WAEFESO
1
Utangulizi
Paulo aliandika waraka huu akiwa gerezani huko Rumi ili kuwatia moyo waamini wa Asia.Unaposoma kwa
uangalifu waraka huu, ingawa Paulo alifungwa huko Kaisaria, utaona kwamba waraka huu uliandikwa kutoka
Rumi ambako Paulo alikuwa na uhuru wa kuhubiri Injili (Mdo.28).Waraka huu ulikuwa kama mwongozo
uliokusudiwa kwa makanisa kadhaa.Katika maandiko mengine ya zamani neno “huko Efeso” halipo. Zaidi ya
hayo, kwenye waraka huu hakuna salamu za watu binafsi, wala hakuna matatizo maalum au hali maalum ya
kanisa la mahali pamoja inayotajwa. Pia mafundisho yaliyomo ni yenye upana mkubwa.Ingawa kanisa la Efeso
ambako Paulo alihudumu kwa zaidi ya miaka miwili linajumuishwa humo, ni wazi kwamba waraka huu
ulikusudiwa kwa makundi mengine ya kanisa kwa ujumla katika eneo hilo la kijeografia la Efeso, yaani, makanisa
ya jirani.
Katika waraka huu, Paulo anapotaja “Kanisa” ana maana ya “Kanisa la po pote.” Anaeleza kwamba Kanisa
limeanzishwa na Mungu, akiwaelezea mpango wa Mungu wa tangu awali wa kuwaokoa watu Wake kwa njia ya
Kristo. Mpango huu ulikuwako hata kabla ya ulimwengu kuumbwa. Kwa wakati huu, wote wanaomwamini Kristo
wanaokolewa kwa neema. Mwenendo wa mwamini uko kinyume kabisa na ule wa maisha ya kale, akionyesha
maisha ya kiroho kama “maisha katika ulimwengu wa roho”. Ingawa inawapasa watu wa Mungu kupigana vita
kali na nguvu za Shetani (6:12), kanisa linashinda na hatimaye uovu unashindwa.Sisi tunaomwamini Kristo ni
viungo vya mwili Wake, yaani, Kanisa, kwa hiyo tunao uwezo wa kushinda.
Katika sehemu ya mwisho ya waraka huu, Paulo anaeleza juu ya maisha yanayowapasa wakristo kuhusu:
Ndoa, tabia, mwenendo, wazazi na watoto wao pia watumishi na mabwana zao.
Wazo Kuu
Kiini cha ujumbe wa waraka huu ni kwamba: Mpango wa Mungu wa milele wa kuuokoa ulimwengu
unatimizwa kwa njia ya Kristo katika mwili Wake, yaani, Kanisa Lake. Mtu anapoamini, anakuwa ndani ya Kristo
na anapata wokovu na kuwa salama. Mungu aliandaa wokovu huu tangu milele na amempa kila aaminiye
mambo yote anayohitaji katika maisha yake ili aweze kusimama, ila ni wajibu wake kupokea mambo hayo
aliyowekewa tayari. Paulo anamalizia kwa kufafanua mambo ambayo Mungu amewaandalia wale wamwaminio,
kusudi waweze kumshinda Shetani anapowashambulia na baada ya mapambano wawe na ushindi wa kudumu.
Mwandishi
Mwandishi wa waraka huu ni Paulo (1:1).
Tarehe
Waraka huu uliandikwa 60 B.K.wakati wa kifungo cha Paulo cha miaka miwili.
Mahali
Rumi.
Mgawanyo
• Mpango wa Mungu na wokovu wa wote wamwaminio (1:1-2:22)
• Siri ya Injili (3:1-21)
• Maisha ya mkristo duniani (4:1-5:21)
• Jinsi wakristo wapaswavyo kuhusiana (5:22-6:9)
• Kupigana na uovu (6:10-24) WAEFESO
2
Salamu
Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa
mapenzi ya Mungu,
Kwa watakatifu walioko Efeso walio
waaminifu katika Kristo Yesu.
2Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba
yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.
