Jibu: Mungu ni mkubwa kuliko sisi na tusitarajie kumuelewa katika kila jambo. Utatu ni jambo gumu kulieleza kwa kina. Hakuna mwanadamu anayeweza kulielewa kwa undani zaidi. Biblia inafundisha kuwa Baba ni Mungu, ya kuwa Yesu ni Mungu na pia Roho mtakatifu ni Mungu. Biblia pia inafundisha kuna Mungu mmoja tu. Ijapokuwa tunaweza kufahamu uhusiano tofauti tofauti wa sehemu za utatu huu ni vigumu kuelewa kwa akili ya kibinadamu. Hii haimaanishi kuwa si kweli au si maagizo ya Biblia.
Utatu ni Mungu mmoja katika nafsi tatu. Aya za biblia zifuatazo
zitatumika kufafanua neno hili.
1) Kuna Mungu mmoja: kumbukumbu la torati 6:4; wakorintho wa kwanza
8:4; wagalatia 3:20; Timotheo wa kwanza 2:5.
2) utatu una nafsi tatu: mwanzo 1:1; 1:26; 3:22; 11:7 Isaya 6:8;
48:16; 61:1; Mathayo 3:16-17; Mathayo 28:19; wakorintho wa pili 13;14. Katika
mwanzo 1:1 neno la wingi “Elohim” linatumika. Katika mwanzo 1:26; 3:22; 11:7 na
Isaya 6:8, neno la wingi “sisi” limetumika. Kwa hivyo neno “Elohim’ na “sisi”
kumaanisha zaidi ya mmoja halina pingamizi.
Katika Isaya 48:16 na 61:1, Mwana azungumza huku akihusisha Baba na
Roho Mtakatifu. Fananisha Isaya 61:1na Luka 4:14-19 kuona Mwana akizungumza.
Mathayo 3:16-17 inaelezea ubatizo wa Yesu. Anayeonekana hapa ni Mungu Roho
mtakatifu akimshukia Mungu Mwanahuku Mungu Baba akitangaza furaha yake katika
Mwana. Mathayo 28:19 na wakorintho wa pili 13:14 ni mifano ya nafsi tatu katika
Mungu mmoja.
3) Nafsi hizi tatu zinatambulika katika maandiko. Katika agano la kale
“ BWANA” linatofautishwa na “Bwana” (mwanzo 19:24; Hosea 1:4). “BWANA” ana
“Mwana” (zaburi 2:7, 12; Methali 30:2-4). Roho anatofautishwa na “BWANA”
(hesabu 27:18) na pia kutoka “Mungu” (zaburi 51:10-12). Mungu mwana
atofautishwa na Mungu Baba (zaburi 45:6-7; waebrania1:8-9). Katika agano jipya,
Yohana 14:16-17 ndipo Yesu anazungumza na Baba juu ya kuleta Msaidizi, Roho
mtakatifu. Hii ina maana ya kuwa Yesu hakujichukulia yeye mwenyewe kuwa Baba
wala Roho Mtakatifu. Katika kila mahali ndani ya agano jipya Yesu alipozungumza
na Mungu Baba alikuwa akizungumza na nafsi moja wapo ya Utatu – Baba.
4) kila nafsi katika utatu huu ni Mungu: Baba ni Mungu: Yohana 6:27;
warumi 1:7; petro wa kwanza 1:2. Mwana ni Mungu: Yohana 1:1, 14; warumi 9:5;
wakolosai 2:9; waebrania 1:8; Yohana wa kwanza 5:20. Roho mtakatifu ni Mungu:
Matendo ya mitume 5:3-4; wakorintho wa kwanza 3:16 (anayedumu ndani ni Roho
mtakatifu –warumi 8:9; Yohana 14:16 –17; Matendo ya mitume 2:1—4).
5) Katika mpangilio ndani ya utatu huu: maandiko yanaonyesha kuwa Roho
Mtakatifu humtumikia Baba na Mwana na Mwana humtumikia Baba. Huu ni uhusiano wa
ushirika wao wala hupunguzi uungu wa nafsi yoyote ile. Kuhusu Mwana tazama:
luka 22:42; Yohana 5:36; Yohana 20:21; Yohana wa kwanza 4:14. kuhusu Roho
Mtakatifu tazama Yohana 14:16; 14:26; 15:26; 16:7 na hasa Yohana 16:13-14.
6) Majukumu ya kila nafsi katika utatu: Baba ndiye aliyesababisha
kuwako kwa 1) ulimwengu (wakorintho wa kwanza 8:6; Ufunuo wa Yohana 4:11), 2)
ufunuo wa kimungu (Ufunuo wa Yohana 1:1) 3)wokovu (Yohana 3:16-17); Matendo ya
kibinadamu ya Yesu ( Yohana 5:17; 14:10). Baba anaonekana kwanza katika haya
yote.
Mwana ni wakala ambaye Baba humtumia kufanyia haya: 1) Kuumba na
kustawisha ulimwengu (wakorintho wa kwanza 8:6; Yohana 1:3; wakolosai 1:16-17);
2) ufunuo wa kimungu (Yohana 1:1; Mathayo 11:27; Yohana 16:12-15; Ufunuo wa
Yohana 1:1); na 3) wokovu ( wakorintho wa pili 5:19; Mathayo 1:21; Yohana
4:42). Baba alifanya mambo haya yote kupitia Mwana anayetenda kazi kama
mwakilishi wake.
Roho Mtakatifu ndiye anayetumiwa na Baba kufanya haya: 1) uumbaji na
ustawishaji wa ulimwengu (mwanzo 1:2; Ayubu 26:13; zaburi 104: 30); 2) ufunuo
wa kimungu (Yohana 16:12-15; waefeso 3:5; petro wa pili 1:21); 3) wokovu
(Yohana 3:6; Tito 3:5; petro wa kwanza 1;2); na 4) matendo ya Yesu ( Isaya
61:1; Matendo ya mitume 10;38). Haya yote Baba ayatenda kupitia Roho Mtakatifu.
Baba, Mwana na Roho si vipande vya Mungu bali kila nafsi ni Mungu.
Mungu asiyeonekana na macho hawezi kuelezwa kwa usahihi na mwenye kuona na
macho ya kibinadamu akaeleweka. Lakini katika hali zote tazama Mungu kama nafsi
tatu zisizogawanyika kuwa Miungu mitatu bali Mungu mmoja tu. “jinsi zilivyo kuu
utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia
zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana?” 9 warumi 11:33-34)
No comments:
Post a Comment