NGUVU YA MUNGU ILIYOPO KATIKA KINYWA CHAKO.
BWANA YESU asifiwe Wana wa MUNGU.
Napenda kuleta kwenu somo hili:
Je Unakiri nini?
“Nanyi mtapokea nguvu akiisha kuwajilia
juu yenu ROHO MTAKATIFU, (Matendo 1: 8).
Je, tunatumia hii nguvu ya MUNGU?
Na je tunaitumia mamlaka ya KRISTO
tuliyopewa kama inavyotakiwa?
Haijalishi mwana wa MUNGU unapita katika magumu kiasi gani, Unachotakiwa
ni kubadilisha kukiri kwako, na kadri unavyotamka kinyume na mazingira yanavyoonekana,elewa
kuna jambo katika ulimwengu wa Roho linafanyika, hata kama huna shilingi mia mfukoni
wewe sema pesa zipo, hata kama wewe ni mgonjwa
umelala kitandani Sema mimi ni mzima, maana Neno la MUNGU linasema aliye dhaifu na aseme ana nguvu.
Ezekieli alipoonyeshwa lile bonde
la mifupa mikavu, kwa macho ya damu na nyama
aliona haiwezekani kwa ile mifupa mikavu kuwa na uhai tena ,lakini MUNGU akamwambia
itabirie hii mifupa mikavu ipate kuishi.
Ndipo Ezekieli akatambua nguvu iliyopo katika kinywa chake, akaanza kutoa
unabii na kuitabiria ile mifupa, akaiambia
’’ enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la BWANA; BWANA MUNGU aiambia mifupa
hii maneno haya; Tazama nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi .Nami nitatia mishipa
juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, nakutia pumzi ndani
yenu nanyi mtaishi.’’ Maneno haya tunayapata
katika kitabu cha (Ezekieli 37:1…..)
Katika maandiko haya tumeona, ni jinsi gani Ezekiel ialivyoweza kutumia nguvu
na uweza ulioko ndani ya kinywa chake na kuweza kuleta uhai tena. Na wewe mwana
wa MUNGU nini ni kimekuwa mifupa mikavu katika maisha yako?
-Yamkini ni ndoa ndio imekuwa mifupa mikavu itabirie nayo itakuwa hai tena,
-au ni uchumi wako,
- afya yako,
-watoto wako,
-hudumayako,
MUNGU anakuambia leo simama na uvitabirie, maana kuna nguvu katika kutamka.
Unakiri nini kushindwa au kushinda?
Nguvu ya MUNGU iko juu yako, badilisha yale yote yanayoonekana kuwa yameshindikana
na yatawezekana kupitia kinywa chako katika Jina la YESU KRISTO mwenye nguvu
zote. AMEEEN.
MUNGU awabariki sana.