" Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu.Mara hiyo akasimama mbele yao, akajitwika kile alichokilalia, akaenda zake nyumbani kwake, huku akimtukuza Mungu. "Luka 5:19 &25
Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe...
Kama ulikuwa hufahamu hili kwamba,KAZI YA DAKTARI NI KUTOA TIBA,BALI KAZI YA MUNGU NI KUPONYA,basi leo ufahamu hilo.
Yeye mwenye kutibu hutegemea kuwezeshwa ili atibu.
Bali aponyaye hategemei kuwezeshwa na yeyote yule maana ndani yake kuna UWEZA.
Mungu ni mwenye UWEZA wala si mwenye UWEZO, nasema ni mwenye UWEZA Yeye hategemei kuwezeshwa na yeyote yule.
Yule anayetibu kapewa UWEZO wa kutibu,kama vile mtu aliyepewa mbegu apande,lakini mwenye kuikuza ile mbegu ni Mungu ambaye ndiye mwenye maisha ya mbegu hiyo. Aliyepewa mbegu ni mwenye uwezo,bali Yeye aikuzaye ni mwenye uweza.
Aponyaye ana UWEZA wa kuponya.
Daktari hutumia tiba za kawaida kabisa ambazo hazina uponyaji ingawa tiba hizo zina uwezo wa kutibu tu,Mungu huponya.
Leo nataka nikutangazie kwamba yupo mmoja aponyaye naye ndiye Bwana Yesu Kristo wa Nazareti,Yeye ni zaidi ya madaktari wote.
Ok,
Sikia;
Ipo tofauti kubwa kati ya kuponya na kutibu. Nguvu ya kuponya ipo ndani ya jina la Yesu pekee, bali nguvu ya kutibu ipo mahali popote,maana imeandikwa;
" Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. " Matendo 4:12
Kwa jina la Yesu tunaponywa.
Matibabu hutolewa na madaktari pamoja na wale wote watalaamu wa tiba,BALI UPONYAJI UTOLEWA NA MUNGU MWENYEWE.
Andiko hilo hapo juu,linatufundisha sahihi kabisa ya kwamba uponyaji wetu upo kwa Yesu Kristo. Hao Watu waliomchukua huyo mgonjwa ( Luka 5:17-20) hawakumpeleka kwa madaktari wa kawaida sababu walijua siri moja kwamba madaktari huwawezi kumponya yule aliyepooza bali kama wangempeleka kwa madaktari wangelimtibu kawaida tu,ndiposa wakamsongeza kwa Yesu aponyaye bila pesa yoyote.
Biblia inasema Yesu alipoiona imani yao, alimwambia," Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako. " Bwana Yesu hukumtizama mgonjwa bali aliitizama IMANI yao. Sio kitu cha kawaida kwamba mgonjwa aletwe mbele yako kisha usiangalie ugonjwa bali uone imani yao waliomleta.
Umenielewa hapo?
Yaani Bwana Yesu hakuuona ugonjwa bali aliiona imani yao.
Bwana Yesu, siku zote huiangalia imani wala si udhaifu uliokuwa nao.
sababu Mungu hufanya kazi yake katika misingi ya imani. Ukimuomba Baba wa mbinguni basi sharti uwe na imani maana pasipo imani haiwezekani kumpendeza(,Waebrania 11:6).
Lipo Jambo moja la ziada tujifunzalo siku ya leo kupitia fundisho hili,nalo ni hili;
* DHAMBI NI MLANGO WA MAGONJWA.
Yesu alipomuona mgonjwa mara akamuambia, " Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako. " Yesu alijua siri hii ya kwamba akimsamehe dhambi zake atakuwa amemponya na magonjwa yake.
Na hii ndio kanuni ya upongaji.
* Kusamehewa dhambi kwanza,kisha kuwa mzima.
Mtunga Zaburi ameliweka Jambo hili vizuri kabisa akituambia;
" Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, " Zab.
Katika kusamehewa dhambi kuna uponyaji. Magonjwa uliyonayo ni sababu mlango upo wazi,mlango wa dhambi.
Tazama pale Bwana Yesu alipomponya yule mgonjwa aliyekuwa akisubili maji yatibuliwe,anamwambia hivi;
" Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi. " Yoh.5:14
Bwana Yesu asifiwe...
Jika la Bwana Yesu lipewe sifa...
Tunae Baba atuponyaye,ni Mungu wa huruma asiyefananishwa na chochote kile. Katika andiko letu la msingi (Luka 5:19) wale watu waliompeleka mgonjwa kwa Bwana Yesu ni mfano wa kanisa lenye kupeleka mahitaji yake kwa Bwana Yesu moja kwa moja pasipo kupinda pinda kwa mwingine awaye yote.
Kanisa linahitaji kumtegemea Bwana Yesu moja kwa moja pasipo njia nyingine yoyote ile,na wala kuwategemea mitume. Lakini Biblia inatuambia kwamba watu hawa walipokosa mpenyo wa kumpitisha mgonjwa wao,wakapata akili ya mwisho ya kupanda juu ya dari na kupisha matofali ya juu. Watu hawa wanatufundisha ujasiri unapomtafuta Bwana Yesu. Ujasiri wa kutoogopa macho ya watu.
* Watu waliomchukua mgonjwa wa kupooza wanatuelekeza kwama Yesu pekee ndio aponyaye.
Haleluya...
Nampenda pia huyu aliyekuwa mgonjwa,jinsi Biblia inavyomsimulia kwamba alipoponywa tu,tazama Biblia inasema;
" akaenda zake nyumbani kwake, huku akimtukuza Mungu" Luka 5:25
Mtu huyu alienda zake akimtukuza Mungu. Suala la kumtukuza Mungu na kumshukuru Mungu sio suala linalohitaji kufundishwa,ni suala linalohitaji kutoka rohoni. Ndio maana hatuoni mtu huyu akifundishwa kumtukuza Mungu.
Leo Watu wengi hufundishwa kushukuru,kinyume kabisa na jinsi ipasavyo. Hivi ngoja nikuulize Jambo hili,
Mfano;
Mtu akikupa zawadi,je utafundishwa maneno ya kumshukuru mtu huyo?
Kama jibu hautafundishwa basi,vfrivyo hivyo hutakiwi kufundishwa kumtukuza na kumshukuru Mungu,tanya kama huyu aliyekuwa mgonjwa,maana yeye hakufundishwa kumtukuza Mungu.
Haleluya...
Yesu ndio njia,yeye ni mponyaji.
Leo tunaye Bwana Yesu,U hai; Halisi na atakuponya tu kwa kila udhaifu uliokuwa nao,Bwana atakupigania ukiamini inawezekana.
Kwa huduma ya maombi na maombezi.
Usisite kunipigia kwa namba yangu hii; Mobile: 0655-111149
No comments:
Post a Comment