Vichwa vya Habari

UTAWALA WA SHETANI DUNIANI NA NGUVU ZA ROHO WA BWANA KWA WAMTAFUTAO

Kulingana na Maandiko, hakuna shaka kwamba Shetani anatawala juu ya majeshi ya pepo wabaya ambao wanakaa katika anga la dunia, na wanaomsaidia kutawala ufalme wa giza. Biblia pia inaonyesha kwamba katika hao pepo, wapo wenye kutawala eneo fulani kijiografia (ona Danieli 10:13, 20, 21; Marko 5:9, 10). Maandiko pia yanaonyesha kwamba Wakristo wana mamlaka ya kutoa pepo katika watu wengine, na wana wajibu wa kumpinga Shetani (ona Marko 16:17; Yakobo 4:7; 1Petro 5:8, 9). Lakini je, Wakristo wanaweza kuangusha mapepo walioko juu ya miji? Jibu ni kwamba, hawawezi, na kujaribu kufanya hivyo ni kupoteza muda wao.
Kwa kuwa tunaweza kutoa pepo katika watu si sababu ya kudhani kwamba tunaweza kuangusha pepo wanaotawala juu ya miji yetu. Ipo mifano mingi sana ya watu kutolewa pepo katika Injili na kitabu cha Matendo, lakini, unaweza kukumbuka mfano hata mmoja wa mtu kuangusha pepo aliyekuwa anatawala mji au eneo la kijiografia katika Injili au Matendo ya Mitume? Huwezi kwa sababu mifano hiyo haipo. Je, unakumbuka fundisho au ushauri hata mmoja katika nyaraka, kuhusu wajibu wetu kuangusha mapepo wabaya kutoka angani? Hakuna. Basi, hatuna msingi wa KiBiblia kuamini kwamba tunaweza au tunapaswa kupambana katika “vita ya kiroho” dhidi ya mapepo wabaya katika anga.Mara nyingi Wakristo hufanya kosa la kupata maana nyingine zaidi ya iliyokusudiwa na Mungu katika vifungu vya Maandiko vinavyotumia lugha ya mfano. Mfano mzuri ni jinsi wengi wanavyoelewa vibaya maneno ya Paulo kuhusu “kuangusha ngome” yafuatayo.
Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili. (Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangushya ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia (2 Wakor. 10:3-6).
Kutokana na maneno hayo – “kuangusha ngome” – ambayo ni lugha ya mfano, fundisho zima limejengwa ili kutetea wazo la kufanya “vita ya kiroho” kwa ajili ya “kuangusha ngome” za mapepo katika anga. Lakini ni vizuri tuelewe kwamba Paulo hapo hasemi juu ya mapepo katika anga, bali ngome za imani za uongo ambazo zimo katika mawazo na akili za watu. Paulo anaharibu fikra, si mapepo wabaya katika ulimwengu wa roho!
Hili linakuwa wazi zaidi tunaposoma maandiko hayo kulingana na mantiki yake. Paulo alisema hivi: “tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo” (maneno mepesi yameongezwa ili kukazia). Vita ambayo Paulo anaizungumzia kwa lugha ya mfano ni vita dhidi ya mawazo au fikra ambazo ziko kinyume na maarifa ya kweli ya Mungu.
Kwa kutumia mifano ya kijeshi, Paulo anaeleza kwamba tuko vitani, vita ili kupata mawazo ya watu walioamini kweli za Shetani. Silaha yetu kubwa katika vita hii ni ukweli, na ndiyo sababu tumeagizwa kwenda duniani kote na kuhubiri Injili, tukivamia eneo la adui kwa ujumbe unaoweza kuwaweka mateka huru. Ngome tunazoharibu zimejengwa kwa matofali ya uongo, na kuunganishwa na sementi ya udanganyifu.

