Vichwa vya Habari

Dhambi za Ngono na Miungano ya Nafsi / Uponyaji wake toka kwa BWANA YESU

Uponyaji Kutokana na Dhambi za Kingono, Miungano ya Nafsi, na Kutazama kwa Picha/Sinema Za Watu Walio Uchi



Dhambi za Kingono

Hapo mwanzo Mungu alimuumba Adamu na Hawa na akawataka waungane kama mume na mke. “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja” (Mwa. 2:24; angalia pia Marko 10:2-12). Kuwa mwili mmoja kuna maana ya muungano usitenganishwa, kiroho na kimwili. Kilichounganishwa duniani (kupitia kwa muungano wa ngono) kitaunganishwa kiroho mbinguni. Mungu hakukusudia kuweko kwa uhusiano wa kingono nje ya ndoa, na kwamba ndoa ya kwanza ingekuwa ndoa pekee. Paulo anasistiza zaidi, akitufunza kwamba kusudi la Mungu kuhusu uhusiano kati ya mume na mke unaweza kutumiwa kama picha ya kusudi la Mungu kuhusu uhusiano kati ya Yesu na kanisa
(Efe. 5:23). Lakini Mungu aliwapa na (kutupa sisi pia) hiari kuchagua. Kisha Shetani, baba wa uwongo ambaye nia yake ni kupotosha na kuharibu, akaingia uwanjani, na amekuwa akifanya kazi ya kugeuza amri na mapenzi ya Mungu tangu wakati huo wa dhambi ya kwanza katiak Bustani la Edeni. La kusikitisha ni kwamba kuna dhambi nyingi za kingono zinazotendeka katika mwili wa Kristo sawa na zile zinazotendeka nje ya mwili wake. Kwa watu wengi, mafundisho ya Biblia yanaonekana kuwa yasiyofaa au yaliyopitwa na wakati. Siku hizi mambo ambayo watu wanahangaishwa nayo ni hatari za kimwili za kufanya ngono bila kinga, badala ya kuhangaishwa na mambo muhmu ambayo ni hatari za kiroho—ambazo tunazokosa kuziona. Fikiria juu ya maandiko yafuatayo kuhusu somo hili:

1. Kutoka 20:14 inasistiza, “Usizini” (inayohusishwa katika kif. Cha 5, ambayo ni “maovu ya baba zao” yatakayopatilizwa wana wao hata kizazi cha tatu na cha nne). 

2. Methali 6:32 inaonyesha kwamba mtu yeyote anayezini “anaangamiza nafsi yake.” 

3. Malaki 2:13-16 anasema kwamba Bwana aliwaumba kitu kimoja katika mwili na roho (kif. cha. 15). 
4. Mathayo 5:32 inaeleza kwamba mtu anayetoka katika ndoa na kuingia katika ndoa nyingine, anazini (Tazama pia Mat. 19:9). 
5. 1 Wakorintho 3:16 na 6:19 inathibitisha: mwili wetu ni hekali ya Mungu. Uzinzi huchafua hekalu ya Mungu. 
6. 1 Wakorintho 5:1-6, ambapo Paulo anazungumza juu ya uzinzi ndani ya Kanisa. 

7. 1 Wakorintho 6:16-20 inaonyesha inaeleza kwamba dhambi za kingono zinaelezwa katika kundi tofauti: "Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, walw wawili watakuwa mwili mmoja.”Dhambi za kingono humfanya mtu atende dhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe.
 8. Wagalatia 5:21 inasema, “… watu watendao mambo ya jinsi hiyo (dhambi za kingono) hawataurithi ufalme wa Mungu.” 

9. 1 Wathesalonike 4:3-6 tunapewa shauri “epukeni uasherati”—ni dhambi dhidi ya mwili wetu wenyewe. 

