Vichwa vya Habari

AINA MBILI ZA KUFUNGA




Somo letu la leo, ni somo la mwisho katika mfululizo wa masomo yahusuyo kufunga.  Ingawa kichwa cha somo letu ni “VIZUIZI VYA NGUVU ITOKANAYO NA KUFUNGA“, hiki kitakuwa ni kimoja kati ya vipengele vitatu tutakavyojifunza katika somo letu la leo:-
(1)      AINA MBILI ZA KUFUNGA;
(2)      KIPINDI CHA KUFUNGA;
(3)      VIZUIZI VYA NGUVU ITOKANAYO NA KUFUNGA.
(1)      AINA MBILI ZA KUFUNGA
Ziko aina mbili za kufunga ambazo kila mtu aliyeokoka anapaswa kuzishiriki:-
  1. KUFUNGA KUTOKANA NA MBIU YA KUFUNGA – (2 NYAKATI 20:3-4; YONA 3:7-8; EZRA 8:21).  
Huku ni kufunga kunakotokana na mbiu ya kufunga inayoletwa kwetu tufunge kwa siku kadha kwa ajili ya jambo fulani na kisha kukutana mahali fulani kwa ajili ya kilele cha maombi, hiyo ni mbiu ya kufunga.  Mbiu ya kufunga inaweza kutangazwa na Kiongozi wa Zoni, Kiongozi wa Kanisa la Nyumbani, Kiongozi wa Kikosi Maalum cha Maombi (Powerhouse), Kiongozi wa Kwaya n.k; na kiongozi huyo ataeleza makusudi ya kufunga huko.  Mbiu ya kufunga, huleta baraka kubwa kwa jinsi inavyojumuisha watu wengi kwa pamoja, wanaopatana kwa nia moja, katika kipindi kimoja, kuombea mambo fulani maalum.
  1. 2.     KUFUNGA KWA UAMUZI WA BINAFSI (NEHEMIA 1:4)
Katika maisha ya mtu aliyeokoka, mtu hujipangia binafsi vipindi vya kufunga na kuomba ili achote baraka zitokanazo na kufunga.  Kama kila mmoja anavyopasa kujipangia binafsi muda wake wa maombi bila kungojea maombi ya pamoja tu kanisani, vivyo hivyo, inampasa kila mmoja wetu kujipangia binafsi vipindi vya kufunga na kuomba, tukiomba kwa ajili ya wenye dhambi wamjue Mungu, kudhihirika kwa miujiza Siku ya Matendo ya Ajabu, tukiomba kwa ajili ya Mchungaji na viongozi wa Kanisa na kazi ya Mungu kwa ujumla katika Kanisa, n.k.
(2)      KIPINDI CHA KUFUNGA
Je tufunge kwa muda gani?  Biblia haiweki sheria juu ya siku ngapi za kufunga.  Hata hivyo, tukiangalia vipindi vilivyotajwa vya mfungo katika Biblia, tutaweza kujifunza mambo kadha.  Mifungo mingi katika Biblia, haitaji siku zilizotumika katika kufunga, lakini hapa tutaangalia ile iliyotajwa siku za mfungo na sababu za kufunga.
NA.ANAYEHUSIKA KUFUNGA

KIPINDI CHA MFUNGO

SABABU ZA KUFUNGA

ANDIKO
1DAUDIAsubuhi hadi Jioni.Kumuombolezea aliyekufa.2 SAMWELI 3:35
2ISRAELIAsubuhi hadi Jioni.Wakati wa Vita inaendelea kumwuliza Bwana juu ya kushindwa kwao.
WAAMUZI 20:24-27
3DAUDIAsubuhi hadi Jioni.Kumlilia aliyekufa2 SAMWELI 1:12
4YUDASiku moja nzima mchana na Usiku.Kuutafuta uso wa Mungu.NEHEMIA 9:1-4
5YUDASiku nzima.Kuutafuta uso wa Mungu.

