Vichwa vya Habari

JE, NITAFAHAMU NAMNA GANI KWAMBA NINAYE ROHO MTAKATIFU?



Utanena kwenye lugha nyingine ambayo Roho mtakatifu atakupa
baada ya kumpokea. Kwa mara ya kwanza Roho Mtakatifu
kupeanwa katika Matendo 2:4, Biblia inasema, "Wote wakaanza
kunena kwa lugha nyingine ambayo Roho mtakatifu aliwawezesha
kunena."
Mungu alinena kupitia nabii lsaya kwamba mambo haya  3
yatafanyika. 'Bali kwa midomo ya watu wageni, na lugha nyingine
Mungu atanena na watu Wake.
(Isaya 28:11) Yesu akasema ya kwamba watu wote watakao weka
imani yao kwake, watanena kwa lugha hata ile hawakujifunza
(Marko 16:17).
Petro alifahamu ya kwamba watu wa Mataifa walipokea Roho
Mtakatifu kwa sababu aliwasikia wakinena kwa lugha nyingine
kwenye nyumbe ya Komelio (Matendo ya Mitume 10:46). Katika
matendo ya Mitume 19:6, Wakati Paulo aliweka mikono yake juu
yao, Roho Mtakatifu aliwashukia. Wakaanzakunena kwa
lughanyingine na kumtukuza Mungu." Hii inazungumza juu ya
wafuasi wa Efeso. Watu wa Mungu hata leo hunena kwa lugha
wanapo pokea Roho Mtakatifu.

No comments:

Post a Comment

NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.