Vichwa vya Habari

Huduma Ya Yesu Ya Kuponya



Huduma Ya Yesu Ya Kuponya 

Mara nyingi imedhaniwa kwamba, kwa kuwa Yesu alikuwa Mwana wa Mungu, alikuwa na uwezo wa kufanya muujiza au kumponya mtu wakati wowote ambao Angetaka. Lakini tunapochunguza Maandiko kwa makini, tunagundua kwamba hata ingawa Yesu kweli alikuwa Mungu, ni kama alikuwa amejiwekea mipaka wakati wa huduma Yake hapa duniani. Aliwahi kusema hivi: “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda” (Yohana 5:19). Hii inaonyesha dhahiri kabisa kwamba Yesu alikuwa na mipaka, na alikuwa anamtegemea Baba Yake.
Kulingana na maelezo ya Paulo ni kwamba, wakati Yesu alipofanyika mwanadamu “alijipunguzia Mwenyewe” mambo fulani ambayo alikuwa na haki nayo kama Mungu. Tunasoma hivi:
Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu (Wafilipi 2:5-7. Maneno mepesi kutilia mkazo).
Je, Yesu “alijipunguzia” nini? Si uungu Wake, wala si utakatifu Wake, wala si upendo Wake. Bila shaka ni nguvu Zake kama Mungu. Ni wazi kwamba hakuwepo kila mahali, tena, hakujua kila kitu, na hakuwa na nguvu zote. Yesu alifanyika mwanadamu. Katika huduma Yake, alifanya huduma kama mtu aliye na upako wa Roho Mtakatifu. Hili linakuwa dhahiri tunapotazama kwa makini zile Injili nne.
Kwa mfano – hebu tuulize hivi: Kama Yesu alikuwa Mwana wa Mungu, mbona ilikuwa lazima Kwake kubatizwa kwa Roho Mtakatifu alipoanza huduma akiwa na umri wa miaka thelathini? Kwa nini Munguajazwe Mungu?
Ni dhahiri kwamba Yesu alihitaji ubatizo wa Roho Mtakatifu ili aweze kupata upako kwa ajili ya huduma. Hii ndiyo sababu mara tu baada ya kubatizwa Kwake, tunasoma habari Zake akihubiri maneno haya: “Roho wa Bwana yu juu yangu, maana amenitia mafuta nihubiri … niwatangazie … niwaweke huru …” (Luka 4:18. Maneno mepesi kutilia mkazo).
Ndiyo sababu pia Petro alihubiri hivi: “Habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu, naye akazunguka huko na huko akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi, kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye” (Matendo 10:38. Maneno mepesi kutilia mkazo).
Vile vile, ndiyo sababu Yesu hakufanya miujiza yoyote mpaka alipobatizwa kwa Roho Mtakatifu, alipokuwa na umri wa miaka thelathini. Je, alipokuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alikuwa Mwana wa Mungu? Ndiyo – bila shaka. Sasa basi, kwa nini hakufanya miujiza yoyote mpaka alipotimiza miaka thelathini? Kwa sababu Yesu “alijipunguzia Mwenyewe” nguvu zisizo za kawaida ambazo Mungu anakuwa nazo, na ilibidi asubiri mpaka wakati wa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu.