YEREMIA 36:6
6FARISAYOSiku nzima mara mbili kwa juma kila wakati.LUKA 18:9-12
7ISRAELISiku nzima.Kumlilia Bwana waokolewe na mkono wa Wafilisti.1 SAMWELI 7:6-14
8ESTA/MORDEKAISiku tatu nzima.Kuutafuta uso wa Mungu ili kutoka katika matatizo.ESTA 4:13-16
9WATU WENGISiku tatu (3).Kumsikiliza Yesu akiwafundisha.MATHAYO 15:32
10PAULOSiku tatu nzima (3).Wakovu na wito wa Paulo.MATENDO 9:9
11DAUDISiku saba (7).Kumwomba Mungu kwa ajili ya mtoto.2 SAM. 12:16-18
12ISRAELISiku saba (7).Kuomboleza kifo cha Sauli na wanawe.1 SAM. 31:13
13PAULO NA WATU 276Siku 14 nzima.Safari iliyojaa misukosuko.MATENDO 27:33,37
14DANIELISiku 21 nzima.Kumwomba Mungu baada ya kufunuliwa Neno.DANIELI 10:1-3
15MUSASiku 40 nzima.Kuketi mbele za Bwana mlimani na pia kuwaombea Waisraeli.KUMBUKUMBU LA TORATI 9:9, 18, 25-29; 10:10

16YOSHUASiku 40 nzima.Mlimani mbele ya Mungu.KUTOKA 24:12-15
17ELIYASiku 40 nzima.Safari ndefu baada ya chakula maalum.1 WAFALME 19:5-8
18YESUSiku 40 nzima.Kujaribiwa nykani kutokana na kuongozwa na Roho.MATHAYO 4:1-2

Kutokana na jedwali hili tunajifunza yafuatayo:-
1.         Kipindi cha kufunga katika kumtafuta Bwana kwa maombi, kinabidi kiwe  siyo chini ya siku moja (saa 24).  Kipindi kifupi chini ya hapo hutumika wakati wa vita inayoendelea ili kuhifadhi nguvu za vita kwa mfano kufunga wakati wa kulihubiri Neno la Mungu au kuhudumu.
2.         Kipindi cha kawaida cha mfungo hufikia siku tatu nzima.  Ni katika uzito usio wa kawaida tunazidisha hapo kwa maongozi ya Roho hata hivyo siku hazizidi saba.
3.         Kufunga zaidi ya siku saba lazima kuambatane na kufunuliwa neno.  Mtu hawezi kufunga siku 40 bila kula na kunywa mpaka kuwe na maongozi DHAHIRI ya Mungu kwake na uwepo wa Mungu na msaada wake maalum (1 WAFALME 19:8).
Mtendakazi mzuri wa Kristo atajipangia ratiba yake na kuwa na moja ya kumi ya siku za mwezi katika kufunga (siku tatu).  Inaweza ikawa siku moja katika wiki mara tatu na siyo mfululizo.
(3)      VIZUIZI VYA NGUVU ITOKANAYO NA KUFUNGA
            1.         NIA YA KUFUNGA (WARUMI 12:2)
Nia ya kufunga ikiwa siyo sawa na neno la Mungu, huzuia kupatikana kwa nguvu itokanayo na kufunga.
2.         KUFUNGA KATIKA DHAMBI (YEREMIA 14:10-12; ISAYA 58:3-5).
3.         KUFUNGA BILA KUOMBA – Kufunga lazima kuambatane na kumtafuta BWANA kwa maombi (2 NYAKATI 20:3-4; EZRA 8:21).
4.         KUFUNGA HAKUPASWI KUCHUKUA NAFASI YA IMANI – Hatupaswi kuwaza KILA jambo haliwezekani mpaka tufunge kwanza.  Pasipo imani ni bure (WAEBRANIA 11:6).  Kufunga kunachochea tu Imani.
- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2015/06/somo-vizuizi-vya-nguvu-itokanayo-na.html#.dpuf

No comments:

Post a Comment

NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.