1Wakorintho 13:1-6
  Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
 2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, 
nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama 
sina upendo, si kitu mimi.
 3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
 4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
No comments:
Post a Comment