Vichwa vya Habari

ZAKA NI SADAKA YA AGANO JIPYA NA MUNGU

ZAKA NI SADAKA YA AGANO JIPYA


ZAKA NI SADAKA YA AGANO JIPYA; NA HUO NDO UKWELI, ILA KUITOA AMA KUITOA NI SWALA LA UTII WAKO!

Malaki 3:7, "Mimi Ni Mungu Nisiyekuwa Na KIGEUGEU"
Tafsiri Ya Kiingereza Inasema, "FOR AM GOD; I CHANGE NOT"
Kwa Kiswahili Naweza Kuisema Hivi; "MIMI NI MUNGU; KAMWE SIBADILIKI" Au "MIMI NI MUNGU NISIYEBADILIKA"
Lengo Kubwa La Kukuandikia Mstari Huu Ni Ili Nikusaidie Katika Jambo Hili; "MUNGU NI MUNGU ASIYEBADILIKA; KANUNI NA TARATIBU ALIZOZIWEKA 'NI ZA ROHONI' HAZIGEUKI, HAZIPITWI NA WAKATI, WALA HAZIKOMI KUFANYA KAZI"
Kama Ukiiona KANUNI YA KIMAFANIKIO "KWENYE AGANO LA KALE" Ukaielewa Na Kuitumia Sasa "KWENYE AGANO JIPYA" Itakupa Matokeo Yaleyale Kama Waliyopata Watu Wa Agano La Kale Bila Kuathiriwa Na MAJIRA WALA NYAKATI; Maana YOTE YATAPITA, LAKINI NENO LA MUNGU LADUMU MILELE MBINGUNI!
Ndio Maana Huwa Sipendi Kujibizana Na Mtu Anayejaribu KUPINGA UTOAJI WA ZAKA [FUNGU LA KUMI] Akisema "NI MAMBO YA AGANO LA KALE HAYO"... Usipoitoa ZAKA Maana Yake Unasema, "SIHITAJI KUPATA BARAKA ANAZOMWAGA MUNGU KATIKA GHALA YANGU HATA KUSIWEKO NAFASI, WALA SIHITAJI MUNGU AMKEMEE YEYE ALAYE; WALA SIHITAJI MUNGU WA IBRAHIMU BABA YANGU [KUPITIA KRISTO] ANITUKUZE NA KUWAFANYA MATAIFA WANIITE HERI" (Malaki 3:10-12).
Wajanja Tunatoa ZAKA Kwa Sababu Tunajua "MFALME WA WAFALME" Aliweka SADAKA HIYO ILI KUWASAIDIA "WAZAO WA RAFIKI YAKE IBRAHIMU" Ambao Sisi Pia Tu Wanae Kupitia IMANI KATIKA KRISTO YESU (Wagalatia 3:7-9, 14-15, 29)... Kwa Hiyo TUNAICHANGAMKIA "KANUNI ILIYOMFANIKISHA IBRAHIMU, ISAKA NA ISRAELI" Maana Inafanya Kazi Na "MUNGU YULEYULE WA BABA YETU IBRAHIMU NDIO MUNGU HUYOHUYO KUPITIA KWA YESU"
Biblia Inamwita YESU Kuwa Ni "MWANA WA IBRAHIMU" (Mathayo 1:1), Ili Sisi TULIOOKOKA Kupitia KWA YESU "TUPATE HAKI KISHERIA YA KUJIPENYEZA KUINGIA KWENYE UZAO WA IBRAHIMU" (Wagalatia 3:7-9, 14-15, 29), Na Kama TUMEKUWA WAZAO WA IBRAHIMU, LAZIMA TUFUATE "KANUNI NA UTARATIBU WA ZAKA" Ambao "WAISRAELI/ WAEBRANIA" Wanaufuata Hadi Leo "ILI KUSIMAMISHA AGANO [KULIFANYA ACTIVE] ALILOWEKA NA IBRAHIMU"
Tatizo Ni Kwamba Wasomaji Wa Biblia Wa Sasa HAWASOMI KWA "JICHO LA ROHONI" Hivyo Wanakosa UFUNUO Na Kudhani SADAKA YA ZAKA [FUNGU LA KUMI] NI KITU CHA AGANO LA KALE; Hapa Ndipo Utakapowasikia Wakiseama, "NIPE MAANDIKO ILI KUTHIBITISHA KUWA ZAKA TUNAITOA KWENYE AGANO JIPYA"
Mimi Nikimsikia Mtu Wa Aina Hii Najua Ni "MCHANGA KIROHO" Hata Kama "NI ASKOFU AU MTUME AMA NABII"

Makala hii imeandikwa na Neema ya Kristo na waweza kumpata facebook gonga hapa


 ---------------------------------------------------------------------------------
Kama una ushuhuda na ungetamani tuwashirikishe na wengine kupitia blogu yako ya Kikristo isiyofungamana na dhehebu lolote usiache kuwasiliana nasi kwenye facebook au tutumie kupitia ushuhudainjili@gmail.com
 
Mungu akubariki sana kwa kufuatana nasi.
Usiache kutufuatilia kwenye Facebook pamoja na

No comments:

Post a Comment

NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.