kupenda fedha

     Je mibaraka au mali yatoka wapi? Imeandikwa, Kumbukumbu la torati 8:18 "Bali utamkumbuka Bwana Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu zakupata utajiri ili alifanye agano lake alilowapa baba zako kama hivi leo.                                                                                                                                 
Yeremia 9:23-24 "Bwana asema hivi mwenye hekima asijisifu kwa hekima yake wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake bali ajisifuye ajisifu kwa sababu hii ya kwamba ananifahamu mimi na kunijua ya kuwa mimi ni Bwana nitendaye wema na hukumu na haki katika nchi maana mimi napendezwa na mambo hayo asema Bwana." Mali yaweza kutupa mfano mbaya juu ya vitu. Imeandiikwa, Luka 12:15 " Yesu akawaambia angalieni, jilindeni na choyo maana uzima wa mtu haumo katika vitu vyake alivyo navyo."
Si vyema kuweka pesa mbele ya vitu vingine vyote. Imeandikwa, Mathayo 6:24 "Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu na ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu hamwezi kumtumikia Mungu na mali." 1 Timotheo 6:9 "Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi na tamaa nyingi zisizo na maana zenye kudhuru ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu."
Ni vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. Imeandikwa, Marko 10:23-25 "Yesu akatazama kotekote akawaambia wanafunzi wake jinsi itakavyokuwa shida kwa mwenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu ,wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake Yesu akajibu tena akawaambia, wanafunzi wake  jinsi ilivyo shida kwa mwenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu."
Kupenda pesa huleta dhambi. Imeandikwa, 1Timotheo 6:10 "Maana shina moja ya mabaya ya kila namna ni kupenda fedha amabayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani na kujichoma kwa maumivu mengi."
Kutosheka sikuwa na mali au fedha nyingi. Imeandikwa, Wafilipi 4:12-13 "Na jua kudhiliwa tena na jua kufanikiwa katika hali yo yote katika mambo yo yote nimefundishwa kushiba na kuona njaa kuwa na vingi na kupungukiwa na yaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu." Mathayo 6:21 "Kwa kuwa hazina yako ilipo ndipo utakapokuwapo moyo wako."

manabii wa uongo

          BWANA Yesu alituonya ya kuwa siku za mwisho kutakuwa na makristo wa uongo na kujifanya wakombozi wa ulimwengu huu. Imeandikwa, Mathayo 24:4-5 "Yesu akajibu akasema angalieni mtu asiwandanganye kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ni kristo nao watawadanganya wengi."
Yesu alisema dalili ya siku za mwisho ni makristo wa uongo. Imeandikwa, Mathayo 24:23-26. "Wakati huo mtu akiwaambia tazama kristo yuko hapa au yuko kule msisadiki maana watatokea makristo wauongo na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza yamkini hata wateule. Tazama nimekwisha kuwaoya mbele. Basi wakiwaambia yuko jangwani msitoke; yumo nyumbani msisadiki."
Paulo aliwaonya watu kuhusu mitume wa uongo wasio hubiri Yesu wabibilia. Imeandikwa, 2Wakorintho 11:3-4 "Lakini nachelea kama yule nyoka alivyo mdanganya Hawa kwa hila yake asije akawaharibu fikara zenu mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Maana yeye ajaye akihubiri Y esu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri au mkipokea roho nyingine msiyoipokea au injili nyingine msiyo ikubali mnatenda vema kuvumilia naye."
Wakristo hao wa uongo wanamtumikia nani? Imeandikwa, 2Wakorintho 11:13-15 "Maana kama watu hao ni mitume wa uongo watendao kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mitume wakristo wala siajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru Basi si neno kubwa watumishi wake wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi yao."
Kabla ya kuja Yesu  mara ya pili kutakuwa na dhihirisho la makristo wa uongo. Imeandikwa, 2Wathesalonike 2:3-4 "Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana siku ile haiji usipokuja kwanza ukengeufu ,akafunuliwa yule mtu wa kuasi mwana wa uharibifu yule mpingamizi ajiinuae nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa ambaye yeye mwenyewe huketi katika hekalu la Mungu akijionyesha nafsi yake kanakwamba yeye ndiye Mungu."
Je? Mwisho wa kristo wauongo utakuwaje na tutawajua vipi? Imeandikwa 2Wathesalonike 2:8-10 " Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake yule ambaye kuja kwake ni mfano wa kutenda kwake shatani kwa uwezo wote na ishara ya ajabu za uongo na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea kwasababu hawakukubali kuipenda ile kweli wapate kuokolewa."
Jambo la kuhuzunisha ni kwamba wale wanao mfuata yule mpinga kristo wanadhani yakuwa wanaifanya kazi ya Mungu. Imeandikwa, Mathayo 7:22-23 "Wengi wataniambia siku ile Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako na kwa njina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi ndipo nitawaambia dhahiri sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu."

injili ya mafanikio ni kibiblia?

