yake. Hata hivyo, si jambo rahisi kufuata miongozo yake. Lakini jitihada hizo zote si za bure kwa sababu ‘Mungu wa amani atakuwa pamoja nawe.’—Wafilipi 4:9.
[Blabu katika ukurasa wa 10]
“Amani ya Mungu . . . itailinda mioyo yenu.”—WAFILIPI 4:7

Friday, October 9, 2015

YESU akasema ‘Kaeni Katika Neno Langu’

‘Kaeni Katika Neno Langu’
“Mkikaa katika neno langu, ninyi kwa kweli ni wanafunzi wangu, nanyi mtaijua kweli, nayo kweli itawaweka ninyi huru.”—YOHANA 8:31, 32.
Inamaanisha Nini? “Neno” la Yesu linamaanisha mafundisho yake, ambayo chanzo chake ni cha juu zaidi. Yesu alisema: “Baba mwenyeYohana 12:49) Alipokuwa akisali kwa Baba yake wa mbinguni, Yehova Mungu, Yesu alisema: “Neno lako ni kweli.” Alinukuu Neno la Mungu mara nyingi ili kuunga mkono mafundisho yake. (Yohana 17:17; Mathayo 4:4, 7,10) Kwa hiyo, Wakristo wa kweli, ‘wanakaa katika neno lake,’ yaani, wanakubali Neno la Mungu Biblia, kuwa “kweli” na msingi pekee wa imani na matendo yao.
we aliyenituma amenipa amri kuhusu jambo la kutangaza na la kusema.” (
Wakristo wa Mapema Walifanyaje Hivyo? Mtume Paulo, ambaye ndiye Mkristo aliyeandika vitabu vingi zaidi katika Biblia, aliliheshimu Neno la Mungu kama Yesu alivyofanya. Aliandika hivi: “Andiko lote limeongozwa na roho ya Mungu nalo ni lenye faida.” (2 Timotheo 3:16) Wanaume waliowekwa rasmi ili kuwafundisha Wakristo wenzao walipaswa “kushikamana na Neno la Mungu lililo hakika na lenye kutegemeka.” (Tito 1:7, 9The Amplified Bible) Wakristo wa mapema walihimizwa wakatae “falsafa na udanganyifu mtupu kulingana na pokeo la wanadamu, kulingana na mambo ya msingi ya ulimwengu na si kulingana na Kristo.”—Wakolosai 2:8.
Ni Nani Wanaofanya Hivyo Leo? Katiba ya Vatikani inayoitwa Dogmatic Constitution on Divine Revelation, iliyoanza kutumika mwaka wa 1965 na ambayo imenukuliwa katika kitabu kimoja cha kanisa Katoliki (Catechism of the Catholic Church) inasema hivi: “Kanisa [Katoliki] halifuati tu Maandiko Matakatifu katika kuhakikisha mambo yote yaliyofunuliwa. Kwa hiyo, mapokeo matakatifu na pia Maandiko Matakatifu yanapaswa kukubaliwa na kuheshimiwa kwa ushikamanifu uleule.” Makala moja katika gazeti laMaclean’s ilinukuu kasisi mmoja huko Toronto, Kanada, ambaye aliuliza: “Kwa nini tunahitaji kuongozwa na sauti ya ‘kimapinduzi’ ya miaka elfu mbili iliyopita? Tuna maoni mazuri ajabu, ambayo uzito wake hupungua nyakati zote kwa sababu tunalazimika kuyaunga mkono kwa kutumia Maandiko na maneno ya Yesu.”
Kitabu New Catholic Encyclopedia kinasema hivi kuhusu Mashahidi wa Yehova: “Wanaiona Biblia kuwa chanzo pekee cha imani na sheria zinazoongoza mwenendo wao.” Hivi karibuni, mwanamume fulani huko Kanada alimkatiza mwanamke fulani Shahidi wa Yehova alipokuwa akijitambulisha. “Ninajua wewe ni nani,” akasema mwanamume huyo huku akiinyooshea kidole Biblia ya Shahidi huyo, “kwa sababu una kitambulisho.”

Saturday, October 3, 2015

UTAINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI ISAYA 58:12


NAMNA YA KUSIKIA NA KUIELEWA SAUTI YA MUNGU ILI IKUSAIDE KATIKA KUFANYA MAAMUZI (Sehemu ya tatu)