10. Galatia 6:8 : Apandaye kwa mwili, katika mwili wake, atavuna uharibifu,



# 04 Uponyaji Kutokana na Dhambi za Ngono na Miungano ya Nafsi 



Katika vifungu visivyopungua 55, Agano Jipya linashutumu “porneia,” neno la Kigriki lenye maana ya “uovu wa kingono.” Uovu wa kingono unaelezewa kama ngono kabla lya ndoa kwa katika ushauri wa Paulo kwa Wakristo ambao hawajaoana (1 Kor. 7:9). Hakuna majadiliano kuhusu iwapo Mungu anazichukulia dhambi za kingono kuwa mbaya sana. Dhambi za kingono ni nambari tatu katika dhambi zinazochukiwa sana, baada ya (1) “msiwe na miungu wengine ila mimi” (Kumbu. 5:7) na (2) mauaji(Kumbu. 5:17). Fahamuni kwamba dhambi hizi hufungua shimo kubwa sana katika ukuta wetu wa kiroho (marejeleo ya somo hili yanaweza kupatikana katika ukurasa wa 2 katika sehemu yenye kichwa hiki, “Uponyaji wa Roho — Utangulizi”). Fikiria pia matokeo 25 ya kuzini (Tazama Meth. 5:4-2, 6:20-25 na 16-22; 2 Sam. 10:12, 11:4-7, 12:1-7 na 13-14). Kulingana na Yeremia 3, Mungu anaiita ibada ya sanamu ya aina yoyote, kuwa ni “kuunganishwa” kwa Mungu mwingine. Anakiita kitendo hiki uasherati wa kiroho. katika kueleza uasherati wa kimwili kama “kuunganishwa pamoja kusikofaa—iwe ni kabla au baada ya ndoa na katika mahusiana ya ngono ya jinsia moja (usenge) au kuhusiana na wanyama kingono,” katika amri ya saba (Kut. 20:14) hii ina maana pana zaidi kuliko kitendo kinachofanyika katika “dhambi ya ngono kati ya mume na mke inayotendwa na watu waliooa/olewa.” Kupitia kwa muungano wa kingono, kuna kuungana kwa roho, nafsi na mwili. Baada ya kitendo cha ngono, miili inaweza kutengana lakini nafsi na roho huwa bado zimeunganishwa pamoja. Kitu fulani katika mwanamume huyo huwa sehemu ya mwanamke huyo, na kitu fulani katika mwanamke huyo huwa sehemu ya mwanamume huyo. Muungano husababisha “muungano wa nafsi” wa kiroho na kimwili kati ya watu hao wawili. Hii ni ndiyo iliyokusudiwa na Mungu atika muungano na ndoa ya kwanza kati ya mume na mke. Jambo la kusikitisha ni kwamba, watu wanapofanya ngono na watu ambao si “mume au mke wake wa kwanza na wa pekee,” hali ya kiroho ya “mwili mmoja” huchanganyika, na mpango kamili wa Mungu kwetu huzuiwa, kama vile mpango wake kwa Adamu na Hawa ulizuiwa. Kinachofungwa duniani hugungwa mbinguni. (Mat. 16:19, 18:18) Tunapoungana kingono na mtu mwingine, sisi huunganishw na mtu huyo kihisia na kiroho. Muungano wa kingono kati ya mume na mke (kama inavyoelezwa katika Mwa. 2:24) huruhusu kule kushiriki pamoja upendo na vipawa vingine vyote kati yao. Muungano wa kingono nje ya mpango wa Mungu kuhusu ndoa (Mwa. 2:24) humfanya mtu apokee mambo yote mabaya kutoka kwa mwenzi wake wa kingono (kama vile roho za giza, kumvutia mtu kwenye mazoea ya tabia mbaya, uovu wote ambao mtu huyo ameupokeakwa ajili ya dhambi zake au dhambi za mababu zake kupitia kwa laana za kizazi, kama ilivyoagizwa katika Kut. 20:5) na matokeo mengine ya dhambi ambazo mwenzi huyo wa ngono aliwahi kutenda (kama vile kujihusisha katika mizungu/ushetani). Kupitia kwa muungano wa kingono, sisi huwa kitu kimoja na roho ya mtu huyo. Hatuungani tu na mtu tuliyehusiana naye kingono, bali pia tunaunganishwa kwa mfano wa mnyororo na kila mtu ambaye amewahi kushirikiana na mtu huyo kingono. Kufanya ngono nje ya ndoa ni kuuvunjia heshima uumbaji wa Mungu na pia ni tukano kwake, la uasi na upumbavu. Dhambi za kingono huwezesha nguvu zozote za giza au mapepo yaliyo ndani ya mtu mmoja kuingia ndani ya mwenzi wake. Na si hilo tu, bali pia humwezesha mwenzi huyo kuingiwa na kila roho ya giza kutoka kwa uhusiano wowote wa awali aliokuwa nao mtu huyo. Hiyo husambaza giza kama vile Virusi vya Ukimwi.