Uthibitisho Zaidi Kwamba Yesu Alifanya Huduma Kama Mtu Mwenye Upako Wa Roho

Tunaposoma Injili tunagundua kwamba kuna nyakati ambapo Yesu alikuwa na maarifa ya kiMungu, na wakati mwingine hakuwa nayo. Ukweli ni kwamba mara nyingi, Yesu aliuliza maswali ili kupata habari.
Kwa mfani: Alimwambia yule mwanamke Msamaria kisimani kwamba aliwahi kuwa na wanaume watano, na kwa wakati huo alikuwa anaishi na mtu ambaye hakuwa mume wake (o0na Yohana 4:17, 18). Je, Yesu alijuaje hayo? Je, ni kwa sababu alikuwa Mungu, na Mungu anajua kila kitu? Hapana, maana ingekuwa hivyo, angefanya hivyo wakati wote. Ingawa alikuwa Mungu na Mungu anajua kila kitu, Yesu “alijipunguzia Mwenyewe” uwezo Wake wa kujua kila kitu alipofanyika mwanadamu. Yesu alijua habari za ndoa ya mwanamke huyo kisimani kwa sababu Roho Mtakatifu alimpa wakati huo karama ya “neno la maarifa” (1Wakor. 12:8), ambalo ni uwezo wa kiMungu kujua kitu kuhusu wakati uliopo, au wakati uliopita. (Tutajifunza kwa upana zaidi mada ya karama za Roho katika sura ifuatayo).
Je, Yesu alijua kila kitu kila wakati? Hapana. Wakati mwanamke aliyekuwa anatokwa damu alipogusa pindo la vazi Lake na akajisikia nguvu za kuponya zikimtoka, aliuliza hivi: “Nani aliyenigusa mavazi yangu?” (Marko 5:30b). Wakati mwingine, Yesu alipoona mtini kwa mbali katika Marko 11:13, “alikwenda ili aone kama atapata kitu (tunda) kwake”.
Mbona Yesu hakumjua aliyemgusa? Mbona hakujua kama mtini ule ulikuwa na matunda? Kwa sababu alikuwa anatenda kazi kama mtu mwenye upako wa Roho Mtakatifu, aliye na karama za Roho. Karama za Roho hufanya kazi kadiri Roho apendavyo (ona 1Wakor. 12:11; Webr. 2:4). Yesu hakujua mambo kimuujiza kama wakati huo Roho Mtakatifu hakumpa karama ya “neno la maarifa”.
Ndivyo ilviyokuwa hata kuhusu huduma Yake ya kuponya. Maandiko yanaweka wazi kabisa kwamba Yesu hakuweza kumponya kila mtu kila wakati. Kwa mfano: Tunasoma katika Injili ya Marko kwamba, alipotembelea mji wa kwao wa Nazareti, hakuweza kufanya kila kitu alichotaka.
Akatoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao; wanafunzi wake wakamfuata. Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si yule seremala mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake. Wala hakuweza kufanya mwujiza wowote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao (Marko 6:1 – 6. Maneno mepesi kutilia mkazo).
Ona kwamba Marko hasemi Yesu alikataa kufanya muujiza wowote huko. Anasema, hakuweza. Kwa nini? Kwa sababu watu wa Nazareti walikuwa hawaamini. Hawakumpokea Yesu kama Mwana wa Mungu mwenye upako, bali kama mtoto wa seremala wa pale, sawa tu na jinsi Yesu Mwenyewe alivyosema, kwamba “Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake” (Marko 6:4). Matokeo yake ni kwamba alichoweza kufanya sana ni kuwaponya watu wachache tu, “wenye maradhi madogo madogo” (kama inavyosema tafsiri nyingine ya Biblia). Hakika – kama kuna mahali popote ambapo Yesu angependa kufanya miujiza mikubwa na kuwaponya watu sana, ingekuwa ni katika mji wa kwao nyumbani – mahali alipoishi muda mrefu wa maisha Yake. Lakini Biblia inasema, hakuweza.

Maelezo Zaidi Kutoka Kwa Luka

Kimsingi, Yesu aliponya kwa njia mbili tofauti: (1) Kwa kufundisha Neno la Mungu ili kuwatia moyo wagonjwa wawe na imani ya kuponywa, na (2) Kwa kufanya kazi katika “karama za kuponya”, kadiri Roho Mtakatifu alivyopenda. Basi, katika huduma Yake ya kuponya, Yesu alikuwa na mipaka aina mbili: (1) Kutokuamini kwa wagonjwa, na (2) Mapenzi ya Roho Mtakatifu kutaka kujidhihirisha kupitia “karama za kuponya”.
Ni dhahiri kwamba idadi kubwa ya wakazi wa mjini kwao Yesu hawakuwa na imani Naye. Ingawa walikuwa wamesikia juu ya miujiza Yake ya uponyaji katika miji mingine, hawakuamini kwamba alikuwa na nguvu za kuponya, na kwa sababu hiyo, Yeye asingeweza kuwaponya. Tena, inaonekana kwamba Roho Mtakatifu hakumpa Yesu “karama za kuponya” zozote zile alipokuwa Nazareti – na hakuna awezaye kuju7a sababu yake.
Luka anaeleza zaidi kuliko Marko, mambo yaliyotokea wakati Yesu alipofanya ziara huko Nazareti. Ni hivi:
Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifngua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa: Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kuutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga chuo…Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. Wakamshuhudia wote wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?( Luka 4:16 – 22).
Yesu alitaka wasikilizaji Wake waamini kwamba Yeye ndiye mtiwa mafuta aliyeahidiwa katika unabii wa Isaya, akitumaini kwamba wangeamini na kupokea faida zote za upako Wake ambazo, kulingana na Isaya, ni pamoja na uhuru kutoka utumwani na kufungwa, pamoja na kuona kwa vipofu.[1] Lakini, hawakuamini, na ingawa walipendezwa na kuvutiwa na uwezo Wake wa kuzungumza, hawakuweza kuamini kwamba mwana wa Yusufu alikuwa mtu maalum. Akitambua kutokuamini kwao, Yesu alijibu hivi:
Hapana shaka mtaniambia mitahli hii, Tabibu, jiponye nafsi yako. Mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe … Amin nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe (Luka 4:23, 24).
Watu katika mji wa nyumbani kwao Yesu walikuwa wanangojea kuona kama angefanya yale waliyokuwa wamesikia ameyafanya huko Kapernaumu. Moyoni, hawakuwa na hali ya kutarajia ka imani, bali ya mashaka. Kukosa kwao imani kulimzuia Yeye asifanye miujiza yoyote, wala asiponye magonjwa makubwa.