Baraka Za Kiroho Zitokazo Kwa Kristo
3Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu
Yesu Kristo aliyetubariki sisi kwa baraka zote za
rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya
Kristo. 4Kwa maana alituchagua katika Yeye
kabla ya kuumbwa ulimwengu ili tuwe watakatifu
na bila lawama mbele Zake. 5Kwa upendo
alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia
ya Yesu Kristo kwa furaha Yake na mapenzi
Yake mwenyewe. 6Kwa hiyo tunamsifu Mungu
kwa huruma zake kuu alizotumiminia kwa
sababu sisi ni wa Mwanae Mpendwa. 7Katika
Yeye tunao ukombozi kwa njia ya damu Yake,
yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na
wingi wa neema Yake 8aliyotumiminia kwa
wingi, kwa hekima yote na maarifa yote. 9Naye
alitujulisha siri ya mapenzi Yake sawasawa na
uradhi wa mapenzi Yake, ambayo alikusudia
katika Kristo, 10ili yapate kutimizwa katika wakati
mkalimifu utakapowadia, yaani, kuvitia vitu
vyote vya mbinguni na vya duniani pamoja chini
ya kiongozi mmoja, ndiye Krsto.
11Katika Kristo sisi nasi tumepata urithi,
tukiisha kuchaguliwa sawasawa na kusudi la
Mungu, Yeye ambaye hufanya mambo yote
kulingana na mapenzi Yake. 12Ili kwamba, sisi
tuliokuwa wa kwanza kuweka tumaini katika
Kristo, tupate kuishi kwa sifa ya utukufu Wake.
13Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia
Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha
kuamini, ndani yake mlitiwa mhuri, kwa yule
Roho Mtakatifu wa ahadi mliyeahidiwa, 14yeye
ndiye amana ya urithi wetu hadi ukombozi wa
milki yake kuwa sifa ya utukufu Wake.
Shukrani Na Maombi
15Kwa sababu hii tangu niliposikia juu ya
imani yenu katika Bwana Yesu na upendo wenu
kwa watakatifu wote, 16sijaacha kumshukuru
Mungu kwa ajili yenu, nikiwakumbuka katika
maombi yangu. 17Nazidi kumwomba Mungu wa
Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu,
awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili
mpate kumjua zaidi. 18Ninaomba pia kwamba
macho ya mioyo yenu yatiwe nuru ili mpate
kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi wa
utukufu Wake kwa watakatifu 19na uweza Wake
mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi
tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani
yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno 20ambayo
aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu,
akamketisha mkono Wake wa kuume katika
mbingu, 21juu sana kuliko falme zote na
mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina
litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na
katika ule ujao pia. 22Naye Mungu ameweka vitu
vyote viwe chini ya miguu Yake na amemfanya
Yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya
Kanisa, 23ambalo ndilo mwili Wake, ukamilifu
Wake Yeye aliye yote katika yote.
Tumefanywa Kuwa Hai Ndani Ya Kristo
Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika
makosa na dhambi zenu, 2ambazo
mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu
huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga,
yule roho atendaye kazi ndani ya wale wasiotii.
3Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani,
tukifuata tamaa za mwili na mawazo yake. Nasi
kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama
mtu mwingine ye yote. 4Lakini Mungu, kwa
upendo Wake mwingi kwetu sisi, ambaye ni
mwingi wa rehema, 5hata tulipokuwa wafu kwa
ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja
na Kristo Yesu, yaani, mmeokolewa kwa
neema. 6Mungu alitufufua pamoja na Kristo na
kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa
roho katika Kristo Yesu, 7ili katika ule ulimwengu
ujao apate kuonyesha wingi wa neema Yake
isiyopimika, iliyodhihirishwa kwetu kwa wema
Wake ndani ya Kristo Yesu. 8Kwa maana
mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani,
wala hii si kwa matendo yenu mema. Hii ni
zawadi kutoka kwa Mungu, 9si kwa matendo,
mtu awaye yote asije akajisifu. 10Kwa maana
sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa
katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo
mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa
tupate kuishi katika hayo.