Utumwa wa nafsi au muungano wa nafsi hutokana na kuunganishwa pamoja kwa aina yoyote. Utumwa wa nafsi au muungano wa nafsi ni kuunganishwa pamoja kwa mwili, roho, au nafsi katika uhusiano ambao nafsi mbili huunganishwa pamoja na kuwa kitu kimoja. Hii inaweza kufanyika kiroho, kihisia, au kimwili. Fahamu kwamba kuna muungano wa nafsi

Katika vifungu visivyopungua 55, Agano Jipya linashutumu “porneia,” neno la Kigriki lenye maana ya “uovu wa kingono.” Uovu wa kingono unaelezewa kama ngono kabla lya ndoa kwa katika ushauri wa Paulo kwa Wakristo ambao hawajaoana (1 Kor. 7:9). Hakuna majadiliano kuhusu iwapo Mungu anazichukulia dhambi za kingono kuwa mbaya sana. Dhambi za kingono ni nambari tatu katika dhambi zinazochukiwa sana, baada ya (1) “msiwe na miungu wengine ila mimi” (Kumbu. 5:7) na (2) mauaji(Kumbu. 5:17). Fahamuni kwamba dhambi hizi hufungua shimo kubwa sana katika ukuta wetu wa kiroho (marejeleo ya somo hili yanaweza kupatikana katika ukurasa wa 2 katika sehemu yenye kichwa hiki, “Uponyaji wa Roho — Utangulizi”). Fikiria pia matokeo 25 ya kuzini (Tazama Meth. 5:4-2, 6:20-25 na 16-22; 2 Sam. 10:12, 11:4-7, 12:1-7 na 13-14). Kulingana na Yeremia 3, Mungu anaiita ibada ya sanamu ya aina yoyote, kuwa ni “kuunganishwa” kwa Mungu mwingine. Anakiita kitendo hiki uasherati wa kiroho. katika kueleza uasherati wa kimwili kama “kuunganishwa pamoja kusikofaa—iwe ni kabla au baada ya ndoa na katika mahusiana ya ngono ya jinsia moja (usenge) au kuhusiana na wanyama kingono,” katika amri ya saba (Kut. 20:14) hii ina maana pana zaidi kuliko kitendo kinachofanyika katika “dhambi ya ngono kati ya mume na mke inayotendwa na watu waliooa/olewa.” Kupitia kwa muungano wa kingono, kuna kuungana kwa roho, nafsi na mwili. Baada ya kitendo cha ngono, miili inaweza kutengana lakini nafsi na roho huwa bado zimeunganishwa pamoja. Kitu fulani katika mwanamume huyo huwa sehemu ya mwanamke huyo, na kitu fulani katika mwanamke huyo huwa sehemu ya mwanamume huyo. Muungano husababisha “muungano wa nafsi” wa kiroho na kimwili kati ya watu hao wawili. Hii ni ndiyo iliyokusudiwa na Mungu atika muungano na ndoa ya kwanza kati ya mume na mke. Jambo la kusikitisha ni kwamba, watu wanapofanya ngono na watu ambao si “mume au mke wake wa kwanza na wa pekee,” hali ya kiroho ya “mwili mmoja” huchanganyika, na mpango kamili wa Mungu kwetu huzuiwa, kama vile mpango wake kwa Adamu na Hawa ulizuiwa. Kinachofungwa duniani hugungwa mbinguni. (Mat. 16:19, 18:18) Tunapoungana kingono na mtu mwingine, sisi huunganishw na mtu huyo kihisia na kiroho. Muungano wa kingono kati ya mume na mke (kama inavyoelezwa katika Mwa. 2:24) huruhusu kule kushiriki pamoja upendo na vipawa vingine vyote kati yao. Muungano wa kingono nje ya mpango wa Mungu kuhusu ndoa (Mwa. 2:24) humfanya mtu apokee mambo yote mabaya kutoka kwa mwenzi wake wa kingono (kama vile roho za giza, kumvutia mtu kwenye mazoea ya tabia mbaya, uovu wote ambao mtu huyo ameupokeakwa ajili ya dhambi zake au dhambi za mababu zake kupitia kwa laana za kizazi, kama ilivyoagizwa katika Kut. 20:5) na matokeo mengine ya dhambi ambazo mwenzi huyo wa ngono aliwahi kutenda (kama vile kujihusisha katika mizungu/ushetani). Kupitia kwa muungano wa kingono, sisi huwa kitu kimoja na roho ya mtu huyo. Hatuungani tu na mtu tuliyehusiana naye kingono, bali pia tunaunganishwa kwa mfano wa mnyororo na kila mtu ambaye amewahi kushirikiana na mtu huyo kingono. Kufanya ngono nje ya ndoa ni kuuvunjia heshima uumbaji wa Mungu na pia ni tukano kwake, la uasi na upumbavu. Dhambi za kingono huwezesha nguvu zozote za giza au mapepo yaliyo ndani ya mtu mmoja kuingia ndani ya mwenzi wake. Na si hilo tu, bali pia humwezesha mwenzi huyo kuingiwa na kila roho ya giza kutoka kwa uhusiano wowote wa awali aliokuwa nao mtu huyo. Hiyo husambaza giza kama vile Virusi vya Ukimwi. 