 Je wewe ni mchungaji,nabii askofu?umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kanisa lako likue? Sababu ya kweli ndani ya moyo wako ni nini? mashindano,kumtumikia MUNGU,kujipatia kipato kikubwa, kujulikana?imefikia hatua mpaka wachungaji na watumishi wengine wanatumia A.K.A! hii inachefua.
umeweka nguvu zote katika kuhubiri mafanikio kuliko ufalme wa MUNGU,na kazi aliyotuagiza BWANA YESU ,kama ilivyoandikwa katika Mathayo 28:19-20 "basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyo waamuru ninyi na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari." unapohubiri mafanikio tuu mwanzo mpk mwisho wa ibada Je, unataka kanisa lako likue ili ujisikie umefanikiwa? Je, unataka uheshimiwe na kuwa na ushawishi mkubwa? Je, unataka kuwa na mamlaka juu ya watu? Je, unatazamia kutajirika? Hizo zote ni sababu mbaya za kutaka kanisa lako likue.
Ukitaka kanisa lako likue ili Mungu atukuzwe kadiri watu wengi wanavyobadilishwa maishani kwa Roho Mtakatifu, basi hiyo ni sababu nzuri kabisa ya kutamani kukua kwa kanisa.Inawezekana ukajidanganya – kufikiri kwamba makusudi yetu ni safi na huku ni ya kimwili kabisa, tena ya kibinafsi.
Tunawezaje kujua ukweli wa makusudi yetu? Tunawezaje kujua kama kweli tunataka kujenga ufalme wa Mungu au kujenga ufalme wetu binafsi tu?
Njia moja ni kwa kufuatilia jinsi tunavyoitikia mafanikio ya wachungaji wengine. Kama tunafikiri makusudi yetu ni safi, kama tunafikiri kwamba kweli tunataka ufalme wa Mungu na kanisaLake likue, lakini tukigundua wivu mioyoni mwetu tunaposikia juu ya kukua kwa makanisa mengine, hiyo inadhihirisha kwamba makusudi yetu si safi. Huonyesha kwamba kweli hatujali sana kukua kwa kanisa, bali tunajali kuhusu kukua kwa kanisa letu. Mbona iwe hivyo? Kwa sababu makusudi yetu yana kiasi fulani cha ubinafsi.
Pia tunaweza kukagua makusudi yetu kwa kupima itikio letu la ndani tunaposikia kwamba kanisa jipya limeanzishwa katika eneo letu. Tukijisikia kutishika, hiyo ni ishara kwamba tunajali zaidi kuhusu ufalme wetu kuliko ufalme wa Mungu.
Hata wachungaji wa makanisa makubwa au yanayokua wanaweza kukagua makusudi yao hivyo hivyo. Wanaweza kujiuliza maswali kama haya: “Je, ningekubali kuanzisha makanisa mapya kwa kuwatuma na kuwaachilia kabisa viongozi muhimu na watu wa kanisani kwangu, na kwa njia hiyo kupunguza idadi ya washirika wangu?” Mchungaji anayepinga sana wazo hilo bila shaka anajenga kanisa lake kwa ajili ya utukufu wake. (Kwa upande wa pili, mchungaji mwenye kanisa kubwa anaweza kuanzisha makanisa mapya kwa ajili ya utukufu wake pia, ili aweze kujigamba kuhusu idadi ya makanisa yaliyozaliwa na kanisa lake.) Swali lingine la kujiuliza ni hili: “Je, nina mahusiano na wachungaji wa makanisa madogo au nimejitenga nao, nikijiona kwamba niko juu kuliko wao?” Au hili: “Je, nitakuwa tayari kuwa mchungaji wa watu kumi na mbili hadi ishirini katika kanisa la nyumbani, au hiyo itaniathiri katika ubinafsi wangu?”
mafanikio au baraka ni nyongeza, pia ni ahadi ya kila aaminiye.

NENO NI UZIMA Designed by 5gear Copyright © 2014-2015

Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.