August 20, 2015
4Na: Patrick Sanga
Mada – Njia anazotumia Mungu kusema na mwanadamu (Sehemu ya kwanza)
Katika sehemu ya kwanza na ya pili ya ujumbe huu naliandika mambo muhimu ya kujua kwanza kuhusu sauti ya Mungu. Ili kusoma sehemu hiyo bonyeza link hii https://sanga.wordpress.com/2015/04/08/namna-ya-kusikia-na-kuielewa-sauti-ya-mungu-ili-ikusaidie-katika-kufanya-maamuzi-sehemu-ya-2/ Katika sehemu hii ya tatu na ya kwanza kwa mada hii nitaendelea na somo hili kwa kuanza kunagalia njia ambazo Mungu hutumia kusema na wanadamu, naam sasa fuatana nami tuendelee;
Katika Yohana 5:30 imeandikwa ‘Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama NISIKIAVYO ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka’. Andiko hili linatuonyesha utaratibu au nidhamu aliyokuwa nayo Yesu katika kutekeleza kusudi la kuletwa kwake hapa duniani.
Yesu anatueleza wazi kwamba katika utumishi wake, hakutafuta kutekeleza mapenzi yake, bali kadri ALIVYOSIKIA kutoka kwa baba yake ndivyo alivyotenda. Ushuhuda huu wa Yesu unatufanya tujue kwamba, kumbesauti ya Mungu ina umuhimu wa kipekee katika kutusaidia kufanya maamuzi mbalimbali yanayotukabili kila siku.
Sauti ya Mungu ni nini? – sauti ya Mungu si tu maneno yanayotoka kwenye kinywa chake kama wengi wanavyofahamu bali ni UJUMBE ambao Mungu analeta kwenye maisha yako kwa NJIA mbalimbali ili kukuondoa kwenye matakwa/makusudi yako na hivyo kukusaidia kuyatenda mapenzi yake makamilifu.
Zifuatazo ni baadhi ya njia muhimu ambazo Mungu hutumia katika kusema, kufikisha ujumbe au kufanya mawasiliano na mwanadamu;
  • Kupitia neno lake
Neno la Mungu ndio msingi mkuu wa Mungu kusema na mwanadamu. Hata njia nyingine ambazo Mungu atatumia kusema na wanadamu ni dhahiri kwamba ujumbe wake lazima uendane na neno lake na si vinginevyo.
Katika 2Timotheo 3:16-17 imeandikwa ‘Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema’.
1
Neno la Mungu ndiyo sauti kuu ya Mungu duniani kwa wanadamu na hivyo kuwa na ufahamu wa kutosha wa neno la Mungu ni lazima kwa mwamini anayetaka kuisikia sauti ya Mungu iliyoko ndani ya neno lake. Kadri mwamini anavyokuwa na neno la kutosha ndani yake, ndivyo anavyojiweka kwenye mazingira sahihi ya kusikia na kuelewa sauti ya Mungu kwenye kila eneo la maisha yako na hivyo kuwa kwenye nafasi bora ya kufanya maamuzi.
  • Kupitia ndoto
Katika Hesabu 12:6 imeandikwa ‘Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, NITASEMA NAYE KATIKA NDOTO’. Ndiyo, Mungu husema kupitia ndoto, kwa kuwa ndoto ni lugha ya picha tena rahisi ya mawasiliano kwa yeye kufikisha ujumbe wake na hivyo kumsaidia mtu aelewe mpango wake (Mungu) kwenye maisha yake na hivyo kufanya maamuzi muafaka.
Pia katika Ayubu 33:14 imeandikwa ‘Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani’. Hapa Biblia inatueleza kwamba kumbe ndani ya ndoto kuna sauti na hivyo mtu anaweza kuisikia sauti ya Mungu kupitia ndoto, ingawa si ndoto zote huambatana na sauti. Ndoto huja pale mtu anapokuwa amelala usingizi na hili lina maana, mtu anahitaji muda na mazingira bora ya kulala ili Mungu aweze kusema naye kwa njia hii. Ndoto inaweza kuja kwa mfano wa hadithi au tukio lenye kisa au uzoefu fulani ndani yake.
2
Endapo, katika ndoto ambayo ni ya kutoka kwa Mungu, ukiona unaongea, maana yake Mungu anakuonyesha nini cha kusema, kufanya au kuomba punde utakapoamka. Kuomba baada ya kuamka au kushtuka ni LAZIMA ili kuhakikisha zile za kutoka kwa Mungu zinatimia na zile za kutoka kwa Shetani zinazuiliwa.Jambo la msingi ni lazima mtu ajifunze kutafsiri ndoto anayoiota kama sauti ya Mungu kwa kuwa ndani ya ndoto kuna ujumbe. Kuwa na ufahamu wa kutosha wa neno la Mungu ndio msingi muhimu wa kuelewa na kufasiri ndoto unazoota. Rejea mifano ifuatayo ndani ya Biblia ili kuelewa zaidi njia hii.
Mungu anasema na Abramu kuhusu uzao wake (Mwanzo 15:12), Mungu anasema na Sulemani juu ya mambo mbalimbali (1Wafalme 3:5-13), Mungu anamonya Abimeleki kuhusu mke wa Abramu (Mwanzo 20:1-7), Mungu anamuonya Yusufu, asimwache Mariam (Matahyo 1:20), Mungu anasema na Yusufu kuhusu ulinzi wa Yesu dhidi ya hila za Herode (Mathayo 2:13).
  • Kupitia watumishi wa Mungu au viongozi wa kiroho   
Katika kuzungumza na wanadamu, Mungu amejiwekea pia utaratibu wa kutumia watumishi wake mbalimbali ikiwa ni pamoja wachungaji, manabii, walimu, manabii na mitume au kwa lugha ya ujumla viongozi wa kiroho. Mungu anatumia watu hawa kwa sababu (a) utaratibu aliojiwekea kama nilivyosema awali (b) kutokana na nafasi zao katika mwili wa Kristo na (c) watu wengi hawako tayari kulipa gharama ya kutafuta kuisikia na kuelewa sauti ya Mungu.
3
Watumishi wamewekwa maalum na Mungu kwa ajili yetu ili watusaidie kuelewa mapezi yake kwenye maisha yetu na hivyo kufanya maamuzi sahihi kwa kila hatua. Katika Luka 16:29 imeandikwa ‘wanao Musa na manabii wawasikilize wao’. Naam kwa lugha nyingine Musa na manabii (watumishi) ndiyo sauti ya Mungu kwao.
Hata hivyo ni lazima watu wawe na tahadhari kwamba watumishi wanaolengwa hapa ni wale walioitwa na Mungu kweli, yaani watumishi wa kweli (nuru) na si wa uongo (giza). Tafadhali rejea maandiko yafutayo kwa ufahamu zaidi (1Samweli 2:27, 1Samweli 9:9).
Mungu akubariki kwa kufuatilia mfululizo huu. Katika sehemu ya nne, nitaendelea kuandika njia nyingine ambazo Mungu hutumia kusema na wanadamu. Somo litaendelea….
Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA wangu.