Kingine Kilichomzuia Yesu Huko Nazareti

Maneno ya Yesu yaliyofuata, aliyowaambia watu wa Nazareti yanadhihirisha pia kwamba alikuwa amezuiwa na mapenzi ya Roho Mtakatifu, kujidhihirisha Mwenyewe kwa njia ya “karama za kuponya”. Anasema hivi:
Lakini kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu (Luka 4:25 – 27).
Hoja ya Yesu ni kwamba Eliya asingeweza kuongeza mafuta na unga ili kumtunza mjane yeyote aliyetaka yeye katika kipindi cha miaka mitatu cha ukame huko Israeli (ona 1Waf. 17:9-16). Ingawa walikuwepo wajane wengi tu wenye kuteseka huko Israeli, Roho alimpaka mafuta Eliya kwenda kumaidia mjane mmoja tu ambaye wala hakuwa Mwisraeli. Vivyo hivyo, Elisha asingeweza kumtakasa mkoma yeyote aliyetaka yeye. Hii ilithibitishwa kwa ukweli kwamba walikuwepo wakoma wengi tu Israeli wakati Naamani anatakaswa. Kama ingekuwa ni uchaguzi wake, bila shaka Elisha angewatakasa Waisraeli wenzake waliokuwa wakoma, kabla ya kumtakasa Naamani, aliyekuwa mwabudu sanamu (ona 2Waf. 5:1-14).
Eliya na Elisha walikuwa manabii – watu waliopakwa mafuta na Roho Mtakatifu, waliotumiwa kwa karama mbalimbali za Roho, kama alivyopenda Mwenyewe. Mbona Mungu hakumtuma Eliya kwa wajane wengine? Hatujui. Mbona Mungu hakumtumia Elisha kuwaponya wenye ukoma wengine? Hatujui. Hakuna ajuaye isipokuwa Mungu.
Hata hivyo, hizo hadithi mbili maarufu sana za Agano la Kale hazithibitishi kwamba hayakuwa mapenzi ya Mungu kuwapa wajane wote mahitaji yao au kumponya kila mwenye ukoma. Watu wa Israeli wangeweza kukomesha njaa yao katika wakati wa Eliya kama wao na mfalme wao mwovu (Ahabu) wangetubia dhambi zao. Njaa ilikuwa ni aina ya adhabu ya Mungu. Na, wakoma wote wa Israeli wangeweza kuponywa kwa kutii na kuamini maneno ya agano lao kutoka kwa Mungu, ambalo, kama tulivyokwisha ona mapema, lilihusisha uponyaji wa mwili.
Yesu aliwafunuliwa wasikilizaji Wake pale Nazareti kwamba alikuwa chini ya mipaka hiyo hiyo kama Eliya na Elisha. Kwa sababu fulani, Roho Mtakatifu hakumpa Yesu “karama za kuponya” aina yoyote ile huko Nazareti. Hilo, pamoja na kutokuamini kwa watu wa Nazareti, vilisababisha isitendeke miujiza yoyote mikubwa katika mji wa kwao Yesu.

