Vichwa vya Habari

SADAKA YENYE MAANA NA YA KUMPENDEZA MUNGU

 SADAKA YENYE MAANA NA YA KUMPENDEZA MUNGU

Mpendwa wangu nakusalimu katika jina la Yesu.
Nina jambo la kukushirikisha siku ya leo kwa habari ya kumtolea Mungu sadaka yenye maana. Unajua kwamba Mungu amelinunua kanisa kwa damu yake ya  thamani; damu ya mwana kondoo wa Mungu Yesu Kristo (Ufunuo 5:9 & 1Kor 6:20). Na kwa kuwa Mungu anaweza kuvitoa vitu vyake vya thamani kwa ajili yetu, yeye ni mfano wa utumishi wa utoaji; nasi tunapaswa kuuiga mfano huu wa utoaji. Lakini si kuuuiga tu bali pia Mungu anatuagiza kumtolea vitu vya thamani tulivyonavyo. Haipaswi kumtolea Mungu vitu dhaifu. Haipaswi ndugu yangu. Haipaswi kabisa. 
"...nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema Bwana.   Lakini na alaaniwe mtu mwenye kudanganya, ambaye katika kundi lake ana mume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema Bwana wa majeshi, na jina langu latisha katika Mataifa" #Malaki 1:13,14
Kuna watu wanamtolea Mungu vitu vya kiudhalimu. Wanaiba huko walikoiba halafu wanakuja kumtolea Mungu kama sadaka. Mungu haitaki sadaka ya namna hiyo. 
Kuna watu wanamtolea Mungu vitu vya halali lakini wanaangalia vile vitu visivyo na thamani ndivyo wanavitoa sadaka. Kama ni wanyama basi wataangalia wale wanyama dhaifu ndo wawatoe sadaka. Kama ni vitu basi wataviangalia vitu dhaifu ndo wavitoe sadaka. Mungu na akuhurumie.
Yesu siku moja akiwaangalia watu wakitoa sadaka akamwona mama mjane akasema huyu ndiye aliyotoa kuliko wote maana alitoa vyenye thamani kwake kuliko wengine.
"
Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili. Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote; maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo" - Luka 21:1-4
Kama ni suruali basi ataangalia suruali iliyochoka ndo mtu amtolee Mungu sadaka. Kale kasuti kalikombanabana na kamechakaa ndo anakatoa sadaka.  Kama ni gari basi anaangalia gari yake ilochokachoka ndo anaitoa sadaka. Ndugu Mungu hataki vitu dhaifu umtolee sadaka.

Kuna watu wanaangalia hata noti zilizochakaa chakaa ndo wanamtolea Mungu sadaka. Mbingu na zikuhurumie.
Mungu anasema usimtolee kilichokigonjwa wala kilema. Mtolee Mungu sadaka ya thamani kama ambavyo alikununua kwa damu ya thamani pale msalabani.
Mungu atuhurumie sana.

Usiache kutufuatilia kwenye facebook hapa au kwenye twitter hapa.

Kama una maoni usisite kutuachia maoni yako hapa au kushare neno hili katika mitandao ya kijamii. Kama una jambo lolote la kutushirikisha basi tutumie kupitia ushuhudainjili@gmail.com

NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.