ROHO YA HEKIMA NA UFUNUO

May 2, 2015
1Na: Patrick Sanga
Salaam katika jina lake BWANA Yesu
Katika Waefeso 1:17 Biblia inasema ‘Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi ROHO YA HEKIMA NA YA UFUNUO KATIKA KUMJUA YEYE’. Hili moja ya maombi muhimu ambayo Mtume Paulo alifanya kwa jili ya Kanisa la Efeso. Kila nisomapo mstari huu nimekuwa nikijuliza sana ni kwa nini Mtume Paulo aliomba maombi haya kwa kanisa hili?.
Katika kutafakari na kuendelea kujifunza niligundua kwamba kulikuwa na sababu kubwa tatu ambazo zilimpelekea Mtume Paulo kuwaombea jambo hili, na kutokana na umuhimu wake hata kwa kanisa la sasa ndiyo maana nimeona ni vema nikaliandika hapa ili na wewe msomaji uweze kujifunza.
Zifuatazo ni sababu kadhaa zilizompelekea Mtume Paulo aliombee kanisa la Efeso roho ya hekima na ufunuo na kwa sababu hiyo zinatusaidia kujua umuhimu wake kwa kanisa la sasa pia;
Ili waweze kumjua Mungu zaidi (Waefeso 1:17)
Waefeso 1:11 ‘Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake’.
4
Kazi ya roho ya ufunuo ni kumfunua Mungu kwa kiwango ambacho bado hujakiona wala kukizoea ili kuboresha uhusiano wako na Mungu na kukufanya umaanishe katika kumpenda. Ndiyo, lengo ni kumfunua Mungu kwako, kutoka kwenye kona tofauti tofauti ili umjue zaidi ili hali kazi ya roho ya hekima ni kukupa ufahamu (maarifa), werevu na busara katika kufanya maamuzi sahihi kuhusu uhusiano wako na Mungu na maisha yako kwa ujumla. Katika ufunuo kuna mambo ambayo Mungu atayaleta kwako na yanahitaji hekima katika kuyafasiri, kuyanena na kutenda.
Naam bado hatumjui Mungu kwa kiwango kitupasacho kumjua na ndio maana tunahitaji roho ya ufunuo. Roho ya ufunuo inamuongoza mtu kujenga mahusaino binafsi na Mungu wake tokana na ufunuo aliopata.  Roho hii inatuleta kwenye ufahamu muhimu kuhusu ulimwengu wa roho na kwamba ni lazima tuanze kuishi maisha katika ulimwengu wa roho kuliko vile tunavyoishi katika ulimwengu wa mwili ili kumjua Mungu zaidi.
Ili kujua mambo ambayo Mungu amewaandalia (1Wakorinto 2:9-10)
Katika fungu hilo Biblia inasema hivi ‘Lakini, kama ilivyoandikwa, MAMBO AMBAYO JICHO HALIKUYAONA WALA SIKIO HALIKUYASIKIA, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. LAKINI MUNGU AMETUFUNULIA SISI KWA ROHO. Maana Roho huchunguza yote, hata MAFUMBO ya Mungu’. Pia katika Waefeso 1:18 imeandikwa ‘MACHO YA MIOYO YENU YATIWE NURU MJUE tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo’
5
Mungu anataka watu wake wajue kwamba yeye anayo mawazo (Yeremia 29:11), mbalimbali ambayo amewaandalia watoto wake. Mawazo hayo yameunganishwa na kusudi la kuwepo kwao hapa duniani na hawana budi kuyajua, kuyapata na kuyatenda. Naam ili wafikie hapo sharti juu yao na ndani yao, wawe na roho ya hekima na ufunuo.
