Menu

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo

Wednesday, October 1, 2014

MUNGU ANASEMA NINI JU YA ADUI ZETU,

Mungu anasema ya kwamba tusilipize kisasi maana kisasi ni chake yeye na kuwapenda maadui zetu. Imeandikwa Warumi 12:19-21 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.