Vichwa vya Habari

NGUVU YA SADAKA NA UFUFUO

Mchungaji Emannuel Mchembe wa Kanisa la AICT Kigamboni
Mpendwa katika Kristo,
Katika kitabu cha matendo ya mitume, kuna fungu linalosomeka hivi:
"Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu. Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.  Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.  Akampa mkono, akamwinua; hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai" - Matendo 9:36-41
Ndugu zangu kwenye sadaka kuna nguvu kubwa sana. Wakristo wengi hawajui tu thamani ya sadaka. Ulishawahi kujiuliza kwanini wanasiasa wanapenda sana kutoa? Unadhani ni wajinga? Kama unataka kupendwa na watu wewe wape vitu!

Lakini huwa najiuliza mara nyingi kwani wakristo tumefumbwa wapi? Kwanini walio gizani ni watoaji wakubwa? Ulishawahi kumuona au kusikia mtu kaenda kwa karumanzila halafu asimtolee huyo 'mungu' aliyemuendea? 

Kikawaida kuna vitu viwili muhimu sana katika utoaji wao hawa walio gizani:

Kwanza ni damu. Siku zote hawa watu huambiwa kutoa damu. Aidha ni damu ya mwanadamu, au hata ya mnyama. Na tangu agano la kale imeandikwa '...karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo". 

Ashukuriwe Bwana Yesu maana alimwaga damu yake pale msalabani kwa ajili ya wote tupate kuokolewa"

Pili ni sadaka. Damu hiyo huambatana na sadaka. Inaweza ikawa fedha au hicho kitakachotolewa damu!

Wana wa giza wamekuwa na hekima kuliko wana wa nuru. 

Mungu atusaidie sana.

Thabitha alifufuliwa kwa sababu ya nguvu ya sadaka ambazo alikuwa akiwapa watu. Watu waliomboleza kwa sababu ya kifo chake wakikumbuka sadaka ambazo alikuwa akiwapa. Kwanini Yesu asibadilishe kifo chake? Yesu alibatilisha hati yake ya kifo na kumfufua maana yeye ni ufufuo, kweli na uzima.
Ndugu jifunze kumtolea Mungu. Sadaka yako itafufua mambo yaliyokufa. 
Sadaka zina nguvu.

Usiache kutufuatilia kwenye facebook hapa au kwenye twitter hapa.

Kama una maoni usisite kutuachia maoni yako hapa au kushare neno hili katika mitandao ya kijamii. Kama una jambo lolote la kutushirikisha basi tutumie kupitia ushuhudainjili@gmail.com

NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.