Tutazame Yesu Akitumia “Karama Ya Kuponya” Katika Tukio Moja

Tunapojifunza maelezo ya Injili kuhusu uponyaji aina mbalimbali uliofanywa na Yesu, tunagundua kwamba sehemu kubwa ya watu waliponywa, si kwa sababu ya “karama za kuponya” bali kwa sababu ya imani yao. Hebu tufikiri kidogo juu ya tofauti kati ya uponyaji wa aina mbili huo, kwa kutazama mifano. Kwanza tutajifunza habari za yule mtu aliyepooza aliyekuwepo katika Birika la Betzatha ambaye, hakuponywa kwa sababu ya imani yake, bali kwa kupitia “karama ya kuponya” ya Yesu.
Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Betzatha, nayo ina matao matano. Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke. Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.] Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda (Yohana 5:2 – 9).
Tunajuaje kwamba mtu huyu aliponywa kwa njia ya “karama ya kuponya” na si imani yake? Sababu ziko kadha.
Kwanza – ona kwamba mtu huyu hakuwa anamtafuta Yesu. Badala yake, yesu alimkuta ameketi kando ya birika. Kama mtu huyo angekuwa anamtafuta Yesu, hiyo ingekuwa ishara kwamba ana imani kwa sehemu fulani.
Pili – Yesu hakumwambia huyo mtu kwamba imani yake imemponya, kama alivyokuwa na kawaida ya kufanya mara nyingi alipowaponya watu.
Tatu – wakati huyo mponywa alipohojiwa baadaye na Wayahudi kwamba nani amemwambia “simama uende”, alijibu kwamba wala hakumjua. Kwa hiyo, ni hakika kabisa kwamba si imani yake katika Yesu iliyosababisha uponyaji huo. Hapa ni mtu aliyeponywa kwa njia ya “karama ya kuponywa” iliyodhihirishwa kama Roho Mtakatifu alivyopenda.
Ona pia kwamba ingawa walikuwepo watu wengi wagonjwa waliokuwa wanasubiri maji yatibuliwe, Yesu alimponya mtu mmoja tu, akawaacha wengine wengi tu wakiwa wagonjwa. Kwa nini? Hapo tena hatuna jibu. Lakini tena, hii si uthibitisho kwamba ni mapenzi ya Mungu kwa watu wengine kubakia wagonjwa. Yeyote na wote katika hao wagonjwa wangeweza kuponywa kwa njia ya kumwamini Yesu. Labda hiyo ndiyo sababu ya huyo mtu mmoja tu kuponywa – ili kuwafanya watu wavutwe kwa Yesu – Yule ambaye angewza kuwaponya, kama tu wangeamini.
Mara nyingi, “karama za kuponya” huangukia katika fungu la “ishara na maajabu”. Yaani, miujiza iliyokusudiwa kuwafanya watu wavutwe kwa Yesu. Hii ndiyo sababu wainjilisti wa Agano Jipya kama Filipo waliwezeshwa kuwa na “karama za kuponya” za aina mbalimbali, kwa sababu miujiza waliyofanya iliwavuta watu waisikilize Injili iliyokuwa ikihubiriwa (ona Matendo 8:5-8).
Wakristo wagonjwa wasingoje mpaka mtu mwenye “karama za kuponya” aje walipo ili kuponywa maana, mtu wa aina hiyo na mwenye karama hiyo anaweza asitokee. Uponyaji unapatikana kwa imani katika Yesu, na hata ingaa si kila mtu atakayueponywa kupitia karama za kuponywa, kila mtua naweza kuponywa kupitia imani yake. Karama za kuponywa zimewekwa kanisani kwa kusudi la kuwaponya wasioamini, na ili watu wavutwe kusikiliza Injili. Hii haimaanishi kwamba Wakristo hawatakaa waponywe kwa njia ya karama za kuponywa. Ila ni kwamba, Mungu anawatazamia watoto Wake wapokee uponyaji kwa imani.

