Vichwa vya Habari

MAOMBI NI VITA! - MWAKASEGE


"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho" EFE 6:12.

Ndugu yangu, Paulo anatueleza jambo zito sana katika waraka wake huu. Paulo anatufundisha kubeba silaha zote za kupigana na adui ili tuweze kusimama kwa ushindi katika hivi vita. Pamoja na silaha zote anamalizia katika mstari wa kumi na nane kwa kusema kwamba "kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo ".!
Anatuambia kwamba kupigana kwetu huku ni kwa njia ya maombi! Kimahesabu, vita vyetu hivi tunavipiga kwa kutumia maombi. Vita hivi vya kiroho tunavipiga kwa kutumia maombi. Maombi ni silaha kubwa katika vita hivi. Ukiangalia silaha zote ambazo anazitaja (1. Kweli 2. Haki (Maisha safi yenye utii) 3. Utayari ktk huduma 4. Imani 5. Wokovu (Uhakika wa mahusiano ya mtu binafsi na Mungu) 6. Upanga wa Roho ambao Neno la Mungu ) Silaha kuu yenye kubeba silaha zote hivi ni maombi! "kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho".
Ndugu, kila siku unapaswa kukaa mkao wa kivita. Paulo anamuonyesha adui kama mtaalamu wa kupanga vita hivi. Ndo maana Paulo asema ktk mstari wa kumi na moja "Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani". Shetani ni mwenye hila kila wakati. Katika kazi zako ataweka hila, katika huduma yako ataweka hila. Katika kanisa lako ataweka hila. Katika uchumi wako ataweka hila. Kila kutaka kwako kumjua Mungu ataweka hila. Basi Paulo asema Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Basi acha kulala mtumishi. Simama tuvipige hivi vita. Kuna watu wanajiona hawana huduma katika kanisa. Huduma hii ya ukamanda wa maombi nafasi hii inakusubiri. Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Chukua hatua. Tumia mbinu zote za kivita vya kiroho tuweze kupambana na adui. 
Tuungane pamoja katika vita hii pia kwa ku-like page yetu tushirikiane katika kuvipiga vita hivi katika jina la Yesu na damu ya mwanakondoo.


Kama una jambo lolote/ una ushuhuda na unatamani tuwafahamishe na wengine basi usisite kuwasiliana nasi. Tuandikie kupitia:ushuhudainjili@gmail.com 

Usiache kutufuatilia kupitia facebook na twitter
Roho Mtakatifu akubariki.
--------------------------------------------

Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia

No comments:

Post a Comment

NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.