Menu

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo

Sunday, February 1, 2015

WALAKA KWA WAEFESO

WAEFESO 1 Utangulizi Paulo aliandika waraka huu akiwa gerezani huko Rumi ili kuwatia moyo waamini wa Asia.Unaposoma kwa uangalifu waraka huu, ingawa Paulo alifungwa huko Kaisaria, utaona kwamba waraka huu uliandikwa kutoka Rumi ambako Paulo alikuwa na uhuru wa kuhubiri Injili (Mdo.28).Waraka huu ulikuwa kama mwongozo uliokusudiwa kwa makanisa kadhaa.Katika maandiko mengine ya zamani neno “huko Efeso” halipo. Zaidi ya hayo, kwenye waraka huu hakuna salamu za watu binafsi, wala hakuna matatizo maalum au hali maalum ya kanisa la mahali pamoja inayotajwa. Pia mafundisho yaliyomo ni yenye upana mkubwa.Ingawa kanisa la Efeso ambako Paulo alihudumu kwa zaidi ya miaka miwili linajumuishwa humo, ni wazi kwamba waraka huu ulikusudiwa kwa makundi mengine ya kanisa kwa ujumla katika eneo hilo la kijeografia la Efeso, yaani, makanisa ya jirani. Katika waraka huu, Paulo anapotaja “Kanisa” ana maana ya “Kanisa la po pote.” Anaeleza kwamba Kanisa limeanzishwa na Mungu, akiwaelezea mpango wa Mungu wa tangu awali wa kuwaokoa watu Wake kwa njia ya Kristo. Mpango huu ulikuwako hata kabla ya ulimwengu kuumbwa. Kwa wakati huu, wote wanaomwamini Kristo wanaokolewa kwa neema. Mwenendo wa mwamini uko kinyume kabisa na ule wa maisha ya kale, akionyesha maisha ya kiroho kama “maisha katika ulimwengu wa roho”. Ingawa inawapasa watu wa Mungu kupigana vita kali na nguvu za Shetani (6:12), kanisa linashinda na hatimaye uovu unashindwa.Sisi tunaomwamini Kristo ni viungo vya mwili Wake, yaani, Kanisa, kwa hiyo tunao uwezo wa kushinda. Katika sehemu ya mwisho ya waraka huu, Paulo anaeleza juu ya maisha yanayowapasa wakristo kuhusu: Ndoa, tabia, mwenendo, wazazi na watoto wao pia watumishi na mabwana zao. Wazo Kuu Kiini cha ujumbe wa waraka huu ni kwamba: Mpango wa Mungu wa milele wa kuuokoa ulimwengu unatimizwa kwa njia ya Kristo katika mwili Wake, yaani, Kanisa Lake. Mtu anapoamini, anakuwa ndani ya Kristo na anapata wokovu na kuwa salama. Mungu aliandaa wokovu huu tangu milele na amempa kila aaminiye mambo yote anayohitaji katika maisha yake ili aweze kusimama, ila ni wajibu wake kupokea mambo hayo aliyowekewa tayari. Paulo anamalizia kwa kufafanua mambo ambayo Mungu amewaandalia wale wamwaminio, kusudi waweze kumshinda Shetani anapowashambulia na baada ya mapambano wawe na ushindi wa kudumu. Mwandishi Mwandishi wa waraka huu ni Paulo (1:1). Tarehe Waraka huu uliandikwa 60 B.K.wakati wa kifungo cha Paulo cha miaka miwili. Mahali Rumi. Mgawanyo • Mpango wa Mungu na wokovu wa wote wamwaminio (1:1-2:22) • Siri ya Injili (3:1-21) • Maisha ya mkristo duniani (4:1-5:21) • Jinsi wakristo wapaswavyo kuhusiana (5:22-6:9) • Kupigana na uovu (6:10-24) WAEFESO 2 Salamu Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu, Kwa watakatifu walioko Efeso walio waaminifu katika Kristo Yesu. 2Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi. Baraka Za Kiroho Zitokazo Kwa Kristo 3Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo. 4Kwa maana alituchagua katika Yeye kabla ya kuumbwa ulimwengu ili tuwe watakatifu na bila lawama mbele Zake. 5Kwa upendo alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo kwa furaha Yake na mapenzi Yake mwenyewe. 6Kwa hiyo tunamsifu Mungu kwa huruma zake kuu alizotumiminia kwa sababu sisi ni wa Mwanae Mpendwa. 7Katika Yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu Yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema Yake 8aliyotumiminia kwa wingi, kwa hekima yote na maarifa yote. 9Naye alitujulisha siri ya mapenzi Yake sawasawa na uradhi wa mapenzi Yake, ambayo alikusudia katika Kristo, 10ili yapate kutimizwa katika wakati mkalimifu utakapowadia, yaani, kuvitia vitu vyote vya mbinguni na vya duniani pamoja chini ya kiongozi mmoja, ndiye Krsto. 11Katika Kristo sisi nasi tumepata urithi, tukiisha kuchaguliwa sawasawa na kusudi la Mungu, Yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na mapenzi Yake. 12Ili kwamba, sisi tuliokuwa wa kwanza kuweka tumaini katika Kristo, tupate kuishi kwa sifa ya utukufu Wake. 13Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake mlitiwa mhuri, kwa yule Roho Mtakatifu wa ahadi mliyeahidiwa, 14yeye ndiye amana ya urithi wetu hadi ukombozi wa milki yake kuwa sifa ya utukufu Wake. Shukrani Na Maombi 15Kwa sababu hii tangu niliposikia juu ya imani yenu katika Bwana Yesu na upendo wenu kwa watakatifu wote, 16sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, nikiwakumbuka katika maombi yangu. 17Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi. 18Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa utukufu Wake kwa watakatifu 19na uweza Wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno 20ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamketisha mkono Wake wa kuume katika mbingu, 21juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. 22Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu Yake na amemfanya Yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, 23ambalo ndilo mwili Wake, ukamilifu Wake Yeye aliye yote katika yote. Tumefanywa Kuwa Hai Ndani Ya Kristo Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu, 2ambazo mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi ndani ya wale wasiotii. 3Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukifuata tamaa za mwili na mawazo yake. Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama mtu mwingine ye yote. 4Lakini Mungu, kwa upendo Wake mwingi kwetu sisi, ambaye ni mwingi wa rehema, 5hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, yaani, mmeokolewa kwa neema. 6Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu, 7ili katika ule ulimwengu ujao apate kuonyesha wingi wa neema Yake isiyopimika, iliyodhihirishwa kwetu kwa wema Wake ndani ya Kristo Yesu. 8Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala hii si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, 9si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. 10Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika hayo. Wamoja Katika Kristo 11Kwa hiyo kumbukeni kwamba ninyi ambao hapo awali mlikuwa watu Mataifa kwa kuzaliwa mlioitwa, “Wasiotahiriwa” na wale wanaojiita “Waliotahiriwa,” yaani, tohara (ifanyikayo katika 1 2WAEFESO 3 mwili kwa mikono ya wanadamu), 12kumbukeni kwamba wakati ule mlikuwa hamna Kristo, mkiwa wageni katika jumuiya ya watu wa Mungu, yaani, Israeli na wageni katika lile agano la ahadi, mliishi duniani mkiwa hamna tumaini wala Mungu. 13Lakini sasa katika Kristo Yesu, ninyi ambao hapo kwanza mlikuwa mbali na Mungu, sasa mmeletwa karibu kwa njia ya damu ya Kristo. 14Kwa maana Yeye mwenyewe ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi tuliokuwa wawili, yaani, Wayahudi na watu Mataifa tuwe wamoja kwa kuvunja kizuizi na kubomoa ule ukuta wa uadui uliokuwa kati yetu. 15Kwa kuibatilisha ile sheria pamoja na amri zake na maagizo yake alipoutoa mwili wake, ili apate kufanya ndani yake mtu mmoja mpya badala ya hao wawili, hivyo akifanya amani, 16naye katika mwili huu mmoja awapatanishe wote wawili na Mungu kwa kupitia msalaba, ambao kwa huo aliangamiza uadui wao. 17Alikuja na kuhubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali na pia akahubiri amani kwao waliokuwa karibu. 18Kwa maana kwa kupitia Kwake, sisi sote tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja. 19Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena wala wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na watakatifu na pia jamaa wa nyumbani Mwake Mungu. 20Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni. 21Ndani Yake jengo lote limeshikamanishwa pamoja na kusimamishwa ili kuwa hekalu takatifu katika Bwana. 22Katika Yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambayo Mungu anaishi ndani yake kwa njia ya Roho Wake. Huduma ya Paulo kwa Watu Mataifa Kwa sababu hii, mimi Paulo, nimekuwa mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi watu Mataifa. 2Kwa hakika mmekwisha kusikia kuhusu ile huduma ya neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu 3na jinsi ile siri ilivyodhihirishwa kwangu kwa njia ya ufunuo, kama nilivyotangulia kuandika kwa kifupi. 4Kwa kusoma haya, basi mtaweza kuelewa ufahamu wangu katika siri ya Kristo. 5Siri hii haikudhihirishwa kwa wanadamu katika vizazi vingine kama vile sasa ilivyodhihirishwa na Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu. 6Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili, watu Mataifa ni warithi pamoja na Israeli, viungo vya mwili mmoja na washiriki pamoja wa ahadi katika Kristo Yesu. 7Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu Yake itendayo kazi. 8Ingawa mimi ni mdogo kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa watakatifu wote, nilipewa neema hii ili niwahubirie watu Mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo na 9kuweka wazi kwa kila mtu jinsi ile siri iliyokuwa imefichwa kwa nyakati zote katika Mungu aliyeumba vitu vyote. 10Ili kwa njia ya Kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kujulikana kwa watawala na wenye mamlaka katika ulimwengu wa roho, 11sawasawa na kusudi Lake la milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. 