Wamoja Katika Kristo
11Kwa hiyo kumbukeni kwamba ninyi ambao
hapo awali mlikuwa watu Mataifa kwa kuzaliwa
mlioitwa, “Wasiotahiriwa” na wale wanaojiita
“Waliotahiriwa,” yaani, tohara (ifanyikayo katika
1
2WAEFESO
3
mwili kwa mikono ya wanadamu), 12kumbukeni
kwamba wakati ule mlikuwa hamna Kristo,
mkiwa wageni katika jumuiya ya watu wa
Mungu, yaani, Israeli na wageni katika lile
agano la ahadi, mliishi duniani mkiwa hamna
tumaini wala Mungu. 13Lakini sasa katika Kristo
Yesu, ninyi ambao hapo kwanza mlikuwa mbali
na Mungu, sasa mmeletwa karibu kwa njia ya
damu ya Kristo.
14Kwa maana Yeye mwenyewe ndiye amani
yetu, aliyetufanya sisi tuliokuwa wawili, yaani,
Wayahudi na watu Mataifa tuwe wamoja kwa
kuvunja kizuizi na kubomoa ule ukuta wa uadui
uliokuwa kati yetu. 15Kwa kuibatilisha ile sheria
pamoja na amri zake na maagizo yake alipoutoa
mwili wake, ili apate kufanya ndani yake mtu
mmoja mpya badala ya hao wawili, hivyo
akifanya amani, 16naye katika mwili huu mmoja
awapatanishe wote wawili na Mungu kwa kupitia
msalaba, ambao kwa huo aliangamiza uadui
wao. 17Alikuja na kuhubiri amani kwenu ninyi
mliokuwa mbali na pia akahubiri amani kwao
waliokuwa karibu. 18Kwa maana kwa kupitia
Kwake, sisi sote tunaweza kumkaribia Baba
katika Roho mmoja.
19Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena wala
wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na
watakatifu na pia jamaa wa nyumbani Mwake
Mungu. 20Mmejengwa juu ya msingi wa mitume
na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ndiye
jiwe kuu la pembeni. 21Ndani Yake jengo lote
limeshikamanishwa pamoja na kusimamishwa ili
kuwa hekalu takatifu katika Bwana. 22Katika
Yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja ili mpate
kuwa makao ambayo Mungu anaishi ndani yake
kwa njia ya Roho Wake.
Huduma ya Paulo kwa Watu Mataifa
Kwa sababu hii, mimi Paulo, nimekuwa
mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu
ninyi watu Mataifa.
2Kwa hakika mmekwisha kusikia kuhusu ile
huduma ya neema ya Mungu niliyopewa kwa
ajili yenu 3na jinsi ile siri ilivyodhihirishwa
kwangu kwa njia ya ufunuo, kama
nilivyotangulia kuandika kwa kifupi. 4Kwa
kusoma haya, basi mtaweza kuelewa ufahamu
wangu katika siri ya Kristo. 5Siri hii
haikudhihirishwa kwa wanadamu katika vizazi
vingine kama vile sasa ilivyodhihirishwa na
Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa
Mungu. 6Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili,
watu Mataifa ni warithi pamoja na Israeli, viungo
vya mwili mmoja na washiriki pamoja wa ahadi
katika Kristo Yesu.
7Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa
cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu
Yake itendayo kazi. 8Ingawa mimi ni mdogo
kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa
watakatifu wote, nilipewa neema hii ili
niwahubirie watu Mataifa kuhusu utajiri
usiopimika ulio ndani ya Kristo na 9kuweka wazi
kwa kila mtu jinsi ile siri iliyokuwa imefichwa kwa
nyakati zote katika Mungu aliyeumba vitu vyote.
10Ili kwa njia ya Kanisa, hekima yote ya Mungu
ipate kujulikana kwa watawala na wenye
mamlaka katika ulimwengu wa roho,
11sawasawa na kusudi Lake la milele katika
Kristo Yesu Bwana wetu. 12Yeye ambaye ndani
Yake na kwa njia ya imani katika Yeye tuweze
kumkaribia Mungu kwa ujasiri na kwa uhuru.