Kumbuka katika kila nyanja ya maisha iwe kazi, uchumi, biashara, familia, huduma, ndoa nk, yapo mambo ambayo ameyaandaa na anataka uyajue. Naam ni jukumu lako kuendelea kujenga na kuboresha mahusaino yako na Roho Mtakatifu yawe mazuri daima.
Ili kuujenga mwili wa Kristo ipasavyo
Katika 1Wakorinto 12:7 Biblia inasema ‘Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana’.  Ukiendelea Katika 1Wakorinto 12:20 imeandikwa ‘Na jicho haliwezi kuuambia mkono, sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuaimbia miguu; sina haja na ninyi’ na ule mstari wa 25 unasema ‘Ili kusiwe na faraka katika mwili, BALI VIUNGO VITUNZANE KILA KIUNGO NA MWENZIWE(1Wakorinto 12:25).
Hivyo roho ya ufunuo inatoa ufunuo ili kufaidiana, lengo ikiwa ni kuusaidia mwili wa Kristo kuimarika zaidi. Naam kumbuka ufunuo huu ni kwa sehemu kwa lengo la kulijenga kanisa, mwili wa Kristo. Katika 1Wakorinto 12:11 imeandikwa ‘Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye’. Na tena Mtume Paulo anamalizia kwa kusema ‘Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake’ (1Wakorinto 12:27).
Naam hakuna mtu anayepewa karama zote, kila mmoja anapewa kwa SEHEMU kama KIUNGO ili kwa kushirikiana, MWILI wa Kristo ujengwe vema. Naam kila kiuingo lazima kihakikishe kina kuwa na ufanisi unaotakiwa, si kwa ajii yake, bali kuhakikisha mwili wa Kristo unajengwa ipasavyo, kupitia ufunuo/uwepo wa kile kiungo.
Kanisa lazima lifike mahali pa kuwa na uelewa kamili juu ya mwili wa Kristo unavyopaswa kutenda kazi kupitia ufunuo wa Roho Mtakatifu kwa kuwa ‘Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka (1Wakorinto 12:18). Naam kila mshirika unayemuona NI KIUNGO CHA MWILI WA KRISTO KUPITA KARAMA, VIPAWA NA HUDUMA ALIZOPEWA kwa lengo la kuujenga mwili wa Kristo.  Roho ya hekima ikuongoze kutenda na kujua kwamba karama, huduma na vipawa ulivyonavyo ni kwa ajili ya kuujenga mwili wa kristo.
Naam hatupaswi kumdharau mtu yoyote kutokana na hali yake ya nje kwa jinsi ya kibinadamu maana yeye ni kiungo kinachostahili heshima zaidi (1 Wakorinto 12:22) Kazi ya Mchungaji na viongozi wa kanisa ni kufuatilia ili kujua Mungu ameweka/ametoa/amefunua kitu gani (karama/vipawa/huduma) juu ya wale wanaowaongoza ili kuviendeleza kwa lengo la kuujenga mwili wa Kristo.
3
Hivyo tokana na umuhimu wa roho ya hekima na ufunuo juu ya kanisa la Mungu na kwa mtu mmoja mmoja ni vizuri tukachukua au ukachukua hatua ya kuanza kumomba Mungu akujalie roho ya hekima na ufunuo wewe binafsi, familia yako, jamaa zako na kanisa kwa ujumla ili manufaa yake yawe dhahiri katika mwili wa Kristo ulimwenguni kote.
Roho ya hekima na ufunuo na iwe nanyi
Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA!