12Yeye ambaye ndani Yake na kwa njia ya imani katika Yeye tuweze kumkaribia Mungu kwa ujasiri na kwa uhuru. 13Kwa hiyo, nawaomba msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, hayo ni utukufu wenu. Maombi Ya Paulo Kwa Waefeso 14Kwa sababu hii nampigia Baba magoti, 15ambaye kwa Yeye ubaba wote wa kila jamaa za mbinguni na za duniani unaitwa. 16Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kwa njia ya Roho Wake kwa kadri ya utajiri wa utukufu Wake, 17ili kwamba, Kristo apate kukaa mioyoni mwenu kwa njia ya imani. Nami ninaomba kwamba ninyi mkiwa wenye mizizi tena imara katika upendo, 18mwe na uwezo wa kufahamu pamoja na watakatifu jinsi ulivyo upana na urefu na kimo na kina upendo wa Kristo 19na kujua upendo huu kwamba unapita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wa Mungu. 20Basi kwa Yeye awezaye kutenda mambo ya ajabu yasiyopimika kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya uweza Wake ule utendao kazi ndani yetu, 21Yeye atukuzwe katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amen. Umoja Katika Mwili Wa Kristo Basi, mimi niliye mfungwa wa Bwana, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa. 2Iweni wanyenyekevu kabisa na wapole, mkiwa wavumilivu, mkichukuliana kwa upendo. 3Jitahidini kudumisha umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 4Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja. 5Tena 3 4WAEFESO 4 kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, 6Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote. 7Lakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Kristo. 8Kwa hiyo husema, “Alipopaa juu, aliteka mateka akawapa wanadamu vipawa.” 9(Asemapo “Alipaa juu,” maana yake nini isipokuwa ni kusema pia kwamba Kristo alishuka pande za chini sana za duniaa? 10Yeye aliyeshuka ndiye aliyepaa juu sanab, kupita mbingu zote, ili apate kuvijaza vitu vyote. 11Yeye ndiye aliyeweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na wengine kuwa walimu, 12kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili kwamba mwili wa Kristo upate kujengwa. 13mpaka sote tutakapoufikia umoja katika imani na katika kumjua sana Mwana wa Mungu na kuwa watu wazima kwa kufikia kipimo cha ukamilifu wa Kristo. 14Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwatupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho kwa hila za watu, kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za udanganyifu. 15Badala yake, tukiambiana kweli kwa upendo, katika mambo yote tutakua, hata tumfikie Yeye aliye kichwa, yaani, Kristo. 16Kutoka Kwake, mwili wote huunganishwa na kushikamanishwa pamoja kwa msaada wa kila kiungo, hukua na kujijenga wenyewe katika upendo, wakati kila kiungo kinafanya kazi yake. Maisha Ya Zamani Na Maisha Mapya 17Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao. 18Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao na ugumu wa mioyo yao. 19Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi. a9 Pande za chini sana za dunia hapa maana yake ni sheol kwa Kiebrania, yaani, kuzimu b10 Juu sana hapa ina maana mbingu za mbingu 20Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyomjifunza Kristo. 21Kama hivyo ndivyo ilivyo, ninyi mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile kweli ilivyo katika Yesu. 22Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu. 23Mfanywe upya roho ya nia zenu, 24mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawa sawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu. Kanuni Za Maisha Mapya 25Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja. 26Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika, 27wala msimpe ibilisi nafasi. 28Yeye ambaye amekuwa akiiba, asiibe tena, lakini mtu wa namna hiyo lazima ajishughulishe, tena afanye kitu kifaacho kwa mikono yake mwenyewe, ili awe na kitu cha kuwagawia wahitaji. 29Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yafaayo kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao. 30Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwa huyo mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi. 31Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu. 32Iweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. Kue Kwa hiyo, mfuateni Mungu kama watoto wapendwao, 2Mkiishi maisha ya upendo, kama vile Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu. nenda Nuruni 3Lakini uasherati, usitajwe miongoni mwenu, wala uchafu wa aina yo yote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu. 4Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu. 5Kwa habari ya mambo haya mjue hakika kwamba: Mwasherati, wala mtu mwovu, wala mwenye tamaa mbaya, mtu kama huyo ni mwabudu sanamu, ambaye kamwe hataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu. 6Mtu ye yote na asiwadanganye kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu 5WAEFESO 5 ya wale wasiomtii. 