13Kwa hiyo, nawaomba msikate tamaa kwa
sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, hayo ni
utukufu wenu.
Maombi Ya Paulo Kwa Waefeso
14Kwa sababu hii nampigia Baba magoti,
15ambaye kwa Yeye ubaba wote wa kila jamaa
za mbinguni na za duniani unaitwa.
16Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia
nguvu mioyo yenu kwa njia ya Roho Wake kwa
kadri ya utajiri wa utukufu Wake, 17ili kwamba,
Kristo apate kukaa mioyoni mwenu kwa njia ya
imani. Nami ninaomba kwamba ninyi mkiwa
wenye mizizi tena imara katika upendo, 18mwe
na uwezo wa kufahamu pamoja na watakatifu
jinsi ulivyo upana na urefu na kimo na kina
upendo wa Kristo 19na kujua upendo huu
kwamba unapita fahamu, ili mpate kujazwa na
kufikia kipimo cha ukamilifu wa Mungu.
20Basi kwa Yeye awezaye kutenda mambo
ya ajabu yasiyopimika kuliko yote tuyaombayo
au tuyawazayo, kwa kadiri ya uweza Wake ule
utendao kazi ndani yetu, 21Yeye atukuzwe
katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi
vyote, milele na milele. Amen.
Umoja Katika Mwili Wa Kristo
Basi, mimi niliye mfungwa wa Bwana,
nawasihi mwenende kama inavyostahili
wito wenu mlioitiwa. 2Iweni wanyenyekevu
kabisa na wapole, mkiwa wavumilivu,
mkichukuliana kwa upendo. 3Jitahidini
kudumisha umoja wa Roho katika kifungo cha
amani. 4Kuna mwili mmoja na Roho mmoja,
kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja. 5Tena
3
4WAEFESO
4
kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo
mmoja, 6Mungu mmoja ambaye ni Baba wa
wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya
yote.
7Lakini kila mmoja wetu amepewa neema
kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Kristo.
8Kwa hiyo husema,
“Alipopaa juu,
aliteka mateka
akawapa wanadamu vipawa.”
9(Asemapo “Alipaa juu,” maana yake nini
isipokuwa ni kusema pia kwamba Kristo
alishuka pande za chini sana za duniaa? 10Yeye
aliyeshuka ndiye aliyepaa juu sanab, kupita
mbingu zote, ili apate kuvijaza vitu vyote. 11Yeye
ndiye aliyeweka wengine kuwa mitume,
wengine kuwa manabii, wengine kuwa
wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na
wengine kuwa walimu, 12kwa kusudi la
kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za
huduma, ili kwamba mwili wa Kristo upate
kujengwa. 13mpaka sote tutakapoufikia umoja
katika imani na katika kumjua sana Mwana wa
Mungu na kuwa watu wazima kwa kufikia kipimo
cha ukamilifu wa Kristo.
14Ili tusiwe tena watoto wachanga,
tukitupwatupwa huku na huku na kuchukuliwa
na kila upepo wa mafundisho kwa hila za watu,
kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za
udanganyifu. 15Badala yake, tukiambiana kweli
kwa upendo, katika mambo yote tutakua, hata
tumfikie Yeye aliye kichwa, yaani, Kristo.
16Kutoka Kwake, mwili wote huunganishwa na
kushikamanishwa pamoja kwa msaada wa kila
kiungo, hukua na kujijenga wenyewe katika
upendo, wakati kila kiungo kinafanya kazi yake.
Maisha Ya Zamani Na Maisha Mapya
17Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza
katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu
Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo
yao. 18Watu hao akili zao zimetiwa giza na
wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa
sababu ya ujinga wao na ugumu wa mioyo yao.
19Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo
ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu,
wakiendelea kutamani zaidi.
a9 Pande za chini sana za dunia hapa maana yake ni sheol kwa
Kiebrania, yaani, kuzimu
b10 Juu sana hapa ina maana mbingu za mbingu
20Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyomjifunza
Kristo. 21Kama hivyo ndivyo ilivyo, ninyi
mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile
kweli ilivyo katika Yesu. 22Mlifundishwa kuuvua
mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale,
ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu.
23Mfanywe upya roho ya nia zenu, 24mkajivike
utu mpya, ulioumbwa sawa sawa na mfano wa
Mungu katika haki yote na utakatifu.
Kanuni Za Maisha Mapya
25Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na
kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana
sisi sote tu viungo vya mwili mmoja.
26Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua
lisichwe mkiwa bado mmekasirika, 27wala
msimpe ibilisi nafasi. 28Yeye ambaye amekuwa
akiiba, asiibe tena, lakini mtu wa namna hiyo
lazima ajishughulishe, tena afanye kitu kifaacho
kwa mikono yake mwenyewe, ili awe na kitu cha
kuwagawia wahitaji.
29Maneno mabaya yasitoke vinywani
mwenu, bali yale yafaayo kwa ajili ya kuwajenga
wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae
wale wasikiao. 30Wala msimhuzunishe Roho
Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwa huyo mlitiwa
muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi. 31Ondoeni
kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na
masingizio pamoja na kila aina ya uovu. 32Iweni
wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa
ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu
katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Kue
Kwa hiyo, mfuateni Mungu kama watoto
wapendwao, 2Mkiishi maisha ya upendo,
kama vile Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa
ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na
dhabihu kwa Mungu.
nenda Nuruni
3Lakini uasherati, usitajwe miongoni
mwenu, wala uchafu wa aina yo yote, wala
tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili
miongoni mwa watakatifu. 4Wala pasiwepo
mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya
upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake
mshukuruni Mungu. 5Kwa habari ya mambo
haya mjue hakika kwamba: Mwasherati, wala
mtu mwovu, wala mwenye tamaa mbaya, mtu
kama huyo ni mwabudu sanamu, ambaye
kamwe hataurithi Ufalme wa Kristo na wa
Mungu. 6Mtu ye yote na asiwadanganye kwa
maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu
huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu
5WAEFESO
5
ya wale wasiomtii. 7Kwa hiyo, msishirikiane nao.
8Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza,
lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni
kama watoto wa nuru 9(kwa kuwa tunda la nuru
hupatikana katika wema wote, haki na kweli,)
10nanyi tafuteni yale yanayompendeza Bwana.
11Msishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali
yafichueni. 12Kwa maana ni aibu hata kutaja
mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya
sirini. 13Lakini kila kitu kilichowekwa nuruni,
huonekana, 14kwa kuwa nuru ndiyo hufanya kila
kitu kionekane. Hii ndiyo sababu imesemekana:
“Amka, wewe uliyelala,
ufufuke kutoka katika wafu,
naye Kristo atakuangazia.”
15Kwa hiyo iweni waangalifu jinsi
mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima,
bali kama wenye hekima, 16mkiukomboa wakati,
kwa sababu nyakati hizi ni za uovu. 17Kwa hiyo
msiwe wajinga, bali mpate kujua nini yaliyo
mapenzi ya Bwana. 18Pia msilewe kwa
mvivyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali
mjazwe Roho. 19Msemezane ninyi kwa ninyi
kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni,
mkimwimbia na kumsifu Bwana mioyoni mwenu,
20sikuzote mkimshukuru Mungu Baba katika
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo kwa kila jambo.
21Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kwa
heshima kwa ajili ya Kristo.
Mafundisho Kuhusu Wake Na Waume
22Ninyi wake, watiini waume zenu kama
kumtii Bwana. 23Kwa maana mume ni kichwa
cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha
Kanisa,ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni
Mwokozi wake. 24Basi, kama vile Kanisa
linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao
imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo.