MAMBO YA KUMSAIDIA KIJANA ALIYEOKOKA AISHI MAISHA YENYE USHUHUDA MZURI

April 16, 2015
AuthorsNa: Patrick S. Sanga

Mtume Paulo katika waraka wake kwa Timotheo anamwambia hivi, ‘Mtu awaye yote ASIUDHARAU ujana wako, bali uwe KIELELEZO kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.JITUNZE nafsi yako, na mafundisho yako. DUMU katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo UTAJIOKOA NAFSI YAKO NA WALE WAKUSIKIAO PIA’ (1Timotheo 4:12 & 14).
Sentensi hizi zinatuonyesha kwamba kijana yeyote ambaye amefanya uamuzi wa kuokoka, kwa hakika amefanya maamuzi ambayo yanamtaka amaanishe katika kumfuata kwake Yesu au kuuishi wakovu wake. Pamoja na kumpa Yesu maisha yake ni lazima kijana afanye maamuzi ya kuishi maisha ya kudumu kumpendeza Mungu kwa kuzikubali gharama zinazohusiana na wokovu aliouchagua na si kuishi maisha yenye kupelekea jina la BWANA kutukanwa kama ilivyo kwa baadhi ya vijana wengi leo.
Ukisoma mstari huu wa 1Timotheo 4:14 kwenye toleo la kiingereza la ESV unasema ‘Keep a close watch on yourself and on the teaching. Persist in this, for by so doing you will save both yourself and your hearers’.Kwa mujibu wa dictionary ya kigiriki na kiebrania neno ‘save’ lina maana ya kuweka huru (deliver), kulinda (protect), kuponya (heal), kutunza (preserve), kuokoa (save). Jambo muhimu ambalo Mtume Paulo alikuwa akilisisitiza hapa ni hili; jambo muhimu si tu kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wako, bali kila mwamini ana kazi kubwa ya kufanya iliKUULINDA NA KUUTUNZA WOKOVU WAKE.
Moja ya changamoto kubwa sana ambazo zinawakabili vijana wengi waliokoka leo ni kuipenda dunia. Kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana wengi na kwa sababu ya kuipenda dunia; (a) Mahusiano ya vijana wengi na Mungu wao yameharibika (b) Maisha ya vijana wengi yamekosa uelekeo (c) Kutokana na uovu wao jina la Bwana Yesu limekuwa likitukanwa.
4
Katika kile kitabu cha 1Yohana 2:16 ni dhahiri kwamba dunia imejaaTAMAA YA MWILI, TAMAA YA MACHO NA KISHA KIBURI CHA UZIMA. Tamaa ina nguvu ya kuvuta pamoja na kudanganya, naam inamuingiza mtu kwenye jaribu. Hii ina maana tamaa ni mlango, naam mlango huu unapaswa kufungwa mapema usikupoteze. Hebu tujifunze kutokana na anguko la mfalme Daudi na mke wa Bathssheba (Samweli 11:1-2). Tunaona anguko la Daudi lilisaabishwa na kumpa Ibilisi nafasi kwa kutokwenda vitani. Mkristo akipoa katika kuvipiga vita vya kiroho inakuwa rahisi kwake kuanguka dhambini             (Yakobo 1:14-15), naamkumbuka kwamba siku zote tamaa inalenga kumfurahisha mtu binafsi (self-pleasing) bila kujali matokeo yake.
Hivyo katika nyakati tulizonazo sasa suala la kuipenda dunia ni lazima litafutiwe ufumbuzi wa kudumu miongoni mwa vijana wetu. Ujumbe huu mfupi unalenga kueleza kwa namna gani kuipenda dunia kumekuwa tanzi kwa vijana na nini vijana wafanye ili kuikabili na kuishinda changamoto husika.
Pia katika waraka 2Timotheo 2:15 Mtume Paulo anaendelea kumwambia kijana Timotheo ‘Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu,mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli’.
Pengine kila mmoja wetu atafakari maisha yake kwa kuhusianisha na maelekezo ya Paulo kwa Timotheo. Naomba jiulize na kujijibu kwa uaminifu kwamba mosi, je, ujana wako wako unaheshimika au unadharauliwa? Pili, je, kwa waamini wenzako umekuwa kielelezo cha kweli kwa habari ya imani, upendo, usafi, usemi na mwenendo au la?
DSCF0028
Binafsi  nimekuwa nikijiuliza ni kwa namna gani kijana atahakikisha kwamba(a) Ujana wake haudharauliwi (b) Anakuwa kielelezo kwa waamini wenzake (c) Anathibitisha kwamba kweli amekubaliwa na Mungu. Naam katika kusoma na kutafakari neno la Mungu nimejifunza kwamba zifuatazo ni njia ambazo zitatusaidia sisi vijana wa leo kuifikia kweli hii ya neno la Mungu.
  • Kijana adumu katika kuomba na kusoma (kutafakari + kulitenda) neno la Mungu
Katika Zaburi 119:9 & 11 Biblia inasema ‘Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii AKILIFUATA neno lako’. Pia kwenye ule mstari wa 11 inasema ‘moyoni mwangu nimeliweka neno lako, NISIJE NIKAKUTENDA DHAMBI’.
