Dhambi Ni Nini?
“Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa
watu na dhambi zao,” Mat. 1:21.
Dhambi Ni Nini?
“...Dhambi ni Uasi”
“Kila atendaye dhambi, anafanya uasi, kwa kuwa dhambi ni uasi,” 1 Yoh. 3:4. “Kila lisilo haki
ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti,” 1 Yoh. 5:17. Dhambi isiyo ya mauti ni ile ambayo
mtu ametubu, yaani ameiacha kabisa kuitenda. Hakuna dhambi ndogo wala kubwa; ikiwa ni
ndogo au kubwa hajaitubia au haachi kuifanya itakupeleka Jehanamu ukateseke milele.
Je, Wote Wametenda Dhambi?
“Kwa sababu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu,” Rum. 3:23.
Matokeo Ya Dhambi Ni Nini?
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.....” Rum. 6:23. “Kwa hiyo kama mtu mmoja dhambi
iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti, na hiyo mauti ikawafikia watu wote kwa
sababu wote wamefanya dhambi,” Rum. 5:12. “Lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na
Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia,” Isa. 59:2.
Tunaitambuaje Dhambi?
“Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile
ahadi kwa imani ya Yesu Kristo,” Gal. 3:22. “Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha!
Walakini nisingelijua dhambi ila kwa sheria; nisingelijua kutamnani kama torati isingelisema,
usitamani,” Rum. 7:7.
Tufanyeje Kuhusu Dhambi?
“Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala
haiwezi kuitii,” Rum. 8:7.
Ni Nini Mungu Alichofanya?
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili
yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi,” Rum. 5:8. “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu
katika mwili wake juu ya mti, ili tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya
haki na kupigwa kwake tumeponywa,” 1 Pet. 2:24. “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja
kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki ili atulete kwa Mungu, mwili wake
ukauawa, bali Roho yake ikahuishwa,” 1 Pet. 3:18. “Yaani Mungu alikuwa ndani ya Kristo,
akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno
la upatanisho,” 2 Kor. 5:19. “Hili ndilo pendo, sio kwamba sisi tumempenda Mungu, bali
kwamba yeye alitupenda sisi, hata akamtuma Mwanawe kuwa upatanisho kwa dhambi
zetu....Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani
yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu,” 1 Yoh. 4:10-12.
Yatupasa Tufanye Nini?
“Amini...tubu” (geuka akilini mwako na umrudie Mungu). “Basi nyumba yote ya Israeli na
wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.
Walipoyasikia hayo wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine;
tutendeje ndugu zetu? Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu
Kristo mpate ondoleo la dhambi....” Mdo. 2:36-38. “Huyo manabii wote humshuhudia, ya
kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi, “ Mdo. 10:43.
Nini Kinachofuata Baada Ya Msamaha Wa Mungu?
“Sasa, basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya
Roho wa uzima ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti,”
Rum. 8:12.
Ikiwa unataka usamehewe dhambi zako na Mungu, hakuna njia nyingie yakufanya isipokuwa ni
ile tu iliyoamuriwa na Mungu mwenyewe katika Injili ya Kristo: amini, tubu dhambi zako, mkiri
Yesu kwa kinywa chako kwamba ni Mwana wa Mungu aliye hai, kisha ubatizwe ili upate
msamaha wa dhambi zako, Mk. 16:15-16. Na iwapo unataka kufanya hivyo, fika au tuandikie
kwa anuani zifuatazo nasi tutajitahidi kukusaidia ili ufanye mambo hayo ambayo hata sisi
tuliyafanya kama Bwana alivyoamuru kwa ajili ya uzima wa milele wa roho zetu.
Kanisa La Kristo
(Rum. 16:16)
Out source
No comments:
Post a Comment