Vichwa vya Habari

MALAIKA: WAJUMBE WA MUNGU

‘Familia yote ya mbinguni na duniani’
Malaika kwa sasa ni sehemu ya lile ambalo mtume Paulo aliiita ‘ubabu wote wa mbinguni’ – Mungu Baba, 
Yesu mwana wa Malaika. Karibu familia itakuwa imekamilika Yesu atakaporudi mara ya pili hapa duniani 
na ndipo wataongezeka ‘wana wa Mungu’-Wanafunzi waaminifu wa Kristo – ambao watatawala dunia.
Pamoja naye; kwa hiyo nampigia Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo magoti, ambaye kwa jina lake 
ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa. (Waefeso 3:14,15,UV). Muumba anakaa katika nusu
isiyoweza kuharibiwa na anaweza kuonekana kuwa yuko mbali sana na sisi mara kwa mara. Lakini ile
familia ya Mungu imetoa ule utofauti uliokuwepo, na siku itakuja ambapo mwisho wa miaka Elfu moja
dhambi zote zitakuwa zimeondolewa na mauti itashindwa na Mungu atakuwa yote katika wote (1
Wakorintho 15:28).
Ni jinsi gani Malaika wanavyotuhudumia?
Kwa mwamini, kule kufahamu kwamba malaika wapo kwa faida yake hii ni msaada wa kutosha. Kama
tunavyoweza kuwa na Imani na daktari wa upasuaji mkubwa (ingawaje hatumuoni kwa macho kwa
sababu ya dawa ya usingizi na ganzi), hivyo kuelewa kazi ya malaika ni kuwa na imani katika ulinzi wa
Mungu kwetu na namna Mungu anavyohusika katika maisha yetu. Kwa hakika, kwa matendo ni kitu zaidi 
ya hapo. Kama kweli tuwaaminifu, tunamwomba Mungu na Mungu anajibu maombi yetu kwa pamoja
kama anavyopenda yeye. Hutuma malaika wake ambaye, bila kuonekana anaamuru mazingira na hali
tulizonazo, na hivyo kubadilisha maisha yetu: Hatua za mtu huimarishwa na BWANA. 
Tufupishe kwa kusema, kweli malaika wanaishi na wapo kwa ajili ya kutusaidia kama tunamcha Mungu. 
Ukweli hautegemei yale tunayoyaona. Na hali ndilo kosa kubwa alilolifanya Bwana Khrushchev. Vitu
kinavyoonekana ni ya muda tu bali visivyoonekana ni vya milele ( 2Wakorintho 4:18,UV).
Wakati Jeshi la mbinguni wanapotumwa kuwakusanya wateule pamoja kwa ajili ya hukumu Yesu
atakaporudi, wateule wataweza kukutana na kuwaona malaika kwa mara ya kwanza Mwaliko huenda
ukawa hivi, ‘Bwana amekuja anawaita!" (Yohana 11:28). Kwa sasa ni wakati wa kumwamini BWANA
MUNGU na malaika zake na hivyo kujiandaa kwa ajili ya tukio hili kubwa: "Unifumbue macho yangu, ili
niyatazame maajabu yatokayo katika Sheria yako". (Zaburi 119:18).
(8)
MALAIKA: WAJUMBE WA MUNGU 
MAFUNDISHO YA BIBLIA KUHUSU HUDUMA YA VIUMBE WA KIROHO. 
Habari imeeleza jinsi mwanaanga wa kwanza wa Kirusi aitwaye Yuri Gagarin, aliagizwa na Khrushchev
waziri mkuu wa serikali ya Urusi ( iliyokuwa inaitwa Soviet) ili kuangalia kama kuna malaika angani,
ilikuwa ni mwezi wa April mwaka 1962. Aliporudi kutoka angani alitoa taarifa kwamba "hakuna malaika
aliowaona". Na Khruschehev" alimpongeza, nilijua usingewaona kwani hakuna vitu vya namna hiyo" 
Ni rahisi kudhania, kwamba kile usichokiona hakipo!.
Je, wewe unaamini kuwa malaika wapo? Je, unafahamu malaika ni nani, au wanafanya nini? Je, ni fikra 