Naam katika Mathayo 26:41 imeandikwa ‘Kesheni, mwombe, MSIJEmkaingia majaribuni; roho I radhi, lakini mwili ni dhaifu’. Yohana 17:17 inasema ‘uwatakase kwa ile kweli ;neno lako ndiyo kweli. Mambo haya mawili yanapaswa kwenda kwa pamoja nakijana akidumu katika kuomba na kusoma neno la Mungu ushindi ni lazima.
  • Kijana asimpe Ibilisi nafasi.
Kijana anapaswa kujiuepusha na mazingira yenye kumfanya aiepende na kuifuatisha namna ya dunia hii. Katika kitabu cha 1Wakorinto 6:12 imeandikwa ‘Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote VIFAAVYO; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya UWEZO wa kitu chochote’.  Ni vizuri ukahakikisha kwamba ufahamu wako hautawaliwi na mambo yasiyo ya msingi (non-essentials of life) – Je ufahamu wako umetawaliwa ni nini?
Hii ndiyo sababu iliyomfanya Paulo awaambie Waefeso ‘Wala msimpe Ibilisi nafasi’ (Waefeso 4:27) na pia awaambie Warumi “Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili hata kuwasha tamaa zake’. Toleo la KJV linasema ‘But put ye on the Lord Jesus Christ, andMAKE NOT PROVISION for the flesh, to fulfill the lusts thereof’.  Na toleo la ESV linasema ‘But put on the Lord Jesus Christ, AND MAKE NO PROVISION FOR THE FLESH, TO GRATIFY ITS DESIRES’ (Warumi 13:14).  Je hivi leo ni kwa namna gani vijana wanaungalia mwili na kumpa Ibilisi nafasi? – Mitandao ya kijamii, kuangalia na kusoma vitu vichafu, hasira, mawazo, mazingira.
Mfano wa Vijana
  • Kijana azikimbie tamaa za ujanani
Katika 2Timotheo 2:22 imeandikwa ‘LAKINI ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi’. Kijana anawezaje kuzikimbia tama za ujanani? Hebu tuangalie mfano wa Yusufu. Ushindi wa Yusufu dhidi ya mke wa Uria (Mwanzo 39:2-9). Hii ni habari ya kijana Yusufu ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa mali za Potifa.
Pamoja na ushawishi aliokutana nao Yusufu alijibu kwamba ‘Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?’ Mwanzo 39:12 inasema ‘huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake akakimbia akatoka nje. Ili kuzikimbia tamaa za ujanani kijana anapswa (a) ajiepushe na mazingira/marafiki wabaya (Mithali 1:10 & 1Wakorinto 15:33) (b) Ajitenge na uovu (Mithali 16:17, Zaburi 1:1).
Ni muhimu ukakumbuka kwamba hukupewa mwili kwa ajili ya zinaa maana miili yenu ni ni viungo vya Kristo na tena hekalu la Roho Mtakatifu (1 Wakorinto 6:15 & 19), tena yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye (1 Wakorinto 6:17) maana tena imeandikwa ‘Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili’ (1Wakorinto 6:13b). Tena imeandikwa ‘Lakini uasherati USITAJWE kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu’   (Waefeso 5:3).
  • Kijana ajifunze kuenenda kwa roho na si kwa mwili
Katika wagalatia 5:16 imeandikwa ‘Basi nasema ENENDENI KWA ROHO, wala HAMTATIMIZA kamwe TAMAA ZA MWILI. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayoyataka’.
Je kuenenda kwa Roho ndio kukoje?
Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, ATAWAONGOZA awatie kwenye kweli yote (Yohana 16:13) na pia imeandikwa ‘kwa kuwa woteWANAOONGOZWA na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu’ (Warumi 8:14). Kuenenda kwa Roho ina maana ya kuishi kwa kufuata utaratibu/uongozi wa Roho Mtakatifu kwenye maisha yako (Warumi 8:2).
Naam kadri unavyokuwa mtiifu kufuata utaratibu wake ndivyo unavyokuwa mbali na sheria ya dhambi na mauti ambayo ni mwili.Kumbuka imeandikwa ‘kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waiufuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia mwili ni mauti bali nia ya roho ni uzima na amani (Warumi 8:5-6) na pia Wafilipi 4:8.
2
Naam imeandikwa ‘Kila mmoja wenu ajue KUUWEZA MWILI wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu. Maana Mungu HAKUTUITIA UCHAFU, bali tuwe katika utakaso’ (1Thesalonike 4:4-5, 7). Ni jambo la ajabu sana kwamba kwamba tumepewa fursa ya kuiweza miili yetu. Ndio tunapaswa kuuweza mwili kwa maana ya kuudhibiti kwa kuuongoza na kuufanya ufuate nia ya roho.
Kijana mwenzangu kama umechagua kumpa Yesu maisha yako kwa njia ya wokovu,  nakusihi na kukushauri zingatia haya ili kuwa na maisha yenye kielelezo na ushuhuda mzuri maana imeandikwa  ‘Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa’ (2Petro 2:20-21).
Neema ya Kristo iwe nanyi, na tuzidi kuombeana.
Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA.

