Maombi siku ya tarehe 22/03/2014 Arusha.
-
Hivi ndivyo ilivyokuwa siku ya j'mosi ya tarehe 22/03/2014 katika viwanja
vya Sheikh Amri Abeid Stadium Arusha kwa ajiri ya maombi maalum kwa wakina
mama w...
VIDEO MPYA
SOMA BIBLIA KILASIKU
LEARN HEBREW LANGUAGE HERE
NYIMBO/VIDEO
SIKILIZA NYIMBO
Gospel Station TV
SIKILIZA RADIO
Follow us on twitter
Send Email:
Total Pageviews
Translate
Blog Archive
:PENDO LA MUNGU KWETU
SOMO :PENDO LA MUNGU KWETU. Haleluya… Jina la BWANA MUNGU LIPEWE SIFA... Karibu mpendwa nikushirikishe tafakari hii fupi ya leo kuhusu pendo la Mungu katika maisha yetu.Kwanza kabisa napenda ifahamike kwamba Mungu wetu atupenda kiasi ambacho hakuna yeyote atakaeweza kueleza namna Pendo la MUNGU kwetu lilivyo, Lakini ninachoweza kusema kwako ni kwamba Yeye Bwana Mungu ni PENDO.Hivyo upendo wake kwetu sisi ni upendo usio na mwisho,( Endless love).Mungu ameachilia upendo huu kwetu sote , yaani kwa wale wacha-Mungu wake, hata kwa wale wasio wacha-Mungu,akitoa Fursa ya pekee kwa wale ambao sio wacha-Mungu kwamba labda ipo siku moja wataokoka nao watakuwa mali yake kweli kweli. Tazama kama ni jua sote twapata,au kama mvua sisi sote twapata,Labda kama ingekuwa yeye Bwana Mungu ni mbaguzi katika Pendo lake,Basi ni dhahili kabisa kama ingekuwa ni mvua angewanyeshea kundi la watu Fulani kisha wengine awanyimwe. Labda pata picha hii ; Tuseme kwamba ndio waovu wote wapo Dar huko Mbezi.Na wema wote wapo Dar huko Magomeni.Kisha mvua ikawanyeshea watu wa Magomeni na watu wa Mbezi wasipate mvua, Una fikiri ingekuwaje ? Haleluya… Lakini Mungu wetu sio wa kiivyo. Tazama mfano wa NGANO na MAGUGU. Biblia inatueleza mfano mzuri sana hapa,Kwamba bwana shamba alipanda mbegu njema katika Konde lake/katika shamba lake, Baadae adui akaja akapanda MAGUGU.Kisha wale watumwa wake wakamuendea kumpasha habari ; Tunasoma Mathayo 13 : 27-30 “ Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing'oa ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu. ” Bwana wao alipotambua kwamba MAGUGU yamepandwa na adui katika shamba alilopanda NGANO akasema viache vikue kwa pamoja hadi mwisho, hii inamaanisha kwamba kama suala la kupata maji,au samadi,au kupaliliwa katika shamba hilo,basi NGANO na MGUGU vilikuwa vinapata vyote kwa pamoja pasipo kubaguliwa, Lakini hapo kuna mtego kwamba mwisho katika mavuno, ndipo zitatengwa NGANO na MAGUGU,Hapo ndipo MAGUGU yatafungwa na kuchomwa moto,Bali NGANO itakusanywa na kutunzwa. Sawa sawa na watu wote tuliopo chini ya mbingu hili,Kwamba tumeachwa tuendelee na mambo yetu mpaka mwisho. Yaani wale wenye kuokoka wataendelea na wale wanaokataa au wale waovu wote nao wataendelea na mambo yao,Lakini hapo mwisho ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno kwa wale wasiomtaka Mungu sasa. Wakikataa kabizi maisha yao kwa Bwana Yesu awe Bwana na Mwokozi wao,wakidhani kwamba wanafanya mambo yao kwa akili zao wenyewe,KUMBE WAMESAHAU MTEGO KWAMBA MWISHO KUTAKUWAKO NA KILIO NA KUSAGA MENO. Ili umpende Mungu ni lazima ufahamu namna ya pendo lake kwako,kwamba ujue Yeye alikupenda kwanza (1 Yoh 4 :19). Tazama bahari ,ambayo mwanzo wake unaweza kuuona lakini huwezi kuona mwisho wake,Huo ni mfano mdogo wa UPENDO wa Mungu kwetu sisi,Tena siwezi kuufananisha na upendo wa Mungu kwetu,maana upendo wa Mungu kwetu hauelezeki. Ukijua kwamba Mungu anakupenda sana kiasi kwamba hataki upotee maana amekupa nafasi tena labda utajerea kwake kwa TOBA. Maana anasema “ Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. ” Isaya 43 : 25-26 • Watu wengi siku ya leo hatupendani,kwa sababu tumemuacha Mungu kwa kusahau au kutokujua UPENDO wa Mungu kwetu. • Ukiona mafarakano katika familia ujue kiwango cha kumpenda Bwana Mungu kiko chini sana au kiwango hicho hakipo kabisa,Maana yeyote ampendaye Mungu,atampenda na jirani yake. Biblia inatutaka tupendane maana tukisema tunampenda Mungu kisha tunawachukia majirani zetu tutakuwa waongo( 1 Yoh.4: 20) Hivyo wito wangu kwako ni kuomba Neema ya kukaa katika pendo la Mungu,Nafasi ndio sasa ya kuifanyia kazi.Waweza kufanya toba kwanza na kisha omba neema hii. UBARIKIWE. BY MTUMISHI GASPER MADUMLA
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Bantu Tegemeo_Elohi(Official Video)
AFRICAN PRAYS SONGS
BLOG MBALIMBALI.