Utumwa na/au Muungano wa Nafsi 




Utumwa wa nafsi au muungano wa nafsi hutokana na kuunganishwa pamoja kwa aina yoyote. Utumwa wa nafsi au muungano wa nafsi ni kuunganishwa pamoja kwa mwili, roho, au nafsi katika uhusiano ambao nafsi mbili huunganishwa pamoja na kuwa kitu kimoja. Hii inaweza kufanyika kiroho, kihisia, au kimwili. Fahamu kwamba kuna muungano wa nafsi


ulio mzuri (mtakatifu, na unawezeshwa na Mungu) na pia kuna muungano wa nafsi ulio mwovu (usiomtakatifu). Muungano Unaowezeshwa na Mungu Muungano unaowezeshwa na kubarikiwa na Mungu ni pamoja na ule ulio halali na mzuri katika uhusiano wa kindoa kati ya “mume na mke”, uhusiano kati ya mzazi na mtoto, uhusiano kati ya ndugu, na uhusiano katia ya jamaa wengine (Mwa. 2:24, Mat. 19:4-9, n.k.). Muungano huo ukivurugwa na kifo, talaka, au uzinzi, kunaweza kuwa na jeraha kubwa sana. Muungano Usiomtakatifu Unaowezeshwa na Shetani Muungano usiomtakatifu unaosababishwa na shughuli za uovu wa kingono (na kwa nadhiri za giza, maagano, laana, viapo, na viapo vya siri vya vyama) huwezeshwa na Shetani na ni chukizo kwa Mungu. Dhambi za kingono huzaa muungano wa nafsi usiomtakatifu kiroho na kimwili nazo zinatakiwa kuvunjwa kabla ya uponyaji kupatikana na mfungwa kuwekwa huru. Muungano Usiosababishwa na Ngono Muungano usiosababishwa na ndoa hutokea wakati ambapo mtu mmoja humtawala mtu mwingine kwa namna ambayo Mungu hakuipanga. Wakati mwingine muungano mbaya wa nafsi usio wa kiongono hujitokeza na wazazi, washauri au marafiki—watu tunaovutiwa nao au ambao tuna uhusiano wa karibu nao au wa siri. Hii huonekana zaidi katika uhusiano wa kutegemeana. Uasherati wa Kiroho Uasherati wa kiroho hutokea (1) wakati ambapo mwenzi wa ndoa humpa mtu mwingine kitu ambacho ni cha mwenzi wake pekee (kwa mfano, kuwasiliana na mtu mwingine kwa njia ya siri kutoka moyoni au kuwa na uhusiano wa ndani na mtu mwingine), (2) iwapo moyo wa mwenzi mmoja wa ndoa haujajivunza kukumbatia chanzo cha uume au uuke katika muungano wao wa ndoa (3) unapomwonyesha mapenzi au kumbusu kwa hisia kali mtu asiye mwenzi wako wa ndoa, au (4) unapomwelezea mtu mwingine (ambaye si mshauri) hisia za 




Muhtasari wa Matokeo ya Dhambi za Kingono 

1. Dhambi za kingono huuzuia upendo wa Mungu unaotiririka kati ya mume na mke katika hali ya kweli na takatifu inayodhihirika katika hali zetu za kufanya mapenzi. 2. Uzinzi ni uharibifu ambao hatimaye huwa na gharama (sheria ya kupanda na kuvuna hujidhihirisha hapa). 3. Dhambi za kingono huzaa mazoea mabaya ya kingono, ukahaba, uzinzi, dhuluma ya kingono, ngono kati ya watu wanaohusiana kidamu, usenge, aibu, haita, na kukosa kujithamini. 4. Uzinzi hauwezi kukaa pamoja na Roho Mtakatifu; uzinzi ukiendelea, Roho Mtakatifu ataondoka. 5. Katika ngono isiyo ya kiungu, kitu fulani kutoka kwa kila mwenzi huenda kwa mwenzake na kuwa sehemu ya mtu huyo (Tazama mfano katika 1 Kor. 6:16, ambapo Paulo anazungumza juu ya watu “wanaungwa” kwa kahaba kuwa “wao hufanyika kuwa mwili mmoja.”).