NAMNA YA KUSIKIA NA KUIELEWA SAUTI YA MUNGU ILI IKUSAIDIE KATIKA KUFANYA MAAMUZI (Sehemu ya 2)

April 8, 2015
Na: Patrick Sanga
1
Mada: Mambo mhumu kujua kuhusu sauti ya Mungu
Katika sehemu ya kwanza ya ujumbe huu niliandika kuhusu mambo matatu ambayo ni kujenga mahusiano na Roho Mtakatifu, kuongeza ufahamu wako kuhusu alama za mawasilano na tatu ujue namna ya kutofautisha sauti ya Mungu na isiyo ya Mungu. Ili kusoma sehemu ya kwanza bonyeza link hii  https://sanga.wordpress.com/2015/04/02/namna-ya-kusikia-na-kuielewa-sauti-ya-mungu-ili-ikusaide-katika-kufanya-maamuzi-sehemu-ya-1/ Sasa fuatana nami tuendelee na mabo mengine muhimu kujua:
  • Vifahamu vikwazo vinavyopelekea kutokusikia sauti ya Mungu
Biblia imeainisha vikwazo kadhaa vyenye kupelekea mtu kutokuisika sauti ya Mungu. Vikwazo hivyo ni pamoja na moja kutenda dhambi au kuishi maisha ya dhambi (Isaya 59: 1-2), pili kukosa uaminifu (Hesabu 12:7-8, 1 Samweli 2:35). Biblia katika Isaya 59: 1-2 inasema ‘Lakini maovu yenu, yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia’ Pia katika Hesabu 12:7-8 imeandikwa ‘Sivyo ilivyo kwa mtumshi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si mafumbo.
2
  • Ongeza ufahamu wako kuhusu njia anazotumia Mungu kuzungumza
Ni dhahiri kwamba zipo njia mbalimbali ambazo Mungu hutumia kusema na wanadamu. Namna Mungu anavyosema na huyu sivyo atakavyosema namtu mwingine. Tofauti hizi zipo tegemeana na mahusainao yaliyopo kati ya Mtu na Mungu na pia ngazi ya kiroho aliyonayo mtu katika ulimwengu wa roho. Hivyo ni muhimu sana kuwa na uelewa wa hizi njia mbalimbali ili kuelewa mazingira yake na hivyo kutafuta kumsika Mungu kupitia njia hizo ili kudumisha mahusiano na mawasiliano yako na Mungu. Katika sehemu ya tatu ya somo hili nitaanza kufundisha njia husika hivyo naamini ufahamu wako utaongezeka.
  • Unahitaji kufahamu umuhimu wa Mungu kuzungumza/kusema nawe
5
Zipo sababu nyingi za Mungu kuzungumza na wanadamu laikini kubwa yenye kuzibeba zote ni ile iliyoandikwa katika Zaburi 32:8 kwamba‘Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama’. Ni muhimu ukakumbuka kwamba kwa mujibu wa Wayumi 8:28 umeitwa ili kulitumika kusudi la Mungu katika siku zako. Ili uweze kulitumika ipasavyo sharti akuongoze katika njia sahihi. Naam njia mojawapo ya kukuongoza na kukufundisha ni kwa yeye kusema na wewe.
Lengo lake katika kusema na wewe ni kukuongoza katika njia sahihi kwa kukuondoa kwenye makusudi ambayo yapo nje na mapenzi yake kwenye maisha yako maana imeandikwa ‘Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam hata mara ya pili ajapokuwa mtu hajali, ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi’ (Ayubu 33:14, 17).
  • Ongeza ufahamu wako kuhusu ulimwengu wa roho
Mambo yote yanayotokea katika ulimwengu wa mwili yameanzia katika uilimwengu wa roho, naam maamuzi ya kile ambacho hutokea katika ulimwengu wa mwili hufanyika katika ulimwengu wa roho. Zaidi hata mapambano (vita vya kiroho) yote aliyoanayo mwamini katika kulitumikia kusudi la Mungu hufanyika katika ulimwengu wa roho.
Hivyo kuwa na ufahamu wa ulimwengu wa roho hususani namna ya kuishi na  kuwasiliana katika ulimwengu huo ni muhimu sana kwa mwamini mwenye kutafuta kujua na kuisikia sauti/mawazo ya Mungu katika maisha yake kwa kuwa Mungu ni roho kama alivyo na Shetani pia. (Rejea 2 Wafalme 6:8-17 na Waefeso 6:10-12).
3
Mpenzi msomaji usiruhusu yale unayoyapitia au yale ambayo watu /mazingira yanasema juu yako yabadilishe au kuongoza maisha yako, bali tafuta kuijua na kuielewa sauti ya Mungu kwenye maisha yako. Na ndiyo maana somo hili limekuja ili kukusaidia kufika mahala ambapo utaweza kuyatenda mapenzi kamili ya Mungu kwenye maisha yako.
Baada ya kuwa tumeangalia mambo haya saba ambayo ni muhimu kujua kuhusiana na sauti ya Mungu, katika sehemu ya tatu nitaanza kuandika kuhusu njia mbalimbali ambazo Mungu hutumia kusema na wanadamu. Somo litaendelea….
Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA.

NAMNA YA KUSIKIA NA KUIELEWA SAUTI YA MUNGU ILI IKUSAIDE KATIKA KUFANYA MAAMUZI (Sehemu ya 1)