za mafundi sanaa katika michoro ya dini toka karne na karne? Hivi kweli kuna kitu tunachopaswa
kukifahamu? Je ni muhimu kujua kama malaika wapo?
Tuangalie Biblia 
Majibu sahihi ya maswali hayo yanapatikana tu katika Biblia . hatuna chanzo kingine cha habari
kinachoaminika .Biblia ni neno lenye pumnzi ya Mungu na lina maktaba ya habari inayoongelewa, kwa
hiyo,ni wapi pa kuangalia? 
Twende moja kwa moja kwenye biblia, kupata ushahidi unaoonekana kuhusu hawa viumbe wa mbinguni. 
Mfano tunaopaswa kuangalia, wa kwanza si tukio la kwanza kabisa wakati malaika wanapotajwa, lakini ni 
wa kutupatia mwanga. Katika nyakati zile, mnamo karne ya 8KK falme za syria na Israel zilikuwa
zikipigana vita. Mfalme wa Shamu alifadhaishwa baada ya kugundua vilipo vikosi vyake vya mbele.
2wafalme 6:8-11. Baada ya kuambiwa kuwa mtoa habari alikuwa Elisha nabii wa Mungu, watumishi wake 
wakamteremkia Elisha na mtumishi wake katika mji mdogo ulio Kaskazini mwa Israeli. Mfalme wa Shamu 
alipeleka jeshi kubwa kwenda kumkamata nabii, wakaizunguka Dothani wakiwa na magari ya farasi na
wapanda farasi wakati wa usiku. Mtumishi wa Elisha alipotazama asubuhi aliliona jeshi kubwa
aliogopeshwa, "Ole wetu, bwana wangu tutafanyaje?" 
Mtu ambaye macho yake yalifumbuliwa 
Ilikuwa ni mwitikio wa asili: Walizingirwa na jeshi kubwa lililokuwa katili na adui aliye penda kutesa
asiyeweza kuonyesha huruma hakika alistahili kwa njia yoyote kutishika. Lakini bwana wake yeye
alitenda tofauti kabisa! Hakuwa na wasiwasi na alikwa mwenyematumaini, mwitikio wa Elisha ulikuwa!
"Usiogope!" usiogope? Ninani asiyeweza kuogopa katika hali ya namna hii? Sababu ilikuwa,
"walioupande wetu ni wengi kuliko walio upande wao": Alikuwa ana maanisha nini? Je, yawezekana
Elisha aliweza kuona kitu ambacho mtumishi wake hakuweza kuona ? Yote yaliweza kuwa wazi wakati
nabii alipomuomba Mungu. 
Bwana ninakusihi mfumbue macho yake ili aweze kuona. Naye BWANA akayafumbua macho ya kijana
naye akaona tazama kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyo kuwa yamemzunguka
Elisha pande zote" (2 Wafalme 6:17). 
Elisha alikuwa mtu wa Mungu, naye BWANA alikuwa ametuma jeshi lake la ulinzi wake katika
kumhudumia nabii wake. Elisha tayali alikuwa ameshaona jambo kama hilo muda kabla ya Eliya
mtangulizi wake hajachukuliwa kwenda juu kutoka kwake ndipo Elisha alilia "Baba yangu, baba, yangu
gari la Israeli na wapanda farasi wake (2 wafalme 2: 12).
Elisha alijua kutokana na tukio aliloliona ya kwamba malaika walikuwepo pale, mtumishi wake ambaye
alikuwa hajawahi kuona alikuwa hafahamu uwezo halisi hutoka wapi. Macho yake kiroho yalikuwa
yamefumbwa. 
Mungu hufanya kazi kupitia Watumishi wake. 
Tukio la Dothani ni ufunuo unaofundisha namna Mungu anavyo fanya kazi kwa kumlinda mtu kwa njia ya 
jeshi lake ambao ni wajumbe watumishi.
(

NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.