-
SEMINA MWEZI WA KUMI 2024 DAR ES SALAAM - HAPO CHINI NI AUDIO YA MAHUBIRI YANGU HUKO DAR ES SALAAM SEPTEMBA / OKTOBA 2024 1. ITOENI MIILI YENU IWE DHABIHU ILIYO HAI. SEHEMU 1 2.ITOENI MIILI YENU IW...
-
Injili Ruksa kuhubiriwa vilabu vya pombe - Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda tarehe 8 mwezi Wa tisa ametoa kibali kwa Watumishi wa Mungu wa Dini zote kuhubiri na kutangaza neno la Mung...
-
MIRIAM CHIRWA NIWEMA WAKE YESU - Ambatana nasi kwenye ukurasa wetu wa facebook kwa habari zaidi. www.facebook.com/gospelkitaa
-
Kubatizwa kwa moto uwakao - 15 - *==== SIKU YA 24 ====* *Kim Joseph: (2 Timotheo 3:1-5)* Wakati nikiomba kwa kunena kwa lugha, ghafla nilianza kulia machozi ya toba. Nilikuwa nimeshan...
-
Hivi kweli Allah anajua maana ya neno “Israeli”? - Ibrahimu alimzaa Isaka. Isaka alikuwa na wana wawili – Esau na Yakobo. Kwa sababu ya hila aliyofanyiwa Esau ya kunyang’anywa mbaraka, alikasirika sana...
-
-
-
Maombi siku ya tarehe 22/03/2014 Arusha. - Hivi ndivyo ilivyokuwa siku ya j'mosi ya tarehe 22/03/2014 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Stadium Arusha kwa ajiri ya maombi maalum kwa wakina mama w...
-
HATUA MUHIMU ZA KUKUA KIROHO - CHUKUA HATUA *MWINJILISTI PAUL* *Joshua 3:1-5* Joshua anawaambia wana wa Israeli kuchukuwa hatua ili kuweza kukabili safari iliyokuwa mbele yao kwa kuwa ...
-
-
-
Follow us on instagram
-
Follow us on facebook
Followers
Popular on NENO ni UZIMA
-
MUHTASARI Uhusiano wetu na Mungu, kama uhusiano baina ya mtu na mtu, lazima uwe na mawasiliano...
-
na mwl christopher mwakasege Je! Umewahi kujiuliza kwa nini wakati mwingine nguvu za Mungu zinakushukia kwa uwingi halafu baada ya mud...
-
FREEMASONS NA ILLUMINANT Hiki ni kitabu chenye siri nzito za Freemasons na Illuminanti. Utangulizi. Ni mpango wa Shetani kuangamiz...
-
Uponyaji Kutokana na Dhambi za Kingono, Miungano ya Nafsi, na Kutazama kwa Picha/Sinema Za Watu Walio Uchi Dhambi za Kingono ...
-
T A B IA 6 ZA LAZIMA KATIKA KUJENGA USHIRIKA AU MAHUSIANO MAZURI NA MUNGU, MKE /MUME, JAMII AU WATU WOTE UTANGULIZI · Mwanadamu sio kis...
-
KUUFAHAMU NA KUUTAWALA ULIMWENGU WA ROHO KWA NGUVU YA MAOMBI Mwalimu, Mgisa Mtebe 0713 497 654 2. KUUFAHAMU NA KUUTAWALA ULIMWENGU...
-
Sifa Na Kuabudu Yule mwanamke akamwambia [Yesu], ‘Bwana, naona ya kuwa u nabii. Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya...
-
"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu y...
-
BWANA YESU Asifiwe ndugu msomaji, leo tupitie somo kuhusu Upendo wa Kiungu (AGAPE) na sifa zake. 2WAKORINTHO 13:1-13. Upendo wa Kiu...
-
ROHO YA HEKIMA NA UFUNUO May 2, 2015 Na: Patrick Sanga Salaam katika jina lake BWANA Yesu Katika Waefeso 1:17 Biblia inasema ‘Mun...
No comments:
Post a Comment