Vichwa vya Habari

UNGANISHA SADAKA YAKO NA UWEPO WA MUNGU ILI AJIDHIHIRISHE KWAKO


by Mwl. Christopher Mwakasege - Day 1
(Viwanja vya Reli - Arusha 9/09/2012)
LENGO: Kuimarisha uhusiano wako wewe na MUNGU kwa kusaidia namna ya kuunganisha sadaka yako, na uwepo wa MUNGU Ipasavyo.
Mambo matatu yanayohusha uwepo wa MUNGU
1. Kunatofauti ya uwepo wa MUNGU na unafanya kazi na ule uwepo wa MUNGU uliopo lakini haufanyi kazi.
Luka 5:17 “Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na uyahudi, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya”
Utaona namba uwepo wa MUNGU ulikuwa mahali hapo,
1 Samweli 4:1-22
2. Ukitoa Sadaka palipo na uwepo wa MUNGU uliokazini(Active)/unaofanya kazi utajua
**Mwanzo 4:3-16 “Hapa tunaona kwa habari ya Kaini na Habili walipotoa sadaka na kwavile kulikuwa na uwepo wa MUNGU mahali pale Mungu alikubali sadaka ya Habili na kukataa ya Kaini, lakini siyo tu alikataa sadaka ya Kaini bali alimkataa pia na Kaini mwenyewe, Hivyo uwepo wa MUNGU ukiwepo Active utajua tu…
**Matendo 4:36 hadi Matendo 5:1-4 “Hapa utapata habari za Anania na Safina walipo jaribu kumdanganya roho wa MUNGU, mahali pale kulikuwa na uwepo wa MUNGU sasa kilichofanya uwepo wa MUNGU kujifunua nikuweka yaliyowazi maana Anania na Safina walidhani watamdanganya Petro, na kumbe kulikuwa na Uwepo wa Bwana mahali pale…
3. Ukitoa Sadaka Mahali palipo na Uwepo wa MUNGU na usijizihirishe unamaana kuna namna unatakiwa ufanye ili kusukuma/kuwasha/kufanya utukufu wa Bwana uwe Active..
**1 Samwel 1:1-6,9 “Hapa tunamwona Ana ambaye yeye alikuwa hana mtoto, Analichukua uamuzi wa kuingia madhabahuni na kufanya au kuwasha uwepo wa MUNGU uwe active, ni kweli Ana alikuwa anakwenda madhabahuni na alikuwa anatoa sadaka, lakini ilibidi atafute namna ya kuweka Uwepo wa MUNGU uwe active, ndipo anaalimwekea MUNGU nadhiri, na kumbuka NADHIRI ni sadaka yako ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako, sawasawa na kitabu cha Kumbukumbu la Torati 23:23
2 Wafalme 4:8-17 “Tunamwona mwanamke ambaye hakuwa na mtoto na alijua inabidi ataufute namna yakuwesha Uwepo wa MUNGU kuwa active, nikweli alikuwa anaomba sasa ilibidi amwambie mumewe watengeneze chumba na tena waweke na kitanda ili mtumishi wa MUNGU apate kulala, najua siyo jambo la kawaida maana hata hajawahi kulala na tena ukifikiria je kama hasingekuja na mwanamke huyo hana mtoto? Kwahiyo yeye alichojali nikutafuta uwepo wa MUNGU kwani sadaka yake ni kumtuza mtumishi wa MUNGU,(Gehazi)
UNGANISHA SADAKA YAKO NA UWEPO WA MUNGU IPASAVYO
by Mwl. Christopher Mwakasege - Day 2
(Viwanja vya Reli - Arusha 10/09/2012)
LENGO: Kuimarisha uhusiano wako wewe na MUNGU kwa kusaidia namna ya kuunganisha sadaka yako, na uwepo wa MUNGU Ipasavyo.
Umuhimu wa Imani katika kumuunganisha mtoa sadaka na MUNGU
Waebrania 11:1 “Basi Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyooneka”.
Imani inamambo Mawili(2)
*Wakika wa mambo yatarajiwayo
*Wakika ndani
Imani inakupa kuona yale yasiyoonekana/usiyoyaona(Fursa ya mambo usio yaona) au inakupa kupita ambako watu wengine wanaona hapapitiki
Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neon la Kristo”.
Mastari wa 10 “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata hakim, na kwa kinywa ukiri hata kupata wokovu”.
Imani haitakiwi iende peke yake ni lazima iende na kitu, na kitu moja wapo ni matendo. “Imani pasipo matendo imekufa”
Unapotoa sadaka ni lazima uunganishe na imani, kwani imani ndio Connector.
Mfano: Waebrania 11:1-33 Inazunumza juu ya Imani na Matendo watu waliyofanya Imani(Waliofanyia imani kazi)
Kwenye Mstari wa 4-31 Wametajwa watu 11 waliotumia imani…
*Tuangalie watu 5 katika hoa 11
Mstari wa 4 “Kwa Imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena”
Mstari wa 17-19 “Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; nay eye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee;18 naam, yeye aliyeambiwa , katika Isaka uzao wako utaitwa, 19 akihesabu ya kuwa Mungu awza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano”.
Habari ya Isaka utaona habari ya sadaka ya mtoto sasa kile chakula ilikuwa sadaka ya
Kunatofauti katika kumpa mzazi sadaka na kumsaidia, na Baraka zake ni tofauti pia.
Mstari 28 utaona jinsi mussa alivyotoa sadaka maana biblia iansema kwa Imani akaifanya Pasaka, sasa uwe na uwakika Pasaka ni uzaliwa wa kwanz…
Mstari wa 31 “Kwa Imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani.
• Katika watu hawa 5 Mungu alimpa mwalimu kufanya Asilimia kulinganisha na wale wote 11, Mwalimu alipata asilimia 45.5% sasa unaweza ona toka Asilimia 100% kwa nini katika sadaka?
Watu hawa walivyotoa sadaka walifungua ukurasa mpya wa maisha yao, MUNGU aliwapatia ukurasa mpya
Mungu akiachilia ukurasa mpya watu wakitoa sadaka, kama watu wakiipoteza hawataipata tena.
Rahabu asingetoa sadaka kwa imani(huku na uwepo wa MUNGU ufanyao kazi) asigne toka katika eneo hilo(ukahaba)
Imani ni Connector ya Future
Mwanzo 15:1-21
Baada ya hayo “maana yake urudi nyuma kabla ya hayo”
Baada ya sadaka mambo hayo(ya awali)
Mungu alimuuliza Ibrahimu kuhusu future baada ya kutoa sadaka ya Fungu la Kumi
Mstari wa 7 “Kisha akamwambia, Mimi ni BWANA, niliyekueta kutoka Uru wa Wakaidayo nikupe nchi hii ili uirithi”
Mstari wa 8 “Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi?
Kinacho msumbua Ibrahimu ni kutokuwa na mtoto ndo maana alipata ujasili wa namna atakavyo rithi nchi..
Mungu alimjibu amatie ndama wa miaka 3, maana yake Mungu alitaka sadaka maana ni taratibu kutoa sadaka
Siyo Sadaka tu Ibrahimu aliachia ni lazima uwe na uwakika na Imani(Uwepo wa MUNGU) ilikuwepo, maana kila mtu anaweza kutoa sadaka
Maswali yatakayo kusaidia kukuza Imani katika hili
1. Mungu anaptaka utoe sadaka, anataka nini kwako?(MUNGU anapata nini?)
2. Wewe utapta nini?(MUNGU atakupa nini?)
3. Nisipotoa anachotaka na unachotaka kitatokea nini? (Ni kikauka kutoa utapata nini?
4. Nimekaribia kiasi gain sura mpya ya maisha yangu ili niweze kutoa sadaka?

NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.