April 2, 2015
Na: Patrick Sanga
1
Salaam katika jina la Yesu Kristo na heri ya Pasaka mpenzi msomaji.
Je ni kweli Mungu anazungumza na mwanadamu hata sasa? Hili ni moja ya swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza na kukosa majibu muafaka kwani baadhi yao hawaamini kwamba ni kawaida ya Mungu kuzungumza na wanadamu. Kama ilivyokuwa katika agano la kale, agano jipya, naam hata sasa, Mungu ni yeye yule jana na leo na hata milele. Hivyo ni kusudio la ujumbe huu kuongeza ufahamu wako ili uweze kujua ni kwa namna gani Mungu huzungumza na mwanadamu na kisha nini ufanye ili kumuelewa Mungu anapozungumza. Naam fuatana name sasa katika mfululizo huu…
Kwa nini Mungu azungumze/aseme na mwanadamu? – mtu anahitaji kusikia sauti ya Mungu ili; (a) aishi sawasawa na kusudi au mapenzi ya Mungu awapo hapa duniani      (b) kujenga na kudumisha mahusiano/mawasiliano mazuri kati yake na Mungu (c) kuona kama Mungu aonavyo na hivyo kutafsiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni (Rejea Zaburi 32:8, 1Samweli 3:1 na Isaya 55:8).
Mambo mhumu kujua kuhusu sauti ya Mungu
Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kukusaidia kuijua, kuisikia na kuielewa sauti ya Mungu, nawe hunabudi kuyafahamu na kuyatenda;
  • Jenga na kudumisha mahusiano mazuri na Roho Mtakatifu – Ni vizuri ukafahamu kwamba Roho Mtakatifu yupo duniani sasa akiliongoza kanisa katika kuyatenda mapenzi ya Mungu. Hivyo uwepo wa mahusiano mazuri kati yako na Roho Mtakatifu ndio ufunguo wa mawasilaino mazuri kati yako na Mungu. Biblia katika 1Wakorinto 2:10 inasema ‘Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu… vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu’. Andiko hili linatuonyesha nafasi ya Roho Mtakatifu katika kutusaidia kuisikia sauti ya Mungu. Hivyo jenga na kudumisha uhusiano wako na yeye, itakusaidia sana katika kiujua na kuisikia sauti ya Mungu.
Roho Mtakatifu
  • Ongeza ufahamu wa viashiria (signal) vya mawasiliano kati yako na Mungu                              Ufahamu wa viashiria (signal) za mawasiliano kati yako na Mungu ni wa lazima ili kusikia na kuielewa sauti ya Mungu. Zipo alama mbalimbali kwa kila mwamini ambazo Mungu hutumia katika kusema naye. Biblia katika 1Samweli 3:9 inasema   ‘… Enenda, kalale, itakauwa AKIKUITA, utasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia…’ Jambo ninalotaka ulijue hapa ni kwamba Mungu ana njia nyingi za KUITA, naam anaweza kukuita kwa sauti itokayo kinywani pake au KWA NJIA KUKULETEA ALAMA/VIASHIRIA VYENYE KUKUFANYA UJUE MUNGU ANANIITA. Kama ilivyo kwa jinsi ya kibinadamu anayekuita si lazima aongee, anaweza kutumia alama za mikono au hata maandishi nk, kukuita. Katika kukuita kwa njia ya viashiria/alama Mungu anaweza kuleta nguvu/msisimuko/ubaridi/maumivu fulani kwenye sehemu ya mwili wako au huzuni moyoni mwako kama ishara/kiashiria cha uwepo wake juu yako na hivyo KUTAFUTA/KUTAKA USIKIVU WAKO ILI ASEME NAWE. Hivyo ni lazima uwe na ufahamu na utafute kujua kuhusu alama/namna ya kwako ambayo Mungu hutumia kutafuta usikivu wako.

  • Ni lazima ujue kutofautisha sauti ya Mungu na sauti nyingine                                                                           Hili ni muhimu sana kwako kulielewa ili usije ukaipuuza sauti ya Mungu kwa kudhani ni mawazo yako au ni ya Shetani au usije ukatekeleza jambo ukiamini kwamba Mungu amesema nawe kumbe Shetani ndiye alisema nawe. Katika             1 Samweli 3:7 imeandikwa ‘Basi Samweli alikuwa hamjui BWANA bado, na neno la BWANA lilikuwa bado halijafunuliwa kwake’. Andiko hili linatuonyesha makosa aliyofanya kijana Samweli katika kuielewa sauti ya Mungu akiichanganya na babu yake Kuhani Eli. Ni muhimu ukaelewa kwamba Mungu anaweza kusema na wewe hata kama uko katikati ya mkutano wa watu wenye kelele nyingi sana. Hii ni kwa sababu Mungu hatumii mdomo kusema nasi bali anatumia moyo wako kuzungumza. Moyo ndio kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya mtu na Mungu.
2
Ukisoma katika Matendo ya Mitume 12:22 Biblia inasema ‘Watu wakapiga kelele, wakasema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya Mwanadamu’. Kauli hii ya watu ilikuja baada ya Mfalme Herode kuhutubia watu na kutoa maneno makuu. Watu waliamini kwamba ile ilikuwa sauti ya Mungu, kumbe sivyo na matokeo yake Herode alipigwa na Mungu akafa. Tahadhari, kuna wakati mtu/watu/watumishi wanaweza kunena mambo makubwa na watu wakadhani Mungu wa kweli anasema ndani yao, kumbe ni mungu wa dunia hii. Na ndio maana ni muhimu wewe binafsi uongeze ufahamu wako katika kuijua, kuisikia na kuielewa sauti ya Mungu, ili hata mwanadamu akinena unajua kwamba hili limetoka kwa Mungu wa kweli au vinginevyo.
Naam zipo sauti mbalimbali ambazo zote zinalenga kupambana/kuharibu kusudi la Mungu ndani ya mtu, zipo sauti za wanadamu (wazazi, walezi, mwenza wa ndoa, viongozi wa kiroho), ipo sauti ya Shetani kupitia majeshi ya pepo wabaya nk. Ni lazima mwanadamu amjue sana Mungu kiasi cha kuweza kutofautisha sauti hizi. Na namna pekee ya kutofautisha sauti hizi na ile ya Mungu ni kuwa na ufahamu mkubwa wa neno la Mungu kwani Mungu hawezi kukuagiza kutenda jambo lililo kinyume na neno lake.
Photo 3
Katika sehemu inayofuata nitakuonyesha mambo mengine kadhaa kujua na kuyaelewa kabla sijaanza sasa kuandika kuhusu njia ambazo Mungu hutumia kusema na wanadamu. Maombi yako ni muhimu sana.
Kwa mara nyingine heri ya Pasaka na amani ya Kristo iwe nawe. Tutaendelea na sehemu ya pili…
Utukufu na heshima vina wewe Yesu! Wastahili BWANA.