7Kwa hiyo, msishirikiane nao. 8Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru 9(kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli,) 10nanyi tafuteni yale yanayompendeza Bwana. 11Msishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni. 12Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini. 13Lakini kila kitu kilichowekwa nuruni, huonekana, 14kwa kuwa nuru ndiyo hufanya kila kitu kionekane. Hii ndiyo sababu imesemekana: “Amka, wewe uliyelala, ufufuke kutoka katika wafu, naye Kristo atakuangazia.” 15Kwa hiyo iweni waangalifu jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima, 16mkiukomboa wakati, kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. 17Kwa hiyo msiwe wajinga, bali mpate kujua nini yaliyo mapenzi ya Bwana. 18Pia msilewe kwa mvivyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho. 19Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu, 20sikuzote mkimshukuru Mungu Baba katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo kwa kila jambo. 21Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kwa heshima kwa ajili ya Kristo. Mafundisho Kuhusu Wake Na Waume 22Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana. 23Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha Kanisa,ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni Mwokozi wake. 24Basi, kama vile Kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo. 25Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake 26kusudi alifanye takatifu, akilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno lake, 27apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lo lote, bali takatifu lisilo na hatia. 28Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza Kanisa Lake. 30Sisi tu viungo vya mwili Wake. 31“Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe na hawa wawili watakuwa mwili mmoja.” 32Siri hii ni kubwa, bali mimi nanena kuhusu Kristo na Kanisa. 33Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe. Mafundisho Kuhusu Watoto Na Wazazi Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. 2“Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, 3“upate baraka na uishi siku nyingi duniani.” 4Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana. Mafundisho Kuhusu Watumwa Na Mabwana 5Ninyi watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnavyomtii Kristo. 6Watiini, si tu wakati wakiwaona ili mpate upendeleo wao, bali mtumike kama watumwa wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. 7Tumikeni kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na si wanadamu. 8Mkijua kwamba Bwana atampa kila mtu thawabu kwa lo lote jema alilotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru. 9Nanyi mabwana, watendeeni watumwa wenu kwa jinsi iyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba Yeye aliye Bwana wenu na Bwana wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo. Silaha Za Mungu 10Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu Zake. 11Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za Shetani. 12Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara. 14Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15nayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani. 16Zaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa 6WAEFESO 6 hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17Vaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu. 18Mkiomba kwa Roho sikuzote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote. 19Niombeeni na mimi pia, ili kila nifuanguapo kinywa changu, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili kwa ujasiri, 20ambayo mimi ni balozi wake katika vifungo. Ombeni kwamba nipate kuhubiri kwa ujasiri kama inipasavyo. Salamu Za Mwisho 21Tikiko aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawaambia kila kitu ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya sasa. 22Ninamtuma kwenu kwa ajili ya kusudi hili hasa, ili mpate kujua hali zetu na kuwatia moyo. 23Amani iwe kwa ndugu na pendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo. 24Neema iwe na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo kwa pendo wa dhati. Amen.