Vichwa vya Habari

Usiwe MTOTO katika KUMJUA MUNGU


Usiwe MTOTO katika KUMJUA MUNGU


waza makubwa
… Usipoteze muda wako KUMWOMBA MUNGU AKUPE PESA… Bali mwombe MUNGU akupe AKILI, HEKIMA NA UFAHAMU WA KIUNGU ambao utakufanya UONE FURSA ZA KIUCHUMI NA KIFEDHA wakati wengine wote wakiwa WANALIA NA KUILAUMU SERIKALI kwa ugumu wa maisha walionao… Usimwombe Mungu ili uwe MTU MKUU… Hili ni jambo dogo sana, Bali mwombe MUNGU akupe HEKIMA NA UFAHAMU utakaokutofauti
sha na wengine na KUKUWEKA MAHALI PA JUU huku ukiwa na Uhakika wa KUKAA HAPO MAISHA YAKO YOTE, Kama ukifika kwenye KILELE CHA MAFANIKIO kwa HEKIMA NA UFAHAMU WA MUNGU, HAUWEZI KUPOROMOKA TENA… Maana MBINGU NA NCHI vimeumbwa na vinadumu kwa HEKIMA NA UFAHAMU WA MUNGU (Mithali 3:19)… Usipoteze muda kumwomba MUNGU UTAJIRI… Badala yake tumia muda wako KUJUA NI KWA NINI MUNGU HUTUPA NGUVU YA KUPATA UTAJIRI ili usije ukanyongwa na huo utajiri wako au ukageuka kuwa mzigo utakaotafuna AMANI NA FURAHA yako… Kabla MUNGU hajakupa KITU CHOCHOTE KIKUBWA kitakacho kutofautisha na wenzio LAZIMA kwanza AJIRIDHISHE kuhusu UADILIFU wa MOYO WAKO… Ndio maana ni LAZIMA kwanza MTU AOKOKE, abadilishwe, afanywe upya ili aweze kupata ACCESS YA SIRI ZA MUNGU… Kumbuka, “MTU WA ASILI [asiye na Yesu ndani yake] HAWEZI KUYAPOKEA MAMBO YA ROHONI [mambo yatokayo moyoni mwa Mungu] KWA MAANA YATAMBULIKANA KWA JINSI YA ROHONI (1 Wakorintho 2:14)!


NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.