Mfano Wa Mtu Kuponywa Kwa Imani yake

Batimayo alikuwa kipofu aliyeponywa kwa imani yake kwa Yesu. Tusome habari zake katika Injili ya Marko, kama ifuatavyo:
Wakafika Yeriko. Hata alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko pamoja na wanafunzi wake na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando yanjia. Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu. Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupata zaudi, Mwana wa Daudi, unirehemu. Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo! Inuka, anakuita. Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu. Yesu akamjibu akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu! Nataka nipate kuona. Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani (Marko 10:46 – 52).
Kwanza – ona kwamba Yesu hakumtafuta Batimayo. (Hii ni kinyume kabisa na mambo ya pale Betzata.) Ukweli ni kwamba Yesu alikuwa anampita, na kama Batimayo asingepaza sauti, Yesu angeendelea kutembea na angepita. Maana yake ni kwamba Batimayo asingeponywa.
Fikiri kidogo juu ya hilo. Ingekuwaje kama Batimayo aneketi hapo na kujiambia hivi: “Kama ni mapenzi ya Yesu mimi niponywe, atakuja nilipo, aniponye”? Nini kingetokea? Batimayo asingeponywa kamwe, ingawa habari hii inaonyesha kwamba yalikuwa mapenzi ya Yesu aponywe. Ishara ya kwanza kwamba Batimayo alikuwa na imani ni kwamba alimpazia Yesu sauti.
Pili – ona kwamba Batimayo hakukubali kukatishwa tamaa na wale waliokuwa wanajaribu kumnyamazisha. Watu walipojaribu kumyamazisha, “alizidi kupiga kelele” (Marko 10:48). Hiyo inaonyesha imani yake.
Tatu – ona kwamba Yesu hakuitikia kilio cha Batimayo mwanzoni. Inawezekana kwamba pengine alikuwa hasikii, lakini kama alisikia, Yesu hakuitika. Yaani, aliruhusu imani ya mtu huyo ipimwe.
Kama Batimayo angekata tamaa baada ya kupiga kelele mara moja tu, asingeponywa. Sisi pia lazima wakati mwingine tukaze imani kwa sababu mara nyingi inaonekana ni kana kwamba maombi yetu hayatajibiwa. Hapo ni imani yetu inapimwa. Basi, tunahitaji kudumu kusimama, tukikataa kuvunjwa moyo na mazingira kinyume.

Ishara Zaidi Za Imani Ya Batimayo

Yesu alipomwambia aje, Biblia inasema Batimayo “alitupa vazi lake”. Kwa ufahamu wangu, vipofu wa siku za Yesu walikuwa wanavaa aina fulani ya vazi lililowatambulisha kwa jamii kama vipofu. Kama ndivyo, pengine Batimayo alitupa vazi lake alipoitwa na Yesu kwa sababu aliamini kwamba asingehitaji tena kutambuliwa kama kipofu. Kama ndivyo, imani yake hapo inaonekana tena.
Tena – Batimayo alipotupa vazi lake, Biblia inasema “aliruka” kuonyesha msisimko wake kwa matarajio kwamba kitu kizuri kilikuwa kitatokea kwake. Watu wenye imani ya kuponywa huwa wamesisimka wanapomwomba Mungu awaponye, kwa sababu wanatarajia kupokea kitu.
Ona kwamba Yesu aliipima imani ya Batimayo mara nyingine tena aliposimama mbele Yake. Alimwuliza alitaka nini, na kutokana na itikio la Batimayo, ni wazi kwamba aliamini Yesu angeweza kumponya upofu wake.
Mwisho – Yesu alimwambia imani yake ndiyo ilikuwa imemponya. Kama Batimayo aliweza kuponywa kwa imani, hata mwingine yeyote anaweza, kwa sababu Mungu “hana upendeleo”.

Ili Kujifunza Zaidi

Yafuatayo ni maelezo kuhusu uponyaji mara ishirini na moja uliofanywa na Yesu, kama tupatavyo katika zile Injili nne. Yesu aliponya watu wengi zaidi ya ishirini na moja, lakini katika haya yote tunajua mambo muhimu kuhusu mgonjwa husika na jinsi alivyoponywa.
Orodha yenyewe imegawanywa katika makundi makubwa mawili – walioponywa kwa imani na wale walioponywa kwa njia ya karama za kuponywa. Mara nyingi itaonekana kwamba, watu walipoponywa kwa imani zao, Yesu aliwaambia wanyamaze kuhusu uponyaji huo. Hii inazidi kuonyesha kwamba hizo hazikuwa “karama za kuponya” kwa sababu wagonjwa hawakuponywa ili kumtangaza Yesu, au Injili.

Nyakati Ambapo Imani Au Kuamini Hutajwa Kama Sababu Ya Kuponywa:

No comments:

Post a Comment

NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.