6. Dhambi ya kingono huwa ni mnyororo wa utumwa ambapo watu, bila kujua huathiriwa na maisha na sifa za watu ambao wameunganishwa nao kingono. 7. Muungano wa nafsi usio wa kiroho hutoa nafasi ya mambo hayo yote kuhamishwa (kwa mapepo kuhamisha kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine—wakati wa kufanya ngono na wakati mwingine unaofuata): roho za giza, kumvutia mtu kwenye mazoea ya tabia mbaya, uovu wote ambao mtu huyo ameupokea kwa ajili ya dhambi za mababu zake kupitia kwa laana za kizazi, Kut. 20:5) na matokeo mengine ya dhambi ambazo mwenzi huyo wa ngono aliwahi kutenda, kama vile kujihusisha katika mizungu/ushetani). 8. Watu wenye wenzi wengi wa kimapenzi hupoteza sura yao. Wao huanza kusahau wao ni kina nani. 9. Fikira juu ya matokeo 25 ya uzinzi yaliyotambuliwa katika maandiko (baadhi ya mifano hiyo ni Meth. 1:8-20, 5:1-12 na 6:20-32, 2 Sam. 11:4-7, 12:1-14). 10. Mungu anachukia uzinzi. Ndiyo dhambi ya tatu mbaya kuliko ibada ya sanamu na kuua 


Neema ya Uponyaji 


Habari Njema ni kwamba Mungu wa mbinguni alimtuma Mwanawe Yesu Kristo afutie msalabani ili tupate msamaha wa dhambi zetu zote, za kingono na zengine pia, tusafishwe kwa damu ya Yesu, na tuweze kuwa na uhusiano mpya naye kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Bwana alimsamehe mfalme Daudi na yule mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi (2 Sam. 12:13, Yohana 8:11). Atakusamehe wewe pia na kukuweka huru. Labda ushakiri kwa Mungu dhambi zako za kingono “ulipozaliwa mara ya pili” na ukasamehewa. Kwa hali yoyote, hiyo haikuwezeshi kuepuka matokeo ya dhambi zako. (kwa mfano, ikiwa ulitoa mimba, je, Mungu atasemehe dhambi yako ya kuua? Ndio; alifanya hivyo msalabani; lakini ataweza kuondoa mara moja matokeo ya dhambi hiyo na kukurudishia mtoto huyo? La. Dhambi hiyo inabebwa na mama huyo lakini matokeo ya dhambi hiyo yanabebwa na mtoto huyo aliyetolewa. Wakristo wanaweza kutubu kwa moyo wao wote na bila kujua waendelee kuwa chini ya athari za giza katika sehemu ya roho zao kama matokeo ya dhambi walizofanya hapo awali) Milango iliyo wazi isipofungwa na haki iliyotolewa kwa nguvu za giza kukanushwa na kupewa Mungu, adui anaweza kuendelea kutumia sehemu hiyo ya dhambi ulizotenda awali dhidi yako, hata kama umesamehewa. 


Maombi ya dhambi za kingono

, muungano wa nafsi, na utakaso ziko hapa chini. Ombi la Kufanywa kwa ajili ya Dhambi za Kingono Ombi hili la kuwekwa huru kutoka kwa dhambi za kingono na utumwa (au muungano wa nafsi) inatakiwa kushughulikia sehemu hizi: 

1. Omba usamehewe.
 2. Omba uwekwe huru na kufunguliwa. 

3. Omba ili kuzivunja nguvu za tamaa ya kurithiwa; omba ili umsamehe mtu aliyeingiza dhambi hiyo katika ukoo wa familia. 

4. Ombea kuvunjwa kwa muungano wowote wa nafsi kati ya mhusika anayetaka kuombewa na watu aliyehusiana nao kingono au na mume wa zamani ambaye hameachana.



4a. Omba kwamba upanga wa Roho Mtakatifu utamtenganisha kila mwenzi na kuvunza kila muungano wa nafsi. 

4b. Uweke msalaba wa Yesu kati ya kila mwenzi na kuwafunika na damu ya Yesu.

 4c. “Mfungue” kila mwenzi kutoka kwa mapatano yasiyo takatifu. 

4d. Katika jina la Yesu, tangaza kutenganishwa kwa roho za watu waliojihusisha katika uzinzi. 

4e. Chukua mamlaka (katika jina la Yesu), na uvunje nguvu zozote za kishetani zilizo ndani ya maisha ya mtu huyo kwa ajili ya kujihusisha katika ngono isiyo halali, ufungwa usio wa kingono, au uzinzi wa kiroho. 

4f. Ikiwa sasa mtu huyo ameolewa kwa mtu ambaye “amezaliwa mara ya pili”, omba kwamba Mungu atatambua muungano huo wa sasa kama inavyosema katika Mwa.2:24 na Marko 10:2-12 kwamba “nao wawili watakuwa mwili mmoja”). 


5. Ombea utakaso wa mwili, nafsi na roho. 

5a. Ombi ili akili ya mtu hiyo itakaswe kutokana na picha za kumfanya mtu awe na ashiki, matukio ya kingono yasiyo ya kiungu na mawazo yote ya dhambi, maneno, na matendo. 

5b. Ombea utakaso wa macho yaliyotazama vitu ambavyo hayakutakiwa kutazama. 