25Ninyi waume, wapendeni wake zenu,
kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa
kwa ajili yake 26kusudi alifanye takatifu,
akilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno
lake, 27apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na
doa wala kunyanzi au waa lo lote, bali takatifu
lisilo na hatia. 28Vivyo hivyo imewapasa waume
kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe.
Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake
mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri,
kama Kristo anavyolitunza Kanisa Lake. 30Sisi tu
viungo vya mwili Wake. 31“Kwa sababu hii,
mwanaume atamwacha baba yake na mama
yake, naye ataambatana na mkewe na hawa
wawili watakuwa mwili mmoja.” 32Siri hii ni
kubwa, bali mimi nanena kuhusu Kristo na
Kanisa. 33Hata hivyo, kila mmoja wenu
ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi
yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu
mumewe.
Mafundisho Kuhusu Watoto Na Wazazi
Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika
Bwana, kwa kuwa hili ni jema.
2“Waheshimu baba yako na mama yako,” hii
ndio amri ya kwanza yenye ahadi, 3“upate
baraka na uishi siku nyingi duniani.”
4Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto
wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho
ya Bwana.
Mafundisho Kuhusu Watumwa Na Mabwana
5Ninyi watumwa, watiini hao walio mabwana
zenu hapa duniani kwa heshima na kwa
kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile
mnavyomtii Kristo. 6Watiini, si tu wakati
wakiwaona ili mpate upendeleo wao, bali
mtumike kama watumwa wa Kristo, mkifanya
mapenzi ya Mungu kwa moyo. 7Tumikeni kwa
moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na
si wanadamu. 8Mkijua kwamba Bwana atampa
kila mtu thawabu kwa lo lote jema alilotenda,
kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru.
9Nanyi mabwana, watendeeni watumwa
wenu kwa jinsi iyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa
mnajua ya kwamba Yeye aliye Bwana wenu na
Bwana wao yuko mbinguni, naye hana
upendeleo.
Silaha Za Mungu
10Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika
Bwana na katika uweza wa nguvu Zake. 11Vaeni
silaha zote za Mungu ili kwamba mweze
kuzipinga hila za Shetani. 12Kwa maana
kushindana kwetu si juu ya nyama na damu,
bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa
giza na majeshi ya pepo wabaya katika
ulimwengu wa roho. 13Kwa hiyo vaeni silaha
zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya
uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote,
simameni imara. 14Kwa hiyo simameni imara
mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii
ya haki kifuani, 15nayo miguu yenu ifungiwe
utayari tuupatao kwa Injili ya amani. 16Zaidi ya
haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa
6WAEFESO
6
hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto
ya yule mwovu. 17Vaeni chapeo ya wokovu na
mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la
Mungu. 18Mkiomba kwa Roho sikuzote katika
sala zote na maombi, mkikesha kila wakati
mkiwaombea watakatifu wote.
19Niombeeni na mimi pia, ili kila
nifuanguapo kinywa changu, nipewe maneno ya
kusema, niweze kutangaza siri ya Injili kwa
ujasiri, 20ambayo mimi ni balozi wake katika
vifungo. Ombeni kwamba nipate kuhubiri kwa
ujasiri kama inipasavyo.
Salamu Za Mwisho
21Tikiko aliye ndugu mpendwa na mtumishi
mwaminifu katika Bwana, atawaambia kila kitu
ili pia mpate kujua hali yangu na kile
ninachofanya sasa. 22Ninamtuma kwenu kwa
ajili ya kusudi hili hasa, ili mpate kujua hali zetu
na kuwatia moyo.
23Amani iwe kwa ndugu na pendo pamoja
na imani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana
Yesu Kristo. 24Neema iwe na wote wampendao
Bwana wetu Yesu Kristo kwa pendo wa dhati.
Amen.
MAOMBI KWA AJILI YA KUPATA MWENZI (MUME/MKE)..
-
*Maandiko*: Mithali 8:22, Mithali 10:24, Zaburi 37:5
*VIPENGELE VYA MAOMBI*
- Katika jina la Yesu (x3)
- Baba wa mbinguni, ninatambua rehema na uamini...