Menu

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo

Wednesday, February 4, 2015

VITA VYA KIROHO


Awali ya yote ninamshukuru Mungu kwa afya,ya rohoni pia ya mwilini.Pia ni matumaini yangu wewe U mzima pia.
Nina kukaribisha katika tafakari hii nzuri ya somo ambalo litakupa mbinu nzuri za kuwa mkristo jasiri katika imani ya maisha ya utauwa.

Yamkini ulishajifunza kuhusu somo kama hili la VITA VYA KIROHO,Lakini sio vibaya tukajifunza tena hapa na wala hautapungukiwa ,maana Roho mwenyewe ni mpya kila iitwayo leo.
Ni mara chache kusikia mchungaji anafundisha somo hili.
Ni mara chache kusikia mafundisho yanayohusu mambo ya rohoni,Lakini leo nataka nikujuze kwa habari ya mambo ya rohoni,KWAMBA TUKO VITANI.
Ninapozungumzia habari ya VITA,ninazungumzia habari ya mashindano makali baina ya pande mbili au zaidi. Vita ni kufa au kupona.Ndani ya mashindano haya ni lazima mmoja au upande mmoja ushinde na upande mwingine ushindwe .
Vita yoyote ni lazima ihusishe :
• Silaha.
• Wapiganaji.
• Sehemu/Mahali kwa kupigania ( LOCATION).

Hivyo basi ninapozungumzia habari ya vita vya kiroho ninazungumzia mashindano makubwa sana baina yetu ya sisi wafuasi wa Kristo Yesu kwa kutumia silaha za Mungu,dhidi ya adui yetu shetani na mapepo yake yote.,Tukipigana katika uwanja wa ULIMWENGU WA ROHO. 
KUMBUKA ;
Ndani ya vita hivi vya kiroho ,hakuna kutoka sale ( kutoka droo), Ni Either Upigwe au upige kulingana na namna gani ulivyoji-position na Kristo Yesu.
Nasema vita hivi ni vya Wakristo halisi/waliokoka dhidi ya shetani,Kwa maana wale ambao sio wakristo au wale wakristo wa majina tu, au wale wakristo wa mapokeo ya dini,au wale wapagani,
Kwa hao wote vita hivi haviwahusu kabisa,MAANA HAO NI MALI YAKE SHETANI SASA HUYO SHETANI APIGANE NAO KWA LIPI ?! ,MAANA HAO NI MALI YAKE. ANA WAMILIKI ATAKAVYO YEYE.
Bali sisi tulio kinyume naye huyo shetani,ndio twapigana hata kumwaga damu,maana tumemkana shetani na mapepo yake yote.Nasi hiyo Vita inatuhusu moja kwa moja.

Wakristo wengi hivi leo,wale wapendwa,wapo katika hali ya hofu kubwa na mashaka juu ya shetani hata kusababisha wasiweze kufanikisha mambo yao binafsi, 

Ukiwa ni mwanafunzi mzuri wa Yesu Kristo haupaswi kumkimbia shetani na mapepo yake, BALI YEYE NDIO YAMPASA KUKUKIMBIA WEWE. Pamoja na hayo mapepo yake yakimbie mbele yako,
Tazama LUKA 8 : 26-28
“ 26 Wakafika pwani ya nchi ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya. 
27 Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini. 
28 Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese. “
Tazama hapo jeshi la mapepo languka mbele ya Yesu,wekitetemeka na wakimsihi wasiteswe,
Hata wewe mkristo Uliyempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako hukamaanisha kutembea katika kweli,nawe ukamvaa Yesu, Hakika jeshi la mapepo litakimbia mbele yako,Kwa maana sio wewe upiganaye katika vita hivyo Bali ni Yeye Yesu Kristo aliye dani yako,maana Yeye ni mkuu kuliko hao vinyamkera.Ikiwa utatembea na Yesu Kwa ukamilifu
Nami ninashang’aa sana kwako wewe mkristo ulalae kama watu wa mataifa, Yaani wewe siku zote unalala mapema tena hata bila kuomba, kwa kizingizio kwamba ‘’ Eti siku hizi ninachoka sana ‘’ 
Kwa taharifa yako adui naye ni mjanja pindi unapoona umechoka ndipo unapompa mwanya,anapokuangamiza na kukupiga,Amka ewe mwana wa Mungu,Omboleza usiku,lia mbele za Bwana wako,acha watu wa mataifa wakalale ,nawe pambana usiku.tena utauona ushindi.
Tazama Mungu asema vita si vyetu bali ni vya kwake,lakini hajakuambia ulale bali upambane
Tazama Yoshua aambiwavyo na Bwana Mungu ;
YOSHUA 1 : 6 
“ 6 Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. ‘’
Katika vita hii ya wokovu,Mungu alikuwa upande wa akina Yoshua laki bado anamwambia “ UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA “ 
Vivyo hivyo wewe mkristo usichoke kupambana,Hivyo Nami nataka hufahamu kwamba ;
• Kila Mkristo halisi yule aliye ndani ya Yesu,yupo vitani,
• Vita vyetu si vya damu na nyama ,Bali katika ulimwengu wa roho.

Okey;
Ikwa Vita vyetu ni katika ulimwengu wa roho Basi ni dhahili kabisa kila jambo unaloliona asili yake ni rohoni .
Kila jambo hulionalo limetokea ujue lilikwisha tokea katika ulimwengu wa roho kwanza,kisha ndipo la dhihilika katika ulimwengu wa mwili,
Tazama WAEBRANIA 11 : 3 ;
“3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. “

Unapoona wanandoa wakitengana ujue walishatengana kwanza katika ulimwengu wa r oho,
Unapooana machafuko yoyote yale katika ulimwengu wa mwili ujue katika ulimwengu wa roho mambo huko si shwari.
Yeyote Yule awezaye kupiga shetani na mapepo yake katika ulimwengu wa roho,ujue hata katika ulimwengu wa mwili aweza kumpiga.
Lakini ni lazima leo nikutangazie kwamba ;
Ipo njia moja tu ya ushindi ndani ya vita vya kiroho nayo Ni Yesu kristo kuwa upande wako, Maana Yesu Kristo alishampiga huyo ibilisi tungu awali na kumtupa chini kwa nguvu ya damu yake Yesu Kristo Damu ya thamani.

No comments:

Post a Comment