5c. Ombea utakaso wa masikio yaliyosikia mambo yasiyo matakatifu.

 5d. Ombea utakaso wa mdomo, ngozi, mikono, na sehemu za siri kwa ajili ya vitu viliyovigusa.


 6. Omba ukipinga roho za uzinzi, kutazama picha zinazoleta ashiki, desturi za kingono zisizo za kawaida, hasa ikiwa mhusika huyo amewahi kufanya ngono na kahaba au mnyama.

 7. Ombea mhusika ili aweze kuwekwa huru kutoka ana uvozu huo wote na kutoka kwa matokeo ya dhambi hizo.

 8. Omba kwamba Mungu atayaponya matukio hayo yote ili Shetani asiweze tena kuyatumia kwa makusudi ya uovu.

 9. Mwombee mhusika huyo ili aponywe kutokana na kila hatia na aibu. 

10. Ombea uponyaji wa dhambi hizo zote na muungano wa nafsi, ili mtu huyo aweze kufunikwa kwa damu ya Yesu. 

11. Kwa watu ambao hawajaingia katika ndoa, omba kwamba “hisia za kawaida za kingono” zitaelekezwa katitka shughuli zinazokubalika na zinazofaa. 

12. Mfungue kutokana na uzinzi na ndoa za wake wengi za vizazi vilivyotangulia


Sehemu hii ya dhambi za kingoni inahitaji kumtumia mwombezi. Ni vigumu sana kwa mhusika kujiombea na kufanikiwa kabisa katika sehemu hii. Kwanza mhusika anahitaji kukiri dhambi hiyo na kutubu kwa sauti akimtaja mwenzi wake (au wenzi wake, ikiwezekana, kama anvyoelekezwa na Mungu). Pia, mhusika anatakiwa kutubu kwa ajili ya matendo ya kingono yasiyo halali na yasiyo ya kawaida pamoja na utazamaji wa picha za kumpa mtu ashiki, ikihitajika kufanya hiyvo. Anatakiwa kukanusha roho wa tamaa, tamaa ya macho, na kukanusha nafasi ya Shetani, aliyopewa hapo awali kwa kufanya matendo hayo yote. Jambo muhimu ni mhusika huyo kuamua kuishi maisha matakatifu au kuoa (1 Kor. 7:1-16). Ni vigumu kuvunja mwenendo wa kingono wa hapo awali, hasa ikiwa mhusika huyo ni kijana ambaye hajaoa. Katika kila hali, mhusika anatakiwa kuonywa kwamba Shetani atamtia katika majaribu baada ya kupata uponyaji.


 Ombi la Kumfungua na Kumweka Mtu Huru
Mwombezi anatakiwakuomba ombi hili


Katika jina la Yesu, ninaamuru roho yako isahau miungano hii. Katika jina la Yesu umefunguliwa kutoka kwa mtu huyo (au watu hao). Ninatangaza kutenganishwa kwa roho yako kutoka kwa kila mwenzi huyo, na ninauweka msalaba wa Yesu kati yako na kila muungano huo usio mtakatifu. Ninakufunika kwa damu ya Yesu kama ngao ya kukulinda kutokana na athari zozote mbaya zilizokujia kupia kwa miungano ya kingono kati yako na mwenzi (au wenzi) hao. Ninaiweka roho yako huru ili iambatane na mwenzi wako wa ndoa. Ninakuweka huru katika jina la Yesu, ninashukuru kwa ajili ya neno la Mungu linalotangaza, “…kila utakachofunga duniani, kitafungwa pia mbinguni; kila utakachofungua duniani, kitafugnuliwa pia mbinguni” (Mat. 16:19). (Endelea kuomba ombi la utakaso, lililo hapa chini.)


Ombi la Utakaso 


Kutoka katika Ezekieli 36:25 (“Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtatakata uchafu wenu wote na sanamu za miungu yenu yote”) na Matendo 11:9 (“Ile sauti ikasikika tena kutoka mbinguni: usiviite najisi vitu ambavyo Mungu amevitakasa.”) tunaamini tumetakaswa; na kutoka Waebrania 10:10 (“Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.”) tunaamini kwamba kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo, tumetakaswa. Ninaomba kwamba Mungu atayanyunyizia maji yake safi juu ya kila kitu kinachohitaji kutakaswa. (Wakati mwingine Mungu anaweza kukupa picha; omba kuhusu unachoona katika picha hiyo.) Yesu, tunakuomba sasa umimine mito yako ya maji ya uzima juu ya _____________ na katika kila seli ya mwili wake. Yaache maji hayo yatiririke juu ya kila sehemu ya mwili wake, kicha, mikono, sehemu za siri, miguu, nyayo. Asante Bwana kwa sababu maji yako ya uzima yanamtakasa mtu huyu “awe mweupe kama theluji,” (“Haya njooni tusemezane, asema BWANA: Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana zitakuwa nyeupe kama theluji; Zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.”—Is. 1:18) kwamba kila sehemu ya kuchafuliwa, aibu, na hatia inaoshwa.


Asante Bwana kwa kumsafisha mtu hulyu, ndani na nje. Bwana, sasa unamwona kuwa safi na mweupe kama alivyokuwa siku ambayo ulimuumba kule mbinguni—umempa mwili mpya katika Yesu, mwili safi na mtakatifu. Asante. Katika jina la Yesu nimeomba. Amina.



Vifaa


1. Doris Wagner, Ministering Freedom to the Sexually Broken (Wagner Publications, 2003). ISBN 1-58502-038-9. (Hiki kitabu kilikuwa kifaa bora zaidi kuhusu somo hili— ambacho mambo mengi yaliyo hapa juu yalitolewa.) (now 4 booklets are combined into one 332 page booklet entitled “How to Minister Freedom”, Wagner, Doris, 2005 ISBN 0830737251, 30 contributors) 2 John & Paula Sandford, Transformation of the Inner Man (Victory House, 1982): 269-94. ISBN 0-932081-13-4. 3. Elaine Rose Penn, Soul Ties (Charisma Training Ministries, PO Box 2410, Albany, NY 12220, 2000). ISBN 0-9700449-0-9. 4 Bill and Sue Banks, Breaking Unhealthy Soul-Ties (Impact Books, 322 Leffingwell Ave., Suite 101, Kirkwood, MO 63122, 1999). ISBN 0-89228-139-1.


Kutazama Sinema/Picha Za Matukio ya Ngono



Neno hili “Ponografi” limebuniwa kutoka katika neno la Kiyunani “porne”asmbalo linaweza kutafsiriwa kuwa na maana ya kahaba wa kike au mtumwa wa kimapenzi. Neno Porneia lina tafsiri ya uzinzi, usherati au uchafu wa kimapenzi. Katika Agano Jipya kuna vishiria 26, sita zikiwa kwenye nyaraka za Paulo kwa Wakorintho. Muktadha wake ni kuwa waumini hawapaswi kuhusika katika tamaduni ambazo ziliwazingira waumini wa nyakati hizo. “Lakini mimi nawaambia: kwamba ye yote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” (Math 5:28). Naamini kuwa andiko hili linaashiria picha na sinema za watu walio uchi tunazozitazama kwenye majarida, runinga, filamu, simu, na komputa na hata kuwatazama watu walio uchi. Miili yetu haikuumbwa kwa kutazamwa ikiwa uchi (1Wakorintho 6:13). Yatupasa tuepukane na tabia hii (1Wakorintho 6:18) na kujikinga tusije tukaishia kuwa watumwa (1 Wakorintho 7:2). Iwapo tumekita mizizi ndani yake lazima tutubu na kumgeukia Mungu (2Wakorintho 12:21) Jambo la kusikitisha ni kuwa kule Marekani Serikali inaruhusu kutazama picha hizi kama sehemu ya haki za wananchi za kikatiba. Tukiuangalia mtandao tunagundua kuwa jambo hili limeenea kote na linafanyika kwenye siri za vyumba vya watu. Yafaa itambuliwe kuwa kila kilichofichika hutumiwa na Shetani kutudhuru sisi. Lipo kundi moja linajiita Wawekaji wa Ahadi lililoanzishwa 1990, katika mojawapo ya mikutano yao kwenye halaiki ya watu 60,000 asilimia 60% walikuwa wamejihusisha katika tendo hili. Hawa walikuwa ni washirika wa kanisa na hata viongozi wenye nafasi za kutamanika kwenye kanisa. Kutokana na mikutano yao kulitokea chombo cha filamu kiitwacho: Personal Holiness in Times of Temptation, kama sehemu ya kujikita kwenye mafunzo ya



Biblia iliyoandaliwa na Dr. Bruce Wilkinson. Shida hii inaathiri watu wengi kanisani na nje yake wala haliathiri watu wachache tu. Tendo hili la ponografi ni uasi kwa Mungu na nafsi yake iliyo ndani yetu. Inaharibu thamani ya kujuana kimapenzi na kuifanya kama chombo cha ubatili. Hudunisha thamani ya mwili wa mwanadamu na ni sumu inayoufanya mwili kuwa chombo cha kibiashara. Wanaume wengi wanaohusika katika tendo hili hupoteza hisia zao za kimapenzi na kumdharau mwanamke aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu ili kumkamilisha mwanamume. Kila mtu anazitazama picha hizo ndivyo anavyodidimia katika utumwa wa kutofurahia tendo la ndoa na mpenzi wake wa halali. Kama chakula kinavyotumika mwilini ndivyo picha hizi zinavyoathiri mawazo na hisia za mtazamaji. Mwishowe mtazamaji anaweza kufananishwa na mtu anayetumia madawa ya kulevya na pombe kali. Utazamaji huu mwishowe humfanya mtu mtumwa na akawa hawezi kufikiri kama Mungu alivyokusudia. Watu wanaotazama picha au filamu hizi mwishowe huanza kutumia vyombo visivyo vya kawaida kukidhi mahitaji yao ya kingono. Dhambi hizi mtu huzitenda kinyume cha mwili wake mwenyewe (1 Wakorintho 6:17. Miili yetu inapaswa kuwa makani/hekalu la Mungu (1 Wakorintho 6:12-20) Tunapojihusisha na matendo yaliyo kinyume ya mapenzi ya Mungu, tunamuasi Mungu. Roho mtakatifu huumia na anaweza kuhama kutoka katika nafsi zetu. (Efeso 4:31). Tendo hili linamzuia Roho Mtakatifu wa Mungu kutenda kazi ndani yetu. Na tunweza kufikia mahali ambapo tunaweza kumuudhi roho. (1 Thes 5:19) Wanadamu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu, ili tumjue, tumpende na kumuabudu Kristo. Tunapaswa kila mara kuishi na kufanana na Mungu ili tufikilie utakatifu. Ili tuiondokee hii dhambi, ni sharti tutubu na kugeukia tabia hii na pia kuwahusisha wakristo wengine ili waweze kuwa msaada wa karibu katika kutuhimiza tuondokane na dhambi hii. Mungu anatuhitaji tuishi katika utakatifu kwenye masuala ya ngono. Hivyo basi kutazama picha za matukio ya ngono au watu walio uchi ni dhambi. Jee kuiga tendo la ndoa kwa kutumia vyombo visivyo vya kibinadamu ni halali? Ijapokuwa Bibilia haisemi chochote kuhusu jambo hili, 



swala tunalopasa kujiuliza ni: Je tendo hili linanielekeza kwa utakatifu? Wengine hunukuu Mwanzo 38:9: “Lakini Onani alijua kwamba uzao haungekuwa wake, kwa hiyo kila alipokutana kimwili na mke wa ndugu yake, alimwaga chini mbegu za kiume ili asimpatie ndugu yake uzao..” ili kueleza kuwa inakubalika kwenye Bibilia. Lakini tuseme tafsiri hii si sahihi. Tendo hilo ni dhambi kwa kuwa mila za Waisraeli zilimtaka ndugu wa kiumu wa mwanamume kumzalia nduguye watoto akikutana na mjane wa nduguye aliyekufa. Mfano huu watuonyesha kuwa Onani hakuwa mtiifu kwa desturi hii ndiposa Bwana akamuua. Je tubadili vipi mawazo yetu kuelekea utakatifu? Jawabu ni toba na kutubu. Kila kilichofichika chatuelekeza dhambini na ni mlango wazi kwa adui kuingilia. Haitoshi kuomba msamaha kwa Mungu pekee. Ni vyema kutubu mbele ya wapendwa na Mungu. Pia ni vyema kutubu kwa mchungaji na kama sisi ni wachungaji tutubu kwa maaskofu ili tupate kuwajibika anayeweza kutusaidia na kututia moyo tusije tukaanguka tena Ombi La Uponyaji Baada ya toba na maombi ya msamaha, mtafutaji asaidiwe kukana tama za mwili, macho na usherati uliokithiri moyoni mwake (Math 5:28). Mwombezi amuombe Mungu amletee mtafutaji picha ya tukio lile la kwanza. Kisha ombi lifanywe ili Yesu aingie kati ya mtafutaji na tukio. Omba damu ya Yesu imfunike mtafutaji kasha yeye mwenyewe amuombe Mungu afute kumbukumbu ya matukio yote yasioletea Mungu utukufu na kumtakasa. Mapepo ya uchu, tamaa ya macho na usherati yapasa kukemewa yatoke Ilani: Habari hizi zimenukuliwa kutoka kwa kitabu cha William M. Struthers, Wired for Intimacy. How pornography hijacks the male brain. 2010, ISBN 978-0-8308-3700-7. Nyongeza A ina orodha ya vifaa vilivyo kwenye mtandao ili kumsaidia mtu kuepukana na Ponografi na ulevi wa ngono. Nyongeza B ina vitabu juu ya namna ya kumsaidia mtu kuepukana na Ponografi na ulevi wa ngono. 




No comments